SI KWELI CHADEMA imethibitisha kufanya mipango ya kuwakusanya wananchi mahakamani kufanya fujo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2






​
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na barua inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kuwa ni taarifa kwa umma iliyotolewa na Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ikitaja kutoa Ufafanuzi juu ya sauti iliyomuhusisha makamu mwenyekiti wetu chama na kudaiwa kupanga kufanya fujo mahakamani.

Aidha imetoa wito kwa wananchi wote, wanachama, wanaharakati, vijana, wanawake, wazee, pamoja na jamii ya kimataifa, 'tuendelee kushirikiana katika matukio yote ya chama na tuzidi kuja mahakamani kwa wingi'

Je, barua hiyo ni halisi imetolewa na CHADEMA?


Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Keyword Search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani haijatolewa na CHADEMA, bali imeghushiwa na wapotoshaji.

Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kutengenezwa na wapotoshaji kwani hazijachapishwa na vyanzo hivyo (Jambo TV, Mwananchi) kama inavyoonekana.

Aidha grafiki hizo zimebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo matumi ya fonti zisizotumiwa na vyombo hivyo, pamoja na kukosekana kwa tarehe kwenye grafiki ya Mwananchi kama ilivyo katika taarifa zake rasmi.​

Attachments

  • 1758202738619.jpeg
    65 KB · Views: 28
  • 1758202755347.jpeg
    52.1 KB · Views: 30
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…