Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Kinjekitile: mheshimiwa Gavana
Tunaomba tuandamane
Gavana: Oh karibu
Kinjekitile: Ahsante, kama ulivyosikia, tunataka tuandamane
Gavana: Bwana Kinje, kwanini
Mnataka kuandamana?
Kinjekitile: Tumechoka kuwa
Watumwa wenu, tunahitaji
Uhuru kamili, alafu mmenyonga kiongozi wetu Nduna Nkomanile.
Gavana: Ok, ngoja niangalie ratiba inaendaje na usalama wa watu na mali zao, kuona kama kuna usalama ili kuepusha uvunjifu wa amani
Kinjekitile : Sawa mkuu
**************************************
Gavana : Uchunguzi unaonyesha hayo maandamano yenu yana viashiria vya uvunjifu wa amani. Kwa hiyo hayataruhusiwa.
Kinjekitile : Basi poa, Nashukuru.
(Miaka 119 baadaye, kwenye magazeti)
GAVANA AWATAKA MANYAPARA KUONGEZA UZALISHAJI, WATUMWA WAZEMBE KUKIONA CHA MOTO.
NB: Si kila maandamano yanahitaji kuratibiwa (kupangwa) au kuombewa kibali hususan maandamano yanayowalenga wale wale wanaotakiwa kutoa kibali!.Unless kama ni maandamano ya tokomeza kansa ya uzazi, maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia na maandamano ya kuunga mkono vita dhidi ya kansa yanayoratibiwa na Ocean road chini ya Wizara ya afya!.
Siku chache zilizopita tumeshuhudia maandamano ya watu huko Lulembela ambapo wananchi wenye hasira kali walionyesha kuchoka juu ya jambo lililokuwa likiwatatiza kwa muda mrefu. Pia tumeshuhudia matukio mengi tu ikiwemo wananchi wenye hasira kali kufunga njia kutokana na ajali nk. Kwa mazingira kama hayo, CHADEMA ilipaswa kuchukua 'Moment' na ku 'benefit from it' wakati ule ule ambapo mwili wa Kibao (Mungu amrehemu) ulipatikana, Hapo hapo CHADEMA na wananchi wote wanaopinga vitendo hivyo wangeweza kuungana kukemea vikali matendo hayo maovu katika jamii, ingewezekana wasingezika mpaka pale majibu ya kueleweka yatakapopatikana!
Kitendo cha kutangaza maandamano siku tofauti na ile, ni sawa na kuwaambia watu waliopo msibani wasilie msibani, bali watapata nafasi kulia vizuri wakiwa makwao!
Kitendo cha Mbowe kutuliza hali kisha baadaye kuja na plan ya kuweka tarehe rasmi na njia ya maandamano alikosea, alishindwa ku' Take advantage of the moment'. Kutangaza route na tarehe ya maandamano ni sawa na kuuza ramani ya vita, hata 'junior army officer' angeweza kuyadhibiti kirahisi sana.
Al in all : Mbowe amefanya kazi kubwa, na kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kutuma ujumbe kwa walengwa.