CHADEMA, huu ni wakati wakuwa Radio na TV ya Chama

DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Ninyi ni Chama kikuu Cha upinzani na Chama mbadala wa CCM, kuwa na media yenu itasaidia sana kueneza Sera na elimu mbalimbali kwa wanachama na wananchi. Uenezi wa Chama unahitaji vyombo vya uhakika vya habari.

Ni aibu kwa Chama Kikuu, kikongwe kama hiki, kutoa matamko yake kwenye Twitter huku mkijua wanachi wengi wako vijijini na hawana Access na hivyo vitu.

Kama tulivyochangia uendeshaji wa Kesi ya Mwenyekiti mbowe na matukio mengine, hatushindwi kuchangia na kufanikisha uwepo wa radio na Tv ya Chama, if need be.

Leo vijana wadogo kqma Zamaradi ana Tv, Majizo ana Tv, Why not CHADEMA.
Hili pia linawahisu ACT-Wazalendo.
 
Wapinzani wao chama tawala watakubali kuwapa masafa? Maana serikali ni ya ccm, labda kama dhana ya masafa ya umma hapo itabidi wawe nayo tu. Hawana hata pro media za kueneza sera zao
 
Wapinzani wao chama tawala watakubali kuwapa masafa? Maana serikali ni ya ccm, labda kama dhana ya masafa ya umma hapo itabidi wawe nayo tu. Hawana hata pro media za kueneza sera zao
Wangetimiza na kufuata matakwa na vigezo vyote vya kuanzisha TV & Radio, then wakikwamishwa ndio warudi kwa wananchi..sasa zingine Watz tupunguze kulalamikalamika ,tujifunze kufuata taratibu na kuchukua hatua na pia tupunguze HOFU na hisia hasi
 
Ni wazo zuri lakini utekelezaji wake ni mgumu sana kwa mazingira yetu ya kisiasa.
 
Hili neno!, angalia hili ni bandiko la lini Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... hivyo alipokuja Mwamba wa Kaskazi nilisema Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Ushauri huu niliwapa toka 2012!, asante sana kwa kuliona leo 2023!.
Mungu ibariki Chadema iweze!
Mungu ibariki Tanzania

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…