CHADEMA ina "Options" gani kuhusiana na Mchakato wa Katiba Mpya?

CHADEMA ina "Options" gani kuhusiana na Mchakato wa Katiba Mpya?

CCM haijatengua maoni ya mtu. CCM ingetaka kufanya hivyo hata rasimu isingekuwa na sura iliyo nayo.

Inachofanya CCM ni kushiriki mchakato kwa kutoa maoni yake kwa kutumia fursa waliyopewa na wananchi ya kuwawakilisha. Watanzania wengi wameipa CCM fursa ya kuwawakilisha kwa njia ya Bunge na mabaraza ya Halmashauri.

CCM kutokupigania maslahi ya wananchi hawa ni KUWATELEKEZA watu walioiamini.

Katika mchakato wa Katiba CCM ina jukumu la kipekee kwamba ndio chama chenye dhamana ya kuliongoza Taifa kuipata Katiba nzuri. mambo yakienda kombo, CCM inabeba lawama.

Umebugi men. CCM hata mchakato wa katiba uliwahusu wanachama tu na jhilo unalifahamu. Mbaya zaidi hata wanachama walipewa waraka si mawazo yao, labda kama chama kina wanachamo mazombie (hawana mawazo) Tafadhali sana ebu tafakari huo waraka wa katiba ni wananchi gani hata walio wa ccm wana maslahi nayo.

Wenye maslahi

1. Kinana

2. Jk

3. Wenye CCM yao (mafisadi na watawala wahalifu waliotangulia)

Wewe Mheshimiwe HAUMO
 
Mchakato wa Katiba haujaanzishwa na Mwenyekiti wa CCM. Umeanzashwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

As usual, Mwanakijiji yuko katika ulaghai...
ZM tunaomba utofuati ya hilo ulilosema.

Ni juzi tu akiwa Kanda ya Ziwa kwa ziara ya kiserikali akaishia "kupokea wanachama {wapya ?}"

Muhumu zaidi ni kuwa CCM haiwezi na haitakaa itokee iathubutu kushiriki mchakato wa kuandika katiba huru na sawa ya Tanzania.

CHADEMA walikosea, mimi naamini hivyo na nilishaweka bayana msimamo wangu kama na MMM alivyokumbushia hapa.
 
CHADEMA walikumbwa na ugonjwa wa "nia njema" wakasaini mkataba na shetani.

Hima sasa wahakikishe wanatafuta exit door iko wapi kwa usalama wao na Tanzania
 
Ndio maana watu kama Wassira wanatoa kauli za matusi ya rejareja kwa kweli...
 
CCM & Co (Mwenyekiti na NEC) hawakuwa na nia dhabiti ya kuwaletea watanzania Katiba yao bali walikuwa na nia ya kutengeneza zaidi katiba ya wanaCCM.Sababu pamoja na watu wengi kulalamikia uchaguzi wa kuingia kwenye mabaraza ,Tume ya Katiba haikuonyesha makali yake sababu muajiri wao ni Serikali ya CCM na haiwezi kwenda kinyume.Hivyo basi kwa wengi wetu tuliotaka UHURU kwenye Utengenezaji wa katiba ya Tanzania itakayowahusu watanzania basi kungekuwa na uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa kusikilizwa.Ni bahati mbaya sana vyama vya upinzani hawakuliona hilo mapema, na hata wangekataa bado uwingi wa wabunge waCCM bungeni ungefanikisha lengo lao.Cha msingi kwa sasa wanachotakiwa kufanya vyama vya upinzani siyo Chadema tu ni kuwaelimisha raia wa Tanzani ili kuikataa rasimuhiyo.Ni bora tubaki na katiba ya zamani kuliko kuingia kwenye katiba itakayotugawa kwa mlengo wa ITIKADI.
 
Back
Top Bottom