Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Baadhi yetu tulikataa na tunaendelea kukataa kutambua mchakato huu wa Katiba Mpya. Tulianisha sababu za kufanya hivyo mapema kabisa Mwenyekiti wa CCM alipotangaza kuanzisha mchakato huu; na tuliweka zaidi bayana za kuukataa tulipopata tu mswada wa ile sheria ya kupitia mchakato wa Katiba. Tulionesha wakati ule kuwa Mkataba huu uko fundamentally biased and inherently flawed in favor of the ruling party.
Juzi nimeona Mtaalamu wa Katiba Prof. Maina naye amejia juu muundo wa baraza la kutunga Katiba ambapo wabunge wote na wajumbe wa BLW la Zanzibar ni wajumbe ( na hivyo kuipa CCM overwhelming majority) ndani ya mchakato huo. Tulipokataa mchakato huu kwa sababu zilizo wazi - kwamba umelengwa kuinufaisha CCM na kufanya matamanio ya watu kuhusu katiba mpya kuwa ya njozini zaidi. Wengine japo tuna michango mizuri tu kuhusiana na rasimu ya Katiba tumekataa kuitoa kwa sababu kutoa michango hii kwa tume ya Warioba ni kuipa uhalali ambao haina. Tulikataa tume na mchakato wenyewe kuwa vimepora mamlaka ya wananchi kuandika Katiba yao.
Hata hivyo chama kikuu cha upinzani ambacho ndicho kilikuwa kinapigania Katiba Mpya kwa muda mrefu kikarukia trela hili la "Katiba Mpya" huku viongozi wake wakitoa pongeza kuwa ni uamuzi mzuri. Na hata walipoonesha tatizo kidogo waliitwa wakawekwa sawa na baadaye kuukumbatia mchakato huu. Sasa mchakato umefika mahali ambapo tunaelekea kuunda Baraza la Kutunga Katiba wapinzani wanaanza kujia juu na wasomi wanaanza kuja juu - rejea jinsi watu wamelalamikia mabadiliko ya sheria hiyo kwa mara nyingine tena. Ni kana kwamba wapinzani walitegemea CCM na serikali yake watengeneze mchakato utakaowafurahisha wapinzani ili uwe halali!
Sasa inaonekana CCM haibadiliki na wala haitatarajii kubadilika; wapinzani walishavua nguo kuoga na sasa maji yanaanza kuwamwagikia wanataka kutoka bafuni! "Oh maji ya moto!"; kana kwamba hawakujua maji ni ya moto kwa sababu tunajua nani anayafungulia.
Maoni yangu ni kuwa CHADEMA imejiweka kwenye kona mbaya; kona ambayo sijui itatoka vipi:
a. Wameshakubali mchakato huu na wameupa uhalali kwa kushiriki kwao. Tayari wameshikiri kiasi cha kufikia kuunda mabaraza ya kupitia rasimu ya Katiba na kukusanya maoni. Kimsingi, CHADEMA wamekubali uhalali wa mchakato huu. Je sasa wanaweza kulalamika kuwa hauna haki? Je hawakujua kuwa hauna haki toka mwanzo? au walitarajia nini wakati toka mwanzo mchakato ulionekana - kisheria - kuipendelea CCM?
b. Wanalazimika kutumia nguvu ya ushawishi kwa wananchi ili waone matatizo na hakuna mahali pazuri pa kufanya hivyo kama Bungeni. Hata hivyo, tayari tumeshaona kuwa Bungeni nafasi hiyo hawapewi tena na hata wakipewa zinatumika kila mbinu kuzima hoja kama tulivyoshuhudia hivi karibuni. Kutumia Bunge kurekebisha mchakato huu ni zoezi gumu kulitekeleza.
c. Wanaweza kuamua kuendelea na mchakato na kutumia nguvu nyingi kuendesha kampeni wakati wa kura ya maoni kukataa Katiba Mpya. Kwa baadhi ya watu option hii inaonekana ni nzuri na yenye mantiki. Hata hivyo tatizo liko pale pale kama nilivyoonesha wakati mchakato huu unafukiziwa ubani Bungeni; sheria inasema rasimu ya katiba Mpya itapita kama itapata asilimia 50 au zaidi (simple majority) ya watu wa Zanzibar na Tanganyika ambao ni wapiga kura. Kimsingi, CCM haiitaji kura hata moja ya wapinzani kupitisha kwani wanahitaji kuhamasisha kura za wana CCM na walio watu huru (independents).
Hili pia lilikuwa tatizo kubwa kwangu kwa sababu fikiria kuwa kufanyia marekebisho Katiba ya sasa haiwezekani isipokuwa mpaka 2/3 ya wabunge wa bara na visiwani wakubali (yaani zaidi ya asilimia 66). Kwa maneno mengine ni vigumu kufanyia marekebisho kipengele cha Katiba ya sasa kuliko kuamua kupitisha Katiba mpya!
Ukiangalia sana utaona kuwa CHADEMA iko mahali pagumu sana; sijui ina options gani nyingi zaidi ya kukubali kwenda na mawimbi tu? Hawawezi kulazimisha mabadiliko ya sheria, hawawezi kuzuia mchakato kuendelea, na hawawezi kuzuia Katiba Mpya kupita! Sasa wafanye nini? wakubali tu matokeo ya kukubali mchakato huu. Sivyo?