Chadema wana ugomvi na bunge na Ndugai ukija kwenye serikali ndio kabisa hawaivi nayo ukienda mahakamani ndio usiseme Lisu alishatukana hadi majaji kuwa hawajui kiingereza na hawana Imani na majaji wa Tanzania
Hiki Chama vipi? Ukidharau mihimili yote utakuwa mgeni wa nani?
1) Ugomvi na serikali hii ya ccm.
Pamoja na kwamba serikali hii imeingia madarakani kwa wizi wa kura 2020, na wizi wa mchakato mzima wa uchaguzi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019, bado CHADEMA iliomba kukutana na Rais Samia, ambaye alikubali kwa maandishi. Hiyo ilikuwa ni heshima kubwa kwa Rais na serikali yake. Kumbuka kutokana na uharamia, ubabe na ujambazi waliofanyiwa CHADEMA kwenye hizo "chaguzi" mbili, hawachukui ruzuku ambayo ni haki yao kwa mujibu wa sheria.
Rais Samia inaonekana alipata ushauri tofauti, na akaukubali, akawatosa CHADEMA. Sasa hivi anazuia hata mikutano ya ndani, kakamata mamia ya wanachadema na kuwasweka rumande.
Sasa hapo mgomvi ni nani? Bila shaka ni Serikali.
2)Ugomvi na Bunge
Baada ya uporaji wa 2020, serikali ya ccm ikagundua kwamba hawataweza kuendesha bunge la vyama vingi kwa wabunge wa chama kimoja. Badala ya kuketi chini na CHADEMA, ukafanyika umafia. Wakaanzisha, kwa nguvu, mchakato wa siri wa kupata "wabunge wa viti maalum" ndani ya CHADEMA , kinyume na taratibu zote. Hii pia ilikusudiwa kuipasua CHADEMA, kuipora pia wabunge wake muhimu na wachapakazi. CHADEMA ilisimama imara na kuwatimua. Uamuzi huu ulikuwa mgumu sana, lakini CHADEMA ilisimama imara. Ndugai daima amesimama upande wa serikali. Kuna wakati Magufuli alimwagiza Spika Ndugai "awashughulikie ndani ya bunge, serikali itawashughulikia nje ya bunge"
Sasa hapo mgomvi ni nani? Ni Ndugai na bunge lake DHAIFU.
3)Ugomvi na Mahakama
Kuna mahakimu na majaji wameteuliwa kinyume na utaratibu, ili kulinda maslahi ya serikali. Mfano hakimu aliyemfunga Sugu, na kisha kuteuliwa ujaji. Kesi hiyo ya kubumba ilikuja futwa kwenye rufaa, baada ya kucheleweshwa sana. Jaji aina ya Luvanda, ambaye anakubali "charge sheet" ina makosa, lakini bado anawarejesha rumande watuhumiwa, kwa kesi ipi?
Mgomvi nani hapo? Ni baadhi ya mahakimu na majaji wa Mahakama