SI KWELI CHADEMA imekiri kwamba wapo tayari kwa maridhiano yatakayo fanyika.

SI KWELI CHADEMA imekiri kwamba wapo tayari kwa maridhiano yatakayo fanyika.

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Mkuu wa Idara ya habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Gervas Lyenda ni amesema Chama chake kipo tayari kushiriki kwenye mchakato wa maridhiano ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na amani na utulivu wa kisiasa wa kudumu.

Lyenda amebainisha hayo wakati akifanya mahojiano na chombo kimoja cha habari Jijini Dar Es Salaam, suala ambalo limepokelewa kwa maoni mseto na baadhi ya Wananchi wakiwemo wanachama wa Chadema na baadhi ya wachambuzi wa siasa, wengi wakiunga mkono kauli hiyo kwa maslahi ya Umma na umoja wa Kitaifa.

"Hiki alichokisema Bwana Lyenda kando ya kwenda kinyume na baadhi ya Viongozi wake wakuu ni suala linalotakiwa kuungwa mkono, ni kitendo cha kikomavu katika siasa na demokrasia kinachopaswa kuungwa mkono na kila mmoja wakiwemo wanachama wa CHADEMA wanaolipenda Taifa lao na wananchi wake." Amesema Bi Asha Manase, Mwanachama wa Chadema kutoka Jijini Dar Es Salaam.

Aidha kwa nyakati tofauti kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii baadhi ya wachambuzi wa siasa akiwemo Bw. Said M. Baruan, amebainisha kuwa kauli ya Bw. Lyenda huenda ikawa inatuma ujumbe kuwa ndani ya Chadema kuna mpasuko, wengi wakionekana kutounga mkono kauli na maazimio ya Viongozi wakuu wa Chama hicho cha siasa.

Baadhi ya machapisho mtandaoni yameelekeza pia pongezi zao kwa Mkuu huyo wa Idara ya habari CHADEMA, wakisisitiza umuhimu wa wanachama wa Chama hicho kufunguka na kutafakari kauli hiyo ya Bw. Lyenda na wafahamu kuwa siasa si ugomvi wala si jukwaa la uchochezi na uchonganishi.

"Rai kwa Viongozi wote wa Chadema, waige mfano wa Bw. Lyenda katika kutoa kauli zao. Wananchi tunataka kauli za kuleta matumaini si kukatisha tamaa, tunataka kauli zenye kuleta mshikamano na sio kubomoa ama kuharibu." Limesema andiko linalosambaa kwa kasi katika mtandao wa WhatsApp.
624486428_122444747636001477_8996229432130935071_n.jpg
 
Tunachokijua
kumekuwapo na chapisho lianosambaa kwenye mitandao ya kijamii likibainisha kuwa CHADEMA ipo tayari kwa ajili ya maridhiano. chapisho linasomeka likiwa na ujumbe ufuatao.

Mkuu wa Idara ya habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Gervas Lyenda amesema Chama chake kipo tayari kushiriki kwenye mchakato wa maridhiano ili kuhakikisha Tanzania inakuwa na amani na utulivu wa kisiasa wa kudumu.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Ufuatialiaji umebaini kuwa Taarifa inayodai kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania, CHADEMA, kimekubali kushiriki katika mchakato wa maridhiano, Si ya kweli.

Ufuatiliaji wa kina umebaini kuwa hakuna ushahidi wa kuhusiana kwa mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA kufanya mahojiano na vyombo vikubwa vya habari nchini Tanzania kuhusu masuala ya maridhiano.

Aidha hakuna chombo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo. Pia taarifa hiyo Potoshi Katika imeshindwa kueleza ni wapi Mkuu wa idara wa Mawasiliano wa CHADEMA amefanya mahojiano na chombo kipi cha habari.

Pia ufuatiliaji Zaidi kwenye kurasa rasmi cha CHADEMA unaonesha, Idara ya Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje ya CHADEMA haijatoa tamko lolote rasmi kuelekea mwaka 2026 linaloashiria mabadiliko ya msimamo wao kuhusu maridhiano nje ya yale yaliyokwishaelezwa huko nyuma.

Gervas Lyenda kupitia ukurasa wake wa X pia amekanusha kuhusu taarifa hiyo kwa kuandika;

Puuzeni hivi vipeperushi. Msimamo wa Chadema upo wazi. Na unafahamika na umma.
Back
Top Bottom