CHADEMA inawahitaji akina Mdee kuliko akina Mdee kuihitaji CHADEMA. Warejesheni kuimarisha chama

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kupata mwanasiasa mwenye kariba ya Halima Mdee na Esther Bulaya kwenye upinzani sio jambo jepesi, hasa katika nyakati hizi ambazo CCM inamtafuta kila mwanasiasa maarufu kutoka upinzani.

Akina Halima ni wazoefu, wasomi, wenye misuli ya fedha za kupiga kampeni zao na za chama na wanakubalika kwenye jamii.

Chadema warejeshi hawa watu ili kuonyesha zile 4Rs za Rais Samia kuwa hata kwenu hizo Rs zinafanya kazi.
 
Hawawezi kurudishwa mpaka ukweli wa wameingiaje bungeni uwe wazi. Kwasasa huwezi kuridisha watu ambao wame gushi nyaraka na hawajakubali makosa. Nani atawazuia kufanya hayo tena! tatizo liko hapo tu bila kukiri wazi na kueleza ukweli hawarudi Chadema!
 
Unaweza kuwa sahihi but…
Chadema wanawaza vyeo sio kumkomboa mwananchi shida iko hapa..
Hii inayoendelea ndani ya watawala ni opportunity ya … nisiseme sana

Upinzani Tanga yenye Nyika hakuna
Wengi ni wafanyabiashara
Mikutano hii inawapotezea muda
Walitakiwa kuwa mahakamani kupinga hizi sheria mpya za uchaguzi kutwa wapo barabarani
Mwenyekigoda anacheza na akili za wananchi

Ipo siku mtaujua ukweli mchungu.
 
Punguza unafiki umekaza shingo kulaumu upinzani huku walioupitisha sheria m ovu za uchaguzi unawaona. Waaana.

Tatizo lako unadhani upinzani ni watu wachache. Yani wewe ukae na ufanye shughuli zako ukitegemea wengine wafanye Tena kwa kuwakebehi. Very stupid.
 
Wakiri,waombe radhi na waape kukilinda chama. kazi ni kupima loss/ benefi analysis. Ila kwa siasa za kisasa warudi kushupaza shingo wakati Lowassa arirudi kwao ni kujiumiza bure
 
Hawawezi kurudishwa mpaka ukweli wa wameingiaje bungeni uwe wazi. Kwasasa huwezi kuridisha watu ambao wame gushi nyaraka na hawajakubali makosa. Nani atawazuia kufanya hayo tena! tatizo liko hapo tu bila kukiri wazi na kueleza ukweli hawarudi Chadema!
Mkihoji hayo itafika October 2025 hamjapata majibu ya hilo kama vile majibu ya kwanini Mbowe na Lisu walifutiwa kesi na kurudishiwa mali zao nje ya mahakama.
 
Unaweza kuwa sahihi but…
Chadema wanawaza vyeo sio kumkomboa mwananchi shida iko hapa..
Hii inayoendelea ndani ya watawala ni opportunity ya … nisiseme sana

Upinzani Tanga yenye Nyika hakuna
Wengi ni wafanyabiashara
Mikutano hii inawapotezea muda
Walitakiwa kuwa mahakamani kupinga hizi sheria mpya za uchaguzi kutwa wapo barabarani
Mwenyekigoda anacheza na akili za wananchi

Ipo siku mtaujua ukweli mchungu.
Waangalie usoni akina Nassari, Lamwai, marando, Kitila Mkumbo, "Tumbili", Lyatonga, Msigwa, Slaa, Lipumba, Devutwa, Mbatia, Sugu, Lema, Kabwe, nk. Woote hawa unaweza kuwaelezea kwa pamoja kwa kutumia sentensi moja tu.
 
Mkihoji hayo itafika October 2025 hamjapata majibu ya hilo kama vile majibu ya kwanini Mbowe na Lisu walifutiwa kesi na kurudishiwa mali zao nje ya mahakama.

Wewe jidanganye tu bila hawa madada kuwa wawazi hakuna mtu atawaamini na hawataweza kukubaliwa. Chadema wangekuwanwanafikiria kama wewe isingekuwepo leo hayo ni mawazo ya wana CCM ! Uongo uongo tu. Ni bora uwe na wacheche makini kuliko matapeli ndani ya chama
 
Ningekuwa kwenye ngazi ya maamuzi ningependekeza kuwa kama wanataka kurudi basi waombe msamaha kwa usaliti wao walioufanya na waeleze kweli yote kwa 100 % jinsi walivyorubuniwa na hadi kuisaliti Chadema. Najua ilitumika nguvu kubwa sana ya vitisho juu ya usalama wao dhidi ya dola na pia hela ilitumika , na kwa kweli kwa aina ya utawala wa kishetani wa yule mwovu wa Chato waliogopeshwa kiasi kikubwa kuzidi uwezo wao wa kustahimili. Lakini ni lazima waeleze ukweli wote kabisa na dunia ijue uhuni wa utawala wa CCM chini ya Magufuli na hata huu wa sasa kwani tumesharudi kule kule tena. Wakitimiza masharti haya wanaweza kusamehewa kwani nani hajawahi kukosea hapa duniani?
 
Punguza unafiki umekaza shingo kulaumu upinzani huku walioupitisha sheria m ovu za uchaguzi unawaona. Waaana.

Tatizo lako unadhani upinzani ni watu wachache. Yani wewe ukae na ufanye shughuli zako ukitegemea wengine wafanye Tena kwa kuwakebehi. Very stupid.
Kuna siku utanielewa
Ukweli mchungu
Sitakutukana
Matusi hayajengi
 
Ningekuwa kwenye ngazi ya maamuzi ningependekeza kuwa kama wanataka kurudi basi waombe msamaha kwa usaliti wao walioufanya na waeleze kweli yote kwa 100 % jinsi walivyorubuniwa na hadi kuisaliti Chadema. Najua ilitumika nguvu kubwa sana ya vitisho juu ya usalama wao dhidi ya dola na pia hela ilitumika , na kwa kweli kwa aina ya utawala wa kishetani wa yule mwovu wa Chato waliogopeshwa kiasi kikubwa kuzidi uwezo wao wa kustahimili. Lakini ni lazima waeleze ukweli wote kabisa na dunia ijue uhuni wa utawala wa CCM chini ya Magufuli na hata huu wa sasa kwani tumesharudi kule kule tena. Wakitimiza masharti haya wanaweza kusamehewa kwani nani hajawahi kukosea hapa duniani?
Ukiwaangalia sana utagundua kuwa hawakuwa wasaliti ila waliiona Fursa wakaichukua. Baada ya CCM "kukomba" viti vyote kasoro kiti kimoja cha Nkasi CHADEMA wakasusia matokeo ya uchaguzi. Walikuwa wanamshinikiza hata yule wa Nkasi asiende kuapishwa. Hata wakati Mbowe, Msigwa, Lema, mnyika, Lissu wanatangazwa kushinda ubunge madai ya kuibwa kura yalikuwepo pia lakini hawakususa kwenda bungeni. Kama akina halima wasingekwenda bungeni viti vile vingechukuliwa na CCM "ukisusa twala".

Serikali iliwala,isha akina halima kuingia bungeni ili nchi isikose misaada na mikopo anayofungamanishwa na demokrasia.
 
Kupata mwanasiasa mwenye kariba ya Halima Mdee na Esther Bulaya kwenye upinzani sio jambo jepesi, hasa katika nyakati hizi ambazo CCM inamtafuta kila mwanasiasa maarufu kutoka upinzani.

Akina Halima ni wazoefu, wasomi, wenye misuli ya fedha za kupiga kampeni zao na za chama na wanakubalika kwenye jamii.

Chadema warejeshi hawa watu ili kuonyesha zile 4Rs za Rais Samia kuwa hata kwenu hizo Rs zinafanya kazi.
Ni jamii ipi hiyo inayowakubali wasaliti?
 
Ni jamii ileile na watu walewale waliokuwa inasukuma magari ya makada wa CCM wanaohamia kilaghai upinzani na kurudi Tena CCM kama akina lyatonga, sumaye, lowassa, Msigwa, Nasari, Lamwai, Dr. Slaa, Kitila, tumbili na wengine wengi orodha yao ni ndefu. Mimi ninaamini Halima na bulaya ni wanachadema sawasawa kuliko Mnyika na Mbowe na wengine wengi ndani ya chadema ambao wanasubiri wakati na Bei yao ya kununuliwa ipande, ni maswala ya muda TU.
 
Takataka TU!! Kwa iyo wakifa na chadema imekufa?

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom