- Source #1
- View Source #1
Wakuu vipi hili limakaaje huko?
- Tunachokijua
- Madai
Oktoba 02, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii imesambaa taarifa inayoambatana na barua yenye utambulisho wa Chama cha demokrasia na maendeo (CHADEMA) kuwa imesitisha kampeni ya "No election 29". Taarifa hiyo inasambazwa pia kupitia baadhi ya grafiki za vyombo vya habari ikiwemo cha Millard Ayo.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupitia utafutaji kwa njia ya mtandao, imebainika kuwa barua hiyo yenye utambulisho wa CHADEMA, ni ya kughushi na haijachapishwa na chama hicho kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii ikiwamo mtandao wa X.
Sambamba na hilo CHADEMA haina kampeni inayoitwa "No election 29" na badala yake kampeni yao inajulikana kwa jina la No reforms No election ambayo wamekuwa wakipaza sauti kwa ajili ya kuhitaji mabadiliko katika mifumo na sheria za uchaguzi ili kupelekea uchaguzi huru.
Aidha grafiki zinazotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi na hazijachapishwa na vyanzo hivyo kama inavyoonekana. Mathalani grafiki yenye utambulisho wa Millard Ayo licha ya kuwa haijachapishwa katika kurasa rasmi za chanzo hicho lakini pia ina baadhi ya mapungufu ikiwemo kutumia aina tofauti ya mwandiko ukilinganisha na grafiki halisi.