Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Katika nchi nyingi za demokrasia halisi uongozi wa vyama vya siasa huwa unabadilishwa punde tu baada ya matokeo ya uchaguzi, hicho ndicho kipindi kizuri cha kufanya tathmini ya uongozi kutokana na performance baada ya uchaguzi.
CHADEMA kuwa inafanya mabadiliko ya uongozi mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu au wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi ni kosa kubwa la kimkakati linalowagharimu sasa.
Kinachopaswa sasa ni kufanya mabadiliko ya haraka ya katiba ya CHADEMA kufanya ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kuwa miezi miwili baada ya uchaguzi mkuu mkuu wa Taifa.
Uchaguzi uliopo uendelee kama kawaida, Mbowe na Wenje wajitoe kwa sasa lakini uchaguzi mwingine wa chama ufanyike January 2026 baada ya uchaguzi mkuu wa taifa na huo ndio utaratibu kwamba uchaguzi wa chama unafanyika muda mfupi baada tu ya uchaguzi mkuu.
Kwa mabadiliko haya wanachama wa CHADEMA watakuwa na kipindi cha kutosha cha mwaka mmoja kumpima Lissu, wakiona amewafaa katika uchaguzi mkuu wa 2025 watamrudisha tena January 2026, wakiona hatoshi watamuondoa kumrudisha Mbowe na timu yake au kuchagua watu wengine kabisa ambao wataenda nao mpaka uchaguzi wa 2030. Hapo kila mtu anakuwa ni mshindi bila kuigawanya au kuisambaratisha CHADEMA.