CHADEMA ilikuwa na wabunge sita wa kuchaguliwa mkoani Kilimanjaro sasa amebaki Mbowe peke yake

Kama watu wasio na kazi wanaweza kweli kujaa mtandaoni na kuwapiku watu wanaolipwa buku 7 na chama serikali, nani anawadanganya mioyo yao? Mimi si Chadema lakini natetea Chadema kwa sababu chama cha siasa kinachoweza kuitetemesha serikali ya kidikteta kama hii ya kwetu lazima kiwe kinapendwa!

Fikiria misukosuko wanayopata wana Chadema kuanzia kutekwa, kuteswa, kufungwa magerezani, kupotezwa, kumiminiwa risasi na hata kuuawa na bado chama kikabakia tishio kwa watawala. Sumve 2015 , sisi watazamaji tunaochungulia kutoka mbali yanayoendelea nchini tunajiuliza huu ujasiri Chadema wanaupata wapi?

Leo hii kwa uwezo walio nao Chadema tunaona jinsi serikali ilivyo na hofu hadi viongozi kuzikimbia ofisi zao kwenda kujifukiza vijijini wakidai wanapambana na corona.Tunaona CCM ilivyoingiwa na woga hadi kuvitumia vyombo vya dola katika juhudi za kuidhibiti na kuisambaratisha Chadema lakini wapi, Chadema hiyoo inadunda!

Au Sumve 2015, naomba nikuulize swali dogo tu...je unaamini toka rohoni kwamba tunaoupinga ubeberu wa serikali yetu kweli tunalipwa na Mbowe? Au na wewe unaamini kwamba sisi si wazalendo na tunatumiwa na mabeberu? Acheni woga, toeni uhuru watu wachague viongozi wanaowataka tuone kama CCM itaambulia chochote.

Watu hampendwi lakini mnag'ang'ania madaraka kwa nguvu huku hamna sifa tena wala uwezo, hekima na busara...je mtawaua Watanzania wangapi?
 
Lumumba buku7 vs Ufipa buku10, sijui hii vita itaisha lini.
 
Asante kwa taarifa.
Mhe. Freeman Mbowe amethibitisha kuwa Mbunge imara ambaye amekataa kuwasaliti wapiga kura waliompeleka Mjengoni Dodoma.
Hongera sana Freeman Mbowe
Hivi wewe ukiwa na mgodi wako unachimba dhahabu halafu wale vibarua wanaokuchimbia mgodi wako wakikukimbia wakaenda kuchimba kwa jirani yako nawewe utawafuata uache mgodi wako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa bado upo usingizini. Ukiendelea kushabikia chadema na haya matumaini hewa. Utakuja kupata kiharusi Oktoba, 2020 kwa mshtuko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hujawaza vizuri hata kabla ya uchaguzi 2015 chadema ngome yake ilikuwa kaskazini, si kwasababu ya wabunge bali kwa sababu ya wanachama na wafuasi wake....hao wanachama na wafuasi bado wapo.....na wapo wakugombea wengi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote walikuwa Mayuda hakuna cha ajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mag3 mdogo wangu umeeleza ukweli mtupu, tukiacha ushabiki tukairuhusu akili kutumika ipasavyo utaona kabisa kati ya CHADEMA na CCM, wapinzani wanapendwa! CCM sasa hivi inapumua kutumia oxygen ya vyombo vya usalama na tume ya uchaguzi bila polisi au wizi wa ma-DED CCM haifikishi saa 6 inakuwa imeshabwagwa! Kudhihirisha CHADEMA wanapendwa angalia watu walivyojitoa kuwachangia kipindi wameamuliwa kufungwa kwa dhuluma!
 
It's very sad!, na Mhe. Mbowe mwenyewe, kwa uchaguzi wa mwaka huu hapo October, ...
Naomba nisimalizie, sitaki ugomvi na watu wa Chadema humu!.

P
Bagheshi Paskali tuache ushabiki maandazi na undezi, ukweli CHADEMA kiko mioyoni mwa watu! Kwa misukosuko kinayopitia kingekuwa chama cha Mbowe tu kingekwishakufa, watu wanafikia kutumia vyombo vya dola kuvunja mikono akinamama? CCM bila Oksijeni ya polisi na tume ya uchaguzi hawafikishi saa 6!
 
We jamaa bado upo usingizini. Ukiendelea kushabikia chadema na haya matumaini hewa. Utakuja kupata kiharusi Oktoba, 2020
Mbona unanipakazia ndugu yangu, je ni matumaini gani unayaongelea hapa? Chadema katu haiwezi kupambana na dola na hata Bashite tu akitaka anaweza kuisambaratisha chadema akiamua.

Je unadhani wananchi wote wa Korea Kaskazini wanampenda Kim Un Jung? Je unadhani wakazi wote wa Mkoa wa Dar wanampenda Bashite? Sasa matumaini yangu yatoke wapi?

Na hapo sijamsahau mkuu wa malaika...nihurumie ndugu yangu kipande! Watanzania wanalia na kama unavyoona wataendelea kulia hadi machozi yawakauke!

Vyoyote vile chadema isambaratike isisambaratike upinzani dhidi ya adui namba wani wa taifa, CCM, itakua na kukua na kukua hadi siku itafika Watanzania kwa ujumla wao watasema imetosha!

Siku hiyo ole wako na wenzio, hakutakuwa na cha mswalie mtume!
 
Yaani hata na Mbowe leo angeenda CCM wala hakuna ambacho kingebadilika/wapiga kura sio wajinga wanajua wakifanyacho.
 
Afrika ni kichekesho kikubwa sana, yaani Rais ndiye anaehamua nani awe mpinzani na ni chama kipi kiwe mpinzani na siyo wananchi!
 
Afrika ni kichekesho kikubwa sana, yaani Rais ndiye anaehamua nani awe mpinzani na ni chama kipi kiwe mpinzani na siyo wananchi!
Africa hua ni noma sana,Kinana alishawahi kutumwa kwenda kutibiwa India,Mbunge mwingine alishashukuru kwa kujengewa reli kwa kiwango cha Lami.
 
Hivi wewe ukiwa na mgodi wako unachimba dhahabu halafu wale vibarua wanaokuchimbia mgodi wako wakikukimbia wakaenda kuchimba kwa jirani yako nawewe utawafuata uache mgodi wako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali sahihi ni kuwa ''Kama wewe una mgodi, lakini Wasimamizi, kwa maana ya Foremen wakaondoka, wakakuacha na vibarua wako, kwa maana ya Wapiga Kura, unafanyaje''?
Jibu lake ni kuwa unaendelea kupiga Nazi huku ukiwapandisha baadhi ya Wapiga Kura kuwa Wasimamizi
 
Nani kakudanganya mioyo ya watu iko CHADEMA?
Matendo ya wakubwa wenu huko Lumumba na dola, ndio yanayosema waziwazi.
Waangalieni wanavyohangaika kwa hila, jasho na damu, kuiua CHADEMA kila kukicha, bila ya mafanikio. Wakubwa wenu wanahangaika sana kulazimisha kuupata mvuto uliyoko kwa wapinzani hasusan CHADEMA.
Hiyo ndio historia yao chafu malumumba.
Mvuto kwa wananchi HUJA kwa kuwajali, kuwatendea haki na kulinda utu na uhuru wao mbele ya Sheria kwa mujibu wa Katiba. Vitisho na ubabe kwa waTz ambavyo baadhi yenu, bila HAYA mnajivunia, ni ushetani unaozidi kuwafanya muwe chukizo mbele yao.
Ngonjera na makelele mengine kama ya akina Ndugai au hizi kwako KAMWE hazitakujawasaidia.
Tutaonana october hii. AMEN
 
Kwenu nyie corona ni siasa. Tz yenda kombo.
 
Ni sawa. Nilichokua najaribu kukionyesha ni kwanini mbowe hawezi kuondoka Chadema kama wengine ni kwasababu ana maslahi napo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…