PreGE2025 CHADEMA inajichinja na kujikaangaa kwa mafuta yake yenyewe

PreGE2025 CHADEMA inajichinja na kujikaangaa kwa mafuta yake yenyewe

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
51,453
Reaction score
41,274
Wailianza kwa mbwembwe sana chini ya uongozi mpya kwamba, mapambano ya kidemokrasia dhidi ya maslahi mapana ya wanachadema na wananchi wote wa Tanzanzania, sasa yanapata pumzi mpya, uelekeo mpya na yatakua yana sura mpya kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania october2025. Na wanachadema wengi waliamini hivyo na hawakua na shaka kabisa.

Badala yake sasa, uongozi mpya ulivyoingia madarakani tu, agenda ya kuwatafuta na kuwashughulikia mahasimu wa uongozi mpya ikaanza kwa vipigo vya mbwa koko, ikilenga zaidi wananwake viongozi ambao wana nguvu na upeo mkubwa wa kujenga hoja na kutoa maoni na mitazamo yao juu ya uendeshaji wa mambo mbalimbali ya chadema bila hofu wala kuogopa mtu.

Hali ikaendelea kwenda mrama zaidi pale misingi, malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa chadema, ikaanza kukiukwa na kupuuzwa na pesa ikawekwa mbele zaidi, kanakwamba ndio agenda kuu ya chadema chini ya uongozi mpya, wanachama wakaanza kuchangishwa pesa kiholela na baadae kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kampeni ya tone tone kidigitali, huku uwazi uliohubiriwa kwenye masuala ya pesa, ukawa ni giza totoro na kizungumkuti ambacho mpaka leo haijulikani tone tone ilikusanaya kiasia gani cha pesa, na zimetumika kwenye whisky na nyama choma au kuna matumizi ya ziada.

Imani ya wanachadema polepole ikaanza kuporomoka, kuzama na kupotea kabisa dhidi ya uongozi mpya wa chadema, wanachadema wakaanza kuikumbuka na kuona afadhali hata misri yao ya uongozi uliopita.

Uongozi mpya, ukaendelea kuingiza agenda binafsi ambazo ni utopian kimanti ndani ya chadema, na kukitenga kabisa chama hicho na michakato ya kidemokrasia na kujiepusha kabisa kisiwe na ndoto ya kushika dola, uongozi mpya ukajikita zaidi kuchochea chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao sikivu na kusaka pesa za matumizi ya chama ikiwa ni pamoja na matumizi ya kununulia whisky na nyama choma kwaajili ya viongozi wa kitaifa wa chadema.

Chadema ikaanza kupotea kabisa kwenye harakati za kidemokrasiasa, na ikawa na sura ya kibaishara zaidi na kujikita kwenye kusaka pesa. Agenda ya mwenyekiti wa Taifa ya No reform No elections ilipotangazwa, wanachadema walishtuka na kushangaa sana. In fact mpaka leo kuna wanachadema bado wamepigwa butwaa, kwasababu hakuna anaehubiri agenda hiyo ispokua mwenyekiti wa chadema Taifa pekee.

Wanachadema wengi shupavu waliipuuza agenda hiyo isiyo na faida, na wakaenda mbali zaidi hata kutangaza nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao, wakimaanisha watashiriki kikamilifu uchaguzi huo wa october whether kuna mabadiliko ya kisheria ama laa, na kuifanya agenda ya mwenyekiti wa taifa ya no reform no elections kua ni useless, nonsense, null and void agenda.

Angalau G55 wameibuka kuja kuifunga breki chadema ambayo ilikua inapelekwa puta na kwenda mrama huku ikiendeshwa na dereva kibaka wa siasa konda addict wa kubeti na utingo tapeli. Bila g55 chadema ilikua inakwenda kuzama kwenye shimo la sahau, ingawa hata hivyo bado yapo madhara makubwa ya mgawanyiko yanaidhoofisha chadema kabla ya kurejea kwenye mstari tena.

Kwa hali ilivyo sasa, hayupo mwanachadema yeyote ndani ya chadema, mwenye uwezo au uthubutu wa kumzuia mwanachadema mwingine kwenda kupiga kura kwenye uchguzi mkuu wa October mwaka huu.

Una maoni gani kama mdau wa siasa?🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom