KIJITOSAMAKI
Member
- Sep 2, 2020
- 29
- 16
CHADEMA inahitaji wataalamu wa stratejia ya siasa (Political Strategists) kuweza kuitoa CCM madarakani kwa urahisi. Vyama vikongwe na vyenye dola kama CCM vinahitaji kufanyiwa mkakati maalumu ambao hauhitaji nguvu. Kama ningepewa fursa ya kutoa ushauri wa kimkakati wa kuitoa CCM ningeshauri ifutavyo:-
1. Kwa wakati huu 2020 - 2025 Chama kijikite katika kuunga mkono mikakati muhimu ya kitaifa inayofanywa kuinua uchumi wa Taifa inayofanywa na CCM. Hii ingefanya CHADEMA kuonekana ni Chama kinachojali maslahi mapana na maendeleo ya Taifa. Masuala ya kupinga kila kitu hata ambayo yalikuwa sera zake toka mwanzo yanakiondolea Chama taswira ya dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwa Taifa. Wasingeweka hata mgombea kwa nafasi ya Rais kwa kipindi hiki ili waonekane na kuaminiwa na wananchi kwamba hawana uroho wa madaraka, wanathamini maendeleo ya taifa, kwani maendeleo hayana vyama. Hii ingewafanya wananchi wakiamini chama zaidi. Misuguano na serikali kwa mambo ya msingi ya kitaifa ambayo kila mtu mwenye akili ya kawaida tu anaona, haina tija kwao. Mwenyekiti Mbowe aliwahi kumpongeza hadharani Rais Magufuli akiwa Hai kwa kazi ya maendeleo anayoifanya, na akasema, "MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI". Kama Mwenyekiti alipongeza, ina maana Chama kinatambua na kuthamini kazi nzuri inayofanywa. Haiwezekani kugeuka tena na kuanza kuona kilichofanyika ni upuuzi. Ukigeugeu huo unafanya wananchi waone CHADEMA haina dhamira ya maendeleo ya kweli. Wanachokisema leo, kesho watakipinga.
2. Kutosimamisha mgombea kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kungefanya CCM watambe sana na kuendelea na makosa wanayoyafanya wakidhani wananchi wanafurahia. CCM wangeendelea kujitegea mabomu wao wenyewe hadi 2025. Wangeendelea na mambo ya miundombinu bila kushughulikia uchumi wa mwananchi mmoja mmoja. Kufika 2025 kila mwananchi angekuwa ameichoka CCM. CHADEMA wangeendelea kukusanya takwimu za makosa ya CCM hadi 2025. Ingekuwa rahisi sana kwa CHADEMA kuitoa madarakani CCM sababu wananchi wote wangekuwa tayari wamejaa chuki kwa CCM. Kwa hulka ya Magufuli angeendelea kushughulika miradi mikubwa ya kimkakati bila kuangalia maslahi ya watu wa kawaida. Sasa hivi CHADEMA imefanya CCM iwe makini zaidi na wakishinda uchaguzi watarekebisha mambo mengi aliyoyapigia kelele Lissu. Ni wazi kwamba Magufuli atashinda tena.
3. Kumwacha Magufuli kuendelea hadi 2025, kungewasaidia CHADEMA kuchukua nchi ikiwa imejaa miundo mbinu ya kila namna, na hivyo kuongoza nchi kwa urahisi. Wangekuwa na kazi moja tu ya kushughulikia maslahi ya mtu mmoja mmoja. Sasa hivi hata Lissu akishinda (kitu ambacho hakiwezekani) atapata shida sana katika kuweka mambo sawa. Wananchi wanatarajia akishinda matatizo yao yataisha ndani ya mwaka mmoja. Ukweli ni kwamba matatizo ya wananchi hayawezi kuisha ndani ya mwaka mmoja. Mwaka ukipita bila kumaliza kero zao, malalamiko yataanza, na yataigharimu sana CHADEMA katika uchaguzi wa 2025. Kitu cha kwanza kitakachogharimu CHADEMA ikishinda ni corona. Washirika wao wa nje watawataka waiweke nchi kwenye Lockdown. Hilo ni lazima. Ni Magufuli tu mwenye jeuri ya kuendelea kuwakatalia wazungu. Lissu hawezi kuwakatalia. Na akikubaliana nao ajue atakosana na kila mwananchi. Kusubiri hadi 2025, kungesaidia CHADEMA kuingia madarakani kukiwa hakuna mambo ya Corona duniani. Hivyo, mashinikizo ya kimataifa juu ya corona hayatakuwepo tena.
4. Sasa hivi CHADEMA imeshiriki uchaguzi huu, lakini kushinda sio rahisi hata kidogo. Na wakishindwa hawatarudi tena 2025. CCM itatumia sera zake na zao pia kuondoa kero kwa wananchi. CHADEMA haitakuwa na hoja tena 2025. Kwa hiyo kutovumilia miaka 5 ijayo kutawakosesha ndoto ya kushika dola hivi karibuni. Miaka 5 haikuwa mingi kuvumilia ikiwa ni mkakati wa kuitoa CCM madarakani kwa urahisi.