Uchaguzi 2020 CHADEMA inahitaji political strategists kuishinda CCM

Uchaguzi 2020 CHADEMA inahitaji political strategists kuishinda CCM

KIJITOSAMAKI

Member
Joined
Sep 2, 2020
Posts
29
Reaction score
16
CHADEMA inahitaji wataalamu wa stratejia ya siasa (Political Strategists) kuweza kuitoa CCM madarakani kwa urahisi. Vyama vikongwe na vyenye dola kama CCM vinahitaji kufanyiwa mkakati maalumu ambao hauhitaji nguvu. Kama ningepewa fursa ya kutoa ushauri wa kimkakati wa kuitoa CCM ningeshauri ifutavyo:-

1. Kwa wakati huu 2020 - 2025 Chama kijikite katika kuunga mkono mikakati muhimu ya kitaifa inayofanywa kuinua uchumi wa Taifa inayofanywa na CCM. Hii ingefanya CHADEMA kuonekana ni Chama kinachojali maslahi mapana na maendeleo ya Taifa. Masuala ya kupinga kila kitu hata ambayo yalikuwa sera zake toka mwanzo yanakiondolea Chama taswira ya dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwa Taifa. Wasingeweka hata mgombea kwa nafasi ya Rais kwa kipindi hiki ili waonekane na kuaminiwa na wananchi kwamba hawana uroho wa madaraka, wanathamini maendeleo ya taifa, kwani maendeleo hayana vyama. Hii ingewafanya wananchi wakiamini chama zaidi. Misuguano na serikali kwa mambo ya msingi ya kitaifa ambayo kila mtu mwenye akili ya kawaida tu anaona, haina tija kwao. Mwenyekiti Mbowe aliwahi kumpongeza hadharani Rais Magufuli akiwa Hai kwa kazi ya maendeleo anayoifanya, na akasema, "MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI". Kama Mwenyekiti alipongeza, ina maana Chama kinatambua na kuthamini kazi nzuri inayofanywa. Haiwezekani kugeuka tena na kuanza kuona kilichofanyika ni upuuzi. Ukigeugeu huo unafanya wananchi waone CHADEMA haina dhamira ya maendeleo ya kweli. Wanachokisema leo, kesho watakipinga.

2. Kutosimamisha mgombea kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kungefanya CCM watambe sana na kuendelea na makosa wanayoyafanya wakidhani wananchi wanafurahia. CCM wangeendelea kujitegea mabomu wao wenyewe hadi 2025. Wangeendelea na mambo ya miundombinu bila kushughulikia uchumi wa mwananchi mmoja mmoja. Kufika 2025 kila mwananchi angekuwa ameichoka CCM. CHADEMA wangeendelea kukusanya takwimu za makosa ya CCM hadi 2025. Ingekuwa rahisi sana kwa CHADEMA kuitoa madarakani CCM sababu wananchi wote wangekuwa tayari wamejaa chuki kwa CCM. Kwa hulka ya Magufuli angeendelea kushughulika miradi mikubwa ya kimkakati bila kuangalia maslahi ya watu wa kawaida. Sasa hivi CHADEMA imefanya CCM iwe makini zaidi na wakishinda uchaguzi watarekebisha mambo mengi aliyoyapigia kelele Lissu. Ni wazi kwamba Magufuli atashinda tena.

3. Kumwacha Magufuli kuendelea hadi 2025, kungewasaidia CHADEMA kuchukua nchi ikiwa imejaa miundo mbinu ya kila namna, na hivyo kuongoza nchi kwa urahisi. Wangekuwa na kazi moja tu ya kushughulikia maslahi ya mtu mmoja mmoja. Sasa hivi hata Lissu akishinda (kitu ambacho hakiwezekani) atapata shida sana katika kuweka mambo sawa. Wananchi wanatarajia akishinda matatizo yao yataisha ndani ya mwaka mmoja. Ukweli ni kwamba matatizo ya wananchi hayawezi kuisha ndani ya mwaka mmoja. Mwaka ukipita bila kumaliza kero zao, malalamiko yataanza, na yataigharimu sana CHADEMA katika uchaguzi wa 2025. Kitu cha kwanza kitakachogharimu CHADEMA ikishinda ni corona. Washirika wao wa nje watawataka waiweke nchi kwenye Lockdown. Hilo ni lazima. Ni Magufuli tu mwenye jeuri ya kuendelea kuwakatalia wazungu. Lissu hawezi kuwakatalia. Na akikubaliana nao ajue atakosana na kila mwananchi. Kusubiri hadi 2025, kungesaidia CHADEMA kuingia madarakani kukiwa hakuna mambo ya Corona duniani. Hivyo, mashinikizo ya kimataifa juu ya corona hayatakuwepo tena.

4. Sasa hivi CHADEMA imeshiriki uchaguzi huu, lakini kushinda sio rahisi hata kidogo. Na wakishindwa hawatarudi tena 2025. CCM itatumia sera zake na zao pia kuondoa kero kwa wananchi. CHADEMA haitakuwa na hoja tena 2025. Kwa hiyo kutovumilia miaka 5 ijayo kutawakosesha ndoto ya kushika dola hivi karibuni. Miaka 5 haikuwa mingi kuvumilia ikiwa ni mkakati wa kuitoa CCM madarakani kwa urahisi.
 
speaking of strategies, Chadema or even ACT are miles ahead of CCM.

CCM kinachowabeba ni nguvu ya dola full stop. na counter pekee ya nguvu ya dola ni "nguvu ya umma" ambayo Chadema (bara) & ACT (Zanzibar) kwenye uchaguzi huu ndiyo wanaonekana kui mobilise with a radical push for total revolt. kauli zinazotolewa na wagombea wa upinzani this time haijawahi kutolewa kwenye uchaguzi mwingine wowote huko nyuma.

and am worried kuwa kunaweza kuwa na international intervention at some point. kikubwa CCM watumie zaidi busara na kuachia matokeo ya uchaguzi yaamuliwe kupitia ballot box, basi.
 
kauli zinazotolewa na wagombea wa upinzani this time haijawahi kutolewa kwenye uchaguzi mwingine wowote huko nyuma.
Kuwa specific, Mkuu. Ainisha hizo strategies za ACT na wenzake zinazowafanya wawe ahead. Pia fafanua hizo kauli ambazo zimekustua za viongozi wa vyama hivyo.

Karibu.
 
Kuwa specific, Mkuu. Ainisha hizo strategies za ACT na wenzake zinazowafanya wawe ahead. Pia fafanua hizo kauli ambazo zimekustua za viongozi wa vyama hivyo.

Karibu.
kutokulisema tatizo hakulifanyi likaondoka lenyewe. wewe unalijua tatizo.
 
Kila ikifika jioni, huwa nasikiliza kampeni za vyama kikiwemo CHADEMA nikitegemea kwamba labda watakuwa na sera mpya za kistaarabu, kwa bahati mbaya sijaona kitu cha namna hiyo.

Kwanza kabisa, sijasikia sera mahsusi za kuweza kuwashawishi Watanzania hasa wenye akili timamu. Zaidi sana nasikia tu sera za kuwavutia vijana wa rika fulani ambao kwa kweli hawajakomaa kiakili, wapo kwenye kipindi cha Bendera fuata upepo na waliojaa mihemko tu.

Kwa hiyo, mpaka leo hii Magufuli amemwacha Lissu mbali saaaaaana. Mimi huwa napita pita mitaani na vijiweni kufanya utafiti kidogo. Asilimia kubwa ya watu hata wa CHADEMA wanamkubali sana Magufuli, na wengi wanasema kwa upande wa Rais watampa kura Magufuli.

Kwa nini Magufuli? Pamoja na sababu zingine, lakini jinsi alivyoshughulikia Issue Corona, watu wanamkubali sana Magufuli. Huyu mwingine shida inayompunguzia sifa ni kukosa staha, adabu, ustahimilivu nk. katika kuongea. Ikumbukwe kuwa, Watanzania hawajazoea na hawapendi shari.
 
Kama wewe ni mpinzani basi ni mpinzani unayajielewa sanaa, hapa ndIo upinzani wote including CHADEMA wanapofeli hawana strategists!!! Siasa sio tu kusimama jukwaani kupiga kelele ni mipango.
 
strategically speaking, Chadema or even ACT are miles ahead of CCM.

CCM kinachowabeba ni nguvu ya dola full stop. na counter pekee ya nguvu ya dola ni "nguvu ya umma" ambayo Chadema (bara) & ACT (Zanzibar) kwenye uchaguzi huu ndiyo wanaonekana kui mobilise with a radical push for total revolt. kauli zinazotolewa na wagombea wa upinzani this time haijawahi kutolewa kwenye uchaguzi mwingine wowote huko nyuma.

and am worried kuwa kunaweza kuwa na international intervention at some point. kikubwa CCM watumie zaidi busara na kuachia matokeo ya uchaguzi yaamuliwe kupitia ballot box, basi.
Jitayarishe Novemba kurudi kwenye maisha baada ya uchaguzi, hakuna intervention yoyote itayotokea hujasoma bado wananchi
 
Ni chama mfu tu ndiyo hukosa hoja. Kumbuka kuna wale walisema JPM hana haja ya kupiga debe mwaka huu, wakidhani CDM imenyongwa hadi kufa na mtu wao amefanya kila kitu (ha ha ha) na sasa hawalali.
Alikua hana haja ya kupiga kampeni kwasababu amefanya mengi sio vinginevyo
 
Chadema ni watu wa matukio , kesho wakiona Lissu amejaza stendi thread ztajaa humu za kudai Lissu aapishwe , ooh watu wameichoka CCM na bla bla kibao , kivumbi cha kigoma Leo kimewanock out kdog, ...... Kuna vitu Tu wananchi wanatamani Raisi avisikie , na wanamtumia Lissu kufikisha huo ujumbe , ila inshort wanazengo hawamwamini na sad enough wengi wao sio wapiga kura .....

Chadema ipo poor organized , viongozi wapo scattered , sio Mbowe , sio Nyalandu wote wanafight for survival , Lissu anajaribu kupambana na somehow amerestore some spirit , but alone without strategic, it is impossible to outshine full organized CCM..... Ni kichekesho kuona CCM inakabidhi nchi Kwa genge ambalo halieleweki kama Chadema , Broadcast zote , jaji mkuu, NEC , wanatangaza Chadema imeshinda, what a fu-ck ....

Kwa Safari hii CCM haihtajiki hata kutumia another alternative japo wamejipanga , kura Tu zinatosha , wasiyumbishwe na makelele ya chura wao kama tembo waendelee Tu kuyanywa maji....

Membe alinena Jambo la msingi Sana japo walimbeza , kuitoa CCM ni zaidi ya ushabiki wa kwenye majukwaa.....ambalo hawalijui hata hao mabeberu wapo upande wa CCM
Umenena, CCM is very organized kuliko mtu anaweza dhania.
 
Kila ikifika jioni, huwa nasikiliza kampeni za vyama kikiwemo CDM nikitegemea kwamba labda watakuwa na sera mpya za kistaarabu, kwa bahati mbaya sijaona kitu cha namna hiyo.
Kwanza kabisa, sijasikia sera mahsusi za kuweza kuwashawishi Watanzania hasa wenye akili timamu. Zaidi sana nasikia tu sera za kuwavutia vijana wa rika fulani ambao kwa kweli hawajakomaa kiakili, wapo kwenye kipindi cha Bendera fuata upepo na waliojaa mihemko tu.
Kwa hiyo, mpaka leo hii JPM amemwacha TAL mbali saaaaaana.
Mimi huwa napita pita mitaani na vijiweni kufanya utafiti kidogo.
Asilimia kubwa ya watu hata wa CDM wanamkubali sana JPM, na wengi wanasema kwa upande wa Rais watampa kura JPM.
Kwa nini JPM? Pamoja na sababu zingine, lakini jinsi alivyoshughulikia Issue Corona, watu wanamkubali sana JPM.
Huyu mwingine shida inayompunguzia sifa ni kukosa staha, adabu, ustahimilivu nk. katika kuongea.
Ikumbukwe kuwa, Watanzania hawajazoea na hawapendi shari.
Umenena, watanzania wengi bado ni wakarimu na wanapenda watu wanyeyekevu. Lissu anasemwa sana kama mtu mwenye dharau na kuonyesha anajua kila kitu (much know) na watanzania hawapendezwi na hilo.
 
Mzee Mtei na marehemu Bob Makani walikuwa wanajua strategies unazoongea sana na ndiyo maana CHADEMA ikapanda hadi kuwa ilivyo leo, ila sasa hivi inaelekea kifo cha mende.
 
Back
Top Bottom