SI KWELI CHADEMA imeondolewa Democrat Union of Africa DUA

SI KWELI CHADEMA imeondolewa Democrat Union of Africa DUA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Salaam wanajukwaa
Nimekutana na hii taarifa kutoka mtandao wa X kwamba CHADEMA imeondolewa kwenye huu umoja wa DUA, Democrat Union Africa, na inaonekana taarifa pia imechapishwa na JamiiForums lakini kwenye account zake sijakutana nayo, naomba kufahamu uhalisia wa hii wakuu.
SIKWELI_JF_DUA (1).jpg

SIKWELI_JF_DUA (2).jpg
 
Tunachokijua
Democrat Union of Africa (DUA) ni muungano wa vyama vya siasa vya mrengo wa kati katika Bara la Afrika ikiwa ni chombo shirikishi cha kikanda cha Muungano wa Kimataifa wa Demokrasia.

DUA hutoa jukwaa kwa vyama wanachama, wataalamu wa sera, wabunge na makundi maalum kukutana na kubadilishana mawazo ya sera, mbinu bora za kampeni na kushinda uchaguzi na taratibu za kukusanya pesa. Pia ni jukwaa muhimu la kuunda ushirikiano wa karibu wa vyama wanachama kupitia mitandao.

Vyama vya siasa ambavyo ni wanachama wa DUA vinatoka katika nchi zaidi ya kumi na tano ambapo kutoka Tanzania Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA ni miongoni mwa vyama wanachama wa umoja huo.

Kumeibuka taarifa kuwa CHADEMA imeondolewa katika umoja wa vyama vya siasa vya mrengo wa kati barani, Afrika Democrat Union of Africa (DUA)


Je ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haikutolewa na DUA, aidha kwa mujibu wa tovuti ya DUA bado CHADEMA inatambuliwa kama mwanachama wa umoja huo wa vyama vya siasa barani Afrika.

Vilevile Barua inayosambaa mtandaoni imebainika kuwa imetengenezwa na wapotoshaji wenye nia ovu kwani ina mapungufu mengi yanayoitofautisha dhidi ya barua rasmi ambazo hutolewa na DUA. Moja kati ya mapungufu hayo ni pamoja na kutofautiana kwa mwandiko (fonts), ambapo mwandiko uliotumika si ule unaotumiwa na DUA katika barua rasmi.

Hata hivyo barua hiyo haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya DUA bali uwepo wa taarifa ya kukanusha barua hiyo yenye lengo la kupotosha umma.

"DUA inatoa rai kwa umma kupuuza barua potofu inayosambaa kuhusu chama chetu pendwa na cha thamani, CHADEMA Barua hiyo bila shaka imetoka kwa maadui wa CHADEMA na Demokrasia, na siyo kutoka DUA. Tafadhali ipuuzeni kabisa barua hiyo"

Pia chapisho ambalo linadaiwa kuwa limetolewa na JamiiForums si la kweli kwani halifanani na machapisho rasmi ya maudhui ya kisiasa ambayo huchapishwa katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, utofauti wa mwandiko (fonts), uwepo wa alama ya zaidi upande wa juu kulia pasipo na maudhui zaidi (slides) vinadhihirisha kuwa chapisho hilo si halisi na halikuchapishwa na JamiiForums tarehe 23 Disemba 2024.​
Back
Top Bottom