Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hata kwa Usimamizi huu huu mbovu (Japo siufagilii), Chadema inaweza kuibuka na ushindi wa kishindo ikiwa Wananchi wataamua kukataa dhuluma.
Wakati wa Kikwete ambaye alikuwa Rais, Amiri Jeshi na Mwenyekiti wa CCM kama hawa waliopo leo.
Chadema ilishinda kwa kishindo kwenye maeneo mengi, likiwemo Jimbo la Chato ambalo mbunge wake alitokea CCM na alijulikana kwa jina moja la Magufuli, ambako kwenye Uchaguzi wa 2014 Chadema ilizoa viti vyote vya uenyekiti kikiwemo kijiji alichoishi Magufuli Mwenyewe.
Tukirudi nyuma zaidi ya hapo Augustino Mrema alimshinda Checkbob Sisco Mtiro wa CCM kwenye Jimbo la Temeke na kuwa Mbunge, zamani vituo vya kupigia kura vilikuwemo hadi kwenye kambi za Jeshi, Polisi Ufundi na Twalipo, Kwenye vituo hivi ambavyo wapiga kura wengi walikuwa ni Askari Mrema alishinda kwa kishindo.
Hivyo basi ikiwa Chadema ikasimama na Wananchi na ukizingatia dhiki na ugumu wa Maisha uliosababishwa na ccm, itashinda kila mahali.