Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa Hakika Hiki chama Hakina watu, hakina wafuasi , hakina Wa Kukiunga Mkono wala kukipenda . Ni chama ambacho kimekatalika Mioyoni Mwa Watanzania na watu wote wenye akili Timamu na wanaojitambua.
Ni Chama ambacho kwa Hakika Kimepuuzwa na Watanzania. Ni Chama ambacho Hakina Mguso kwa watu na hakieleweki wala kukubalika kwa watu.
Embu Fikiria Ndugu zangu Watanzania chama hiki ambacho kimezoea kuombaomba kila kitu licha ya kuwa na umri wa zaidi ya Miaka 30 na kushindwa kuwa na kitega Uchumi hata kimoja cha kukipatia na kukiingizia pesa licha ya kupokea Mamilioni kwa Mamilioni ya Ruzuku kwa Miaka mingi lakini kimeishia Kuwa Tegemezi kwa Kila Kitu.
Hiki chama Ukweli Ni kuwa Hakina wanachama. Kwa sababu kingekuwa na wanachama walau hata Laki nne yaani 400,000 na kila mmoja akachangia ama kutoa walau Elfu moja moja kwa kila mwanachama Mpaka Muda huu napoandika hapa Maana yake zingekuwa zimepatikana Millioni Mia Nne yaani 400,000,000/=
Yaani 1,000 x 400,000 = 400,000,000/=
Pesa ambayo ingekuwa ni kubwa kuliko ile ambayo wanaitaka . Au hata kama wangechanga mia tano tano kila mmoja maana yake mpaka muda huu wangekuwa na millioni mia mbili
Yaani: 500 x 400,000 =200,000,000/=
Lakini kinachoendelea kwenye Michango ya CHADEMA mpaka kufikia leo kinachekesha kwelikweli na kuvunja mbavu . Ni Aibu kubwa sana tena sana isiyosemeka wala kuelezeka. Sasa kwa msingi huo unafikiri chama hiki kinaweza kushinda uchaguzi upi na kwa njia ipi? Kwa sababu hakina wanachama wala wafuasi na chama ni watu .
Na ukweli ni Kuwa kote ambako CHADEMA ilikuwaga inashinda kiti cha Ubunge ilikuwa ni kwa sababu wana CCM walikuwa wameamua kupigia kura upinzani hasa baada ya kusimamishwa na kupitishwa kwa mgombea ambaye alikuwa hakubaliki kwa watu ndani ya chama na nje ya chama . Yaani ile unakuta mtu hakushinda kura za maoni na wala hakubaliki halafu akapewa kugombea ubunge ndio maeneo kama hayo wana CCM walikuwa wanapiga kura za hasira kama sehemu ya kupaza sauti zao na kutoridhishwa na Mgombea wao.
Lakini ni ngumu sana CCM kushindwa na kupoteza kiti cha Ubunge sehemu na mahali ambako wana CCM wameungana na kuwa kitu kimoja pasipo kuwa na Makundi . Ndio sababu hata kwenye Urais CHADEMA imekuwa ikipata kura ambazo hazijai hata kwenye kiganja cha Mkono au kutosha kwenye Mfuko wa Suruali .
Na hii ni kwa sababu CHADEMA haina sera wala ajenda wala hoja zenye Kugusa Maisha ya watu. CHADEMA haina uwezo hata wa kuandaa Ilani yake achilia mbali kuwa na Wagombea wa kueleweka . CHADEMA ni kama kusanyiko la wasaka tonge na watu walipoteza matumaini ya Maisha na kuamua kujikusanya tu ili wakitumie chama kushibisha Matumbo yao kwa michango ya kinyonyaji kwa wanachama wake kiduchu.
Ni Aibu sana kwa hili chama ndugu zangu . Yaani chama kinachechemea na kuhangaika kutembea utafikiri kimekatwa miguu. Ukweli ni kuwa kama kingekuwa kinapendwa na kama kingekuwa na wanachama wengi basi mpaka kufikia Muda Huu Pesa zingekuwa zimemiminika mpaka kuvuka malengo.
Yaani harambee ya kumchangia Pesa Mwimbaji wa Injili Upendo Nkome Ilipatikana kwa Muda Mfupi na kwa haraka kuliko hata CHADEMA nzima na namna inavyohangaika na michango yake. Hii maana yake ni Kuwa Upendo Nkome anao ushawishi Mkubwa kwenye Nchi Hii na mioyoni Mwa Watanzania kuzidi CHADEMA nzima . Yaani Mwimbaji Upendo Nkome ni Mkubwa kuliko CHADEMA. Na anasikilizwa na kupendwa sana kuliko CHADEMA.
Kwa hakika CHADEMA siyo chama bali ni kagenge fulani hivi kaliko jikusanya kwa maslahi yake Binafsi. Huku kakiwa kamekaa tu na kubweteka bila kufanya kazi wala kujishughulisha na kazi zaidi ya kuwaza namna ya kuwachangisha watu pesa ili wazitafune kama Mchwa .
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.