Uchaguzi 2020 CHADEMA inahitaji political strategists kuishinda CCM

Uchaguzi 2020 CHADEMA inahitaji political strategists kuishinda CCM

All politics is local ...kutoshiriki uchaguzi wa mwaka Jana ,was a colossal mistake..Lengo la hawa jamaa lilikua ku-demoralize and it successes,mtaniami October 30 tally zikianza kutangazwa
 
Umenena, CCM is very organized kuliko mtu anaweza dhania.
Kweli kabisa wako very organized, kule Tunduma wamesema bayana bila kuchagua ccm maji hampati ng'oo [emoji23] [emoji23] Sasa kama mtu hajapata maji since independence (about 60 years) ndo atastuka kunyimwa maji for 5 years???
 
Umenena, watanzania wengi bado ni wakarimu na wanapenda watu wanyeyekevu. Lissu anasemwa sana kama mtu mwenye dharau na kuonyesha anajua kila kitu (much know) na watanzania hawapendezwi na hilo.
Rubbish [emoji706] [emoji706] [emoji706] Lissu ni msema kweli, hana muda wa nyeupe kuuita nyekundu, na kama ujuavyo tuna viongozi walizoea kudanganya watu (ndiyo maana ya kubana vyombo vya habari na masheria kandamizi kibao). Pili Lissu ni mtu anayefuatilia issues na msomaji mzuri wa sheria, taratibu na kanuni, ninyi mavilaza msiopenda kusoma hata page moja mmebweteka eti serikali itatoa taarifa sahihi kwa kila kitu, sasa Lissu ujinga huo hana, mzee Warioba kashasema jiandaeni kupambana na utawala wa sheria ikiwa Lissu atashinda.
 
Yaani hizi hoja zako zimenifanya nicheke ile mbaya, eti upinzani ukitaka kuitoa ccm imuunge mkono Magufuli, halafu 2025 ndio ichukue nchi. Umesema upinzani lakini umeitaja cdm tu. Sasa ngoja tuone kwenye uhalisia wa hizi hoja zako.

  1. UDP na TLP wamemuunga mkono Magufuli, hivyo tutarajie kuwa 2025 watachukua nchi kwa hii nadharia yako? Kwa taarifa yako Magufuli angeachiwa safari hii apite bila kupingwa angejiongezea muda wa kukaa madarakani. Wapinzani kushiriki uchaguzi huu, tena wakiwa wamefanyiwa kila aina ya ukatili, na kuendelea kupata watu wengi kwenye mikutano yao, ni wazi kuwa hakuna uwezekano tena wa nchi hii kuendelea kuongozwa tu na ccm kwa kura halali.
  2. Kwa taarifa yako ujenzi wa miundombinu ni tabia binafsi ya Magufuli na sio ccm. Hivyo hata akitangazwa mshindi sio akishinda bado ataendelea na hiyo miundombinu. Mpaka sasa tayari Magufuli ana miradi miwili mikubwa ya 15t+, na yote analazimisha amalize ndani ya muda wake halali wa kisheria, iwapo hatachezea katiba. Mpaka sasa hakuna mradi hata mmoja uliofikia robo ya kukamilika na tayari wananchi wameshaumia sana. Hivyo kama ni kutua hela hajatoa hata nusu ya pesa yaani 7t. Hivyo anatakiwa ndani ya hii miaka mitano lazima apate 8-10t, ni wapi atapata hizo hela, achia mbali mahitaji mengine? Kwa vyovyote kufika hiyo 2025 bado ccm itazidi kuwa kwenye wakati mgumu maana kupata hizi hela za kumalizia hiyo miradi ni kiama.
  3. Hoja ya cdm kuchukua nchi ikiwa imejaa miundombinu ya kila namna, na kuwa rahisi kuendesha nchi kwa kujali maslahi ya mtu mmoja mmoja. Hoja hii ni kiini macho, tazama deni la taifa mpaka sasa ni kiasi gani toka awamu hii iingie madarakani. Ni wazi serikali sasa inakopa sana, huku terms za mikopo ikiwa inafahamika na mtu mmoja na genge lake. Katika mazingira hayo, una uhakika gani wa kuendesha nchi kirahisi ukiwa na madeni mazito hivyo? Kuhusu hoja ya Corona hapa ndio nimeona hujui unaoongea nini, kwani Corona Ni ugonjwa wa kudumu mpaka useme wazungu watalazimisha nchi iwekwe lockdown? Halafu acha upotoshaji wa kijinga, ni nani anataka kuchukua nchi ili apewe maelekezo na wazungu? Hii ni dhahiri uko na hoja za kuokoteza.
  4. Kwamba sasa hivi cdm imeshiriki uchaguzi huu na haitashinda hata kidogo. Kwani kushiriki ni lazima ushinde? Ingekuwa kushiriki kwenye ushindani wowote lazima ushinde, basi ligi kuu ya nchi yetu ingekuwa na simba na yanga tu maana ndio wenye uwezo wa dhahiri kushinda ligi. Halafu uchaguzi mkuu sio urais tu, bali kuna wabunge na madiwani, na kura za urais hutoa wabunge wa viti maalum. Kama miaka hii mitano tuliaminishwa kuwa ccm imeua upinzani, na kinachoonekana ni tofauti, ni kipi kitafanya sasa na hiyo 2025 isiwe rahisi kuitoa ccm? Kwa taarifa yako cdm ingeingia mkenge wa huu ushauri wako fake, kufika 2025 katiba ingekuwa imeshabadilishwa na ingehalalishwa kuwa upinzani umekufa.
Ukisikia kujenga hoja za msingi na za maana ndiyo hii sasa, hongera sana mkuuu [emoji120][emoji120][emoji106][emoji106][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Rubbish [emoji706] [emoji706] [emoji706] Lissu ni msema kweli, hana muda wa nyeupe kuuita nyekundu, na kama ujuavyo tuna viongozi walizoea kudanganya watu (ndiyo maana ya kubana vyombo vya habari na masheria kandamizi kibao). Pili Lissu ni mtu anayefuatilia issues na msomaji mzuri wa sheria, taratibu na kanuni, ninyi mavilaza msiopenda kusoma hata page moja mmebweteka eti serikali itatoa taarifa sahihi kwa kila kitu, sasa Lissu ujinga huo hana, mzee Warioba kashasema jiandaeni kupambana na utawala wa sheria ikiwa Lissu atashinda.
Sikushangai mana na wewe unaangukia kundi hilo hilo ya kukosa busara na hekima la mgombea wako Lissu, watu wanapingana kwa hoja wewe unaita mtanzania mwenzako Rubbish, mtavuna mnachopanda.

Sasa nikuulize swali, Lissu unayesema ni mfwatiliaji mzuri wa issues, inakuwaje alikosa data kuhusu reli ya Kaliua kwenda Mpanda akadai imekufa na haifanyi kazi mbele ya watu wanaoitumia reli hio, nani muongo sasa kati ya serikali na Lissu? Huku sio kuigombanisha serikali na wananchi wake?

Sent from my SM-J510L using JamiiForums mobile app
 
Kwel ujinga na ushamba ni mzigo mzito
Nakupa big up mkuu. CHADEMA hili hawalielewi, wanadhani kura zipo kwa mabodaboda. Watu wenye akili timaru hawawezi kuchagua Lissu. Mbowe mwenyewe kiukweli hataki Lissu apite. Maana uenyekiti wake utakuwa mashakani. Lissu amepewa fursa ya kugombea kwa sababu zifuatazo:-

1. Kumpoza maumivu ya risasi, kuondoa lawama kwa Lissu na kuonesha kuwa Mbowe hakuhusika kwenye mpango wa kumpiga risasi.

2. Wamempa mtego. Akishinda watamchekea kiunafiki huku wakiumia. Sababu hawaamini akili za Lissu, hawajui kesho ataamka na lipi. Lissu akishinda atashinda kwa nguvu zake sio nguvu za Chama chake. Lakini baada ya kushinda watamtumia ipasavyo kufanikisha malengo yao ya kujitajirisha wakijifanya walimpa support kwenye ushindi wake.

3. Wamempa fursa ili ashindwe na uwe ndo mwisho wake kwa CHADEMA. Watasema wamempa nafasi ameshindwa. Aache na wengine wajaribu kete zao.

Baada ya Lissu kushindwa uchaguzi CHADEMA watamlaumu sana na kuona ameharibu Chama. Maana baada ya uchaguzi Chama kitapoteza credibility kabisa na kitakuwa kwenye misuguano mikali na serikali na kupigwa pini kila mahali. Lissu asishangae kufukuzwa uanachama.
 
Rubbish [emoji706] [emoji706] [emoji706] Lissu ni msema kweli, hana muda wa nyeupe kuuita nyekundu, na kama ujuavyo tuna viongozi walizoea kudanganya watu (ndiyo maana ya kubana vyombo vya habari na masheria kandamizi kibao). Pili Lissu ni mtu anayefuatilia issues na msomaji mzuri wa sheria, taratibu na kanuni, ninyi mavilaza msiopenda kusoma hata page moja mmebweteka eti serikali itatoa taarifa sahihi kwa kila kitu, sasa Lissu ujinga huo hana, mzee Warioba kashasema jiandaeni kupambana na utawala wa sheria ikiwa Lissu atashinda.

Hizo ni ndoto za mchana kufikiria LISSU atashinda. Nani ampigie kura mwendawazimu.
 
CHADEMA inahitaji wataalamu wa stratejia ya siasa (Political Strategists) kuweza kuitoa CCM madarakani kwa urahisi. Vyama vikongwe na vyenye dola kama CCM vinahitaji kufanyiwa mkakati maalumu ambao hauhitaji nguvu. Kama ningepewa fursa ya kutoa ushauri wa kimkakati wa kuitoa CCM ningeshauri ifutavyo:-

1. Kwa wakati huu 2020 - 2025 Chama kijikite katika kuunga mkono mikakati muhimu ya kitaifa inayofanywa kuinua uchumi wa Taifa inayofanywa na CCM. Hii ingefanya CHADEMA kuonekana ni Chama kinachojali maslahi mapana na maendeleo ya Taifa. Masuala ya kupinga kila kitu hata ambayo yalikuwa sera zake toka mwanzo yanakiondolea Chama taswira ya dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwa Taifa. Wasingeweka hata mgombea kwa nafasi ya Rais kwa kipindi hiki ili waonekane na kuaminiwa na wananchi kwamba hawana uroho wa madaraka, wanathamini maendeleo ya taifa, kwani maendeleo hayana vyama. Hii ingewafanya wananchi wakiamini chama zaidi. Misuguano na serikali kwa mambo ya msingi ya kitaifa ambayo kila mtu mwenye akili ya kawaida tu anaona, haina tija kwao. Mwenyekiti Mbowe aliwahi kumpongeza hadharani Rais Magufuli akiwa Hai kwa kazi ya maendeleo anayoifanya, na akasema, "MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI". Kama Mwenyekiti alipongeza, ina maana Chama kinatambua na kuthamini kazi nzuri inayofanywa. Haiwezekani kugeuka tena na kuanza kuona kilichofanyika ni upuuzi. Ukigeugeu huo unafanya wananchi waone CHADEMA haina dhamira ya maendeleo ya kweli. Wanachokisema leo, kesho watakipinga.

2. Kutosimamisha mgombea kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kungefanya CCM watambe sana na kuendelea na makosa wanayoyafanya wakidhani wananchi wanafurahia. CCM wangeendelea kujitegea mabomu wao wenyewe hadi 2025. Wangeendelea na mambo ya miundombinu bila kushughulikia uchumi wa mwananchi mmoja mmoja. Kufika 2025 kila mwananchi angekuwa ameichoka CCM. CHADEMA wangeendelea kukusanya takwimu za makosa ya CCM hadi 2025. Ingekuwa rahisi sana kwa CHADEMA kuitoa madarakani CCM sababu wananchi wote wangekuwa tayari wamejaa chuki kwa CCM. Kwa hulka ya Magufuli angeendelea kushughulika miradi mikubwa ya kimkakati bila kuangalia maslahi ya watu wa kawaida. Sasa hivi CHADEMA imefanya CCM iwe makini zaidi na wakishinda uchaguzi watarekebisha mambo mengi aliyoyapigia kelele Lissu. Ni wazi kwamba Magufuli atashinda tena.

3. Kumwacha Magufuli kuendelea hadi 2025, kungewasaidia CHADEMA kuchukua nchi ikiwa imejaa miundo mbinu ya kila namna, na hivyo kuongoza nchi kwa urahisi. Wangekuwa na kazi moja tu ya kushughulikia maslahi ya mtu mmoja mmoja. Sasa hivi hata Lissu akishinda (kitu ambacho hakiwezekani) atapata shida sana katika kuweka mambo sawa. Wananchi wanatarajia akishinda matatizo yao yataisha ndani ya mwaka mmoja. Ukweli ni kwamba matatizo ya wananchi hayawezi kuisha ndani ya mwaka mmoja. Mwaka ukipita bila kumaliza kero zao, malalamiko yataanza, na yataigharimu sana CHADEMA katika uchaguzi wa 2025. Kitu cha kwanza kitakachogharimu CHADEMA ikishinda ni corona. Washirika wao wa nje watawataka waiweke nchi kwenye Lockdown. Hilo ni lazima. Ni Magufuli tu mwenye jeuri ya kuendelea kuwakatalia wazungu. Lissu hawezi kuwakatalia. Na akikubaliana nao ajue atakosana na kila mwananchi. Kusubiri hadi 2025, kungesaidia CHADEMA kuingia madarakani kukiwa hakuna mambo ya Corona duniani. Hivyo, mashinikizo ya kimataifa juu ya corona hayatakuwepo tena.

4. Sasa hivi CHADEMA imeshiriki uchaguzi huu, lakini kushinda sio rahisi hata kidogo. Na wakishindwa hawatarudi tena 2025. CCM itatumia sera zake na zao pia kuondoa kero kwa wananchi. CHADEMA haitakuwa na hoja tena 2025. Kwa hiyo kutovumilia miaka 5 ijayo kutawakosesha ndoto ya kushika dola hivi karibuni. Miaka 5 haikuwa mingi kuvumilia ikiwa ni mkakati wa kuitoa CCM madarakani kwa urahisi.
Peleka Ujinga wako huu Chato
 
Kubalini katiba mpya ya wananchi + Tume huru ya uchaguzi kwanza otherwise your advice is null and void!
 
Sijasoma hata neno moja la post yako ambayo naamini ni ya kipuuzi. Kinachohitajika ni TUME HURU
Subiri tu utaletewa hiyo tume huru ikiwa imejaa kwenye sahani kubwa na ya kumeremeta!
 
Hakuna lolote; CCM ni weupe pee; bila wizi wa kura na udanganyifu hawana lolote.

Kama CDM na wapiga kura wote wataungana pamoja kwa nguvu zote CCM itaogopa kujaribu zoezi la wizi...

Ref. naifanya kwa kurecall chaguzi zote ndogo na zile za Serikali ya mitaa ambazo zilikuwa ni uhuni mtupu tena wa waziwazi.
 
Back
Top Bottom