CHADEMA isiogope kujirudi ili tusonge mbele kwa pamoja

CHADEMA isiogope kujirudi ili tusonge mbele kwa pamoja

Joined
Nov 27, 2019
Posts
35
Reaction score
146
Nianze kwa kumpongeza sana Mh. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA, kwa mambo mawili. Kwanza kitendo chake cha kuhudhuria sherehe za Uhuru mwezi Disemba, 2019 kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike.

Pili kwa kitendo chake cha kumuandikia barua Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitoa mapendekezo kuhusu ya kurejesha utengamano wetu kama taifa.

Kufungua milango ya majadiliano kwenye siasa ni jambo jema hasa kwa nchi kama yetu ambayo miaka yote tumeepuka machafuko ya kisiasa huku tukibaki kuwa kisiwa cha amani Afrika na dunia nzima.

Ila kuna mambo machache naona ni muhimu Mh. Freeman Mbowe akayatizama na kuona ni namna gani anaweza kuyafanyia kazi. Kwanza kabisa, kurudi hatua chache nyuma mpaka mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Sote tunafahamu kwamba CHADEMA walikataa matokeo ya uchaguzi na walitamka kutomtambua Rais, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli. Wakati Rais anahutubia Bunge kwa mara ya kwanza CHADEMA walitoka nje na Mbunge pekee aliyebaki Bungeni [kwa bahati mbaya] alikuwa Ndugu Zitto Zuberi Kabwe! CHADEMA hawajawahi kumtambua rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ingawaje muda ulivyozidi kwenda ni wazi wamemtambua na ndio maana hata barua imeandikwa kwa kumtaja kwa nafasi hiyo.

Hili linaweza kuonekana ni jambo dogo na hakuna sababu ya kulishikilia bango. Lakini ukiangalia mambo mengine utaona sio jambo dogo. Nitatoa mfano wa tukio la karibuni kabisa ambalo ndio linasababisha suala hili niliangalie tofauti.

Mh. Freeman Mbowe ameandika maneno haya kwenye barua yake kwa Mh. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli

“CHADEMA, kama Chama Kikuu cha upinzani kinaamini kuna kila sababu sasa kuanza kuchukua hatua za makusudi na shirikishi kukabiliana na changamoto hizi; na wewe kama Rais, una mamlaka yote ya kuanzisha mchakato wa kurudisha utengemano wa nchi yetu”.

Wakati huo huo barua hiyo ilipoandikwa Mh. Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA amesambaza ujumbe wenye maneno haya kwa wabunge wa CHADEMA,

“Ushauri wangu ni kwamba Wabunge wetu wote ambao wameathiriwa na vitendo hivi wawasilishe malalamiko yao kwa IPU ili yachunguzwe. Kufanya hivyo kutaongeza shinikizo kwa utawala huu wa mabavu, pamoja na uongozi wa Bunge.

Angalau wananchi wetu, na Serikali ya Magufuli na Bunge la Spika Ndugai, watajua kwamba vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu na za Wabunge wa upinzani zinamulikiwa taa na dunia”.

Ukisoma ujumbe wa Mh. Tundu Lissu ni wazi yeye njia ya kupata suluhu ni IPU (Inter-Parliamentary Union). Huko ndio litatoka shinikizo kwa utawala wa mabavu! Pia serikali ni ya Magufuli na bunge ni la spika Ndugai. Namna mtu anavyoandika mwenye kuelewa anaweza kujua fikra, mawazo au hata heshima mtu aliyonayo dhidi ya mamlaka, serikali na bunge.

Najaribu kuwaza ni namna gani Mh. Rais anaweza kuanzisha mchakato wa kurudisha utengamano nchini wakati huo huo kiongozi wa juu wa CHADEMA anahamasisha wabunge wa chama hicho watumie vyombo vya nje kuweka shinikizo dhidi ya nchi yetu?

Mh. Rais anawezaje kuona ‘nia njema na ya dhati’ kwa upande wa CHADEMA wakati kiongozi wa juu wa CHADEMA anaendelea kusambaza ujumbe kwamba serikali yake ni ya mabavu? Najaribu kufikiria kwa sauti.

Mh. Freeman Mbowe ameandika kwa busara kubwa kabisa maneno haya,

“Nina hakika tunahitaji maridhiano ya Kitaifa. Kama viongozi tuna wajibu huo mbele ya wananchi wenzetu na hata mbele ya Mungu; na wewe kama Kiongozi Mkuu wa nchi yetu una turufu na wajibu wa kipekee kuwezesha matamanio haya ya haki kupatikana”.

Lakini Mh. Tundu Lissu, kwa mujibu wa ujumbe wake, kama wabunge wa CHADEMA wakikubali anaahidi,

“niko tayari kuwasaidia kuandaa hoja za kupeleka IPU au, bora zaidi, kuwaomba mawakili wangu wa London, yaani Amsterdam & Partners, kufanya hivyo kwa niaba yetu wote”

Kwa mfano huu wa alichokisambaza Mh. Tundu Lissu kwa wabunge wa CHADEMA wakati huo huo ambao Mwenyekiti wake Mh. Freeman Mbowe ameandika barua kwenda kwa Mh. Rais, Dkt John Pombe Magufuli aanzishe mchakato wa kutafuta utengamano wa kitaifa unaweza kuona kwa nini ni vigumu kufika huko ambako Mh. Freeman Mbowe anasihi tufike.

Sio kwamba Mh. Tundu Lissu hapaswi au hana haki kutafuta haki yake sehemu yoyote anayoona inaweza kupatikana, la hasha. Ila hatua hizo kwa kiasi kikubwa sana zinaondoa uhalali au zinatia shaka kuhusu nia ambayo imeonyeshwa vizuri tu kwenye barua ya Mh. Freeman Mbowe.

Na zaidi ya hilo, ni pale ambapo baadhi ya viongozi wa CHADEMA pamoja na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe wanaendelea kushawishi mataifa ya nje wahisani pamoja na taasisi za fedha kuinyima nchi yetu misaada na kuifanya ionekane inakiuka haki za binadamu na utawala wa sheria kwa kiasi kikubwa.

Hoja ambazo Mh. Tundu Lissu anaahidi kuwasaidia wabunge kupeleka IPU ndio hizo hizo zinazotumika kushawishi nchi yetu inyimwe misaada!! Majadiliano yanaanzia wapi?

Nimalizie kwa kusema wazi kabisa kwamba mara baada ya uchaguzi mpaka leo CHADEMA (na baadae ACT Wazalendo) wamekuwa wakitoa maneno ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa na lengo la kumdhalilisha na kumfedhehesha Rais.

Hapa zinaweza kuibuka hoja nyingi tu kwa mfano, lugha zilizotumika sio matusi au za fedheha ndio kazi ya upinzani, ukiwa kiongozi lazima ukubaliane na matusi au fedheha nk.

Lakini ukweli utabaki kwamba kauli na majina kama 1. Dikteta uchwara 2. Mshamba 3. Muuaji 4. Jiwe 5. Meko na mengine mengi kamwe hayawezi kuwa ni maneno ya kufurahisha. Hata kama mtu akikaa kimya ni lazima tutambue kwamba kila mwanadamu ana moyo.

Kwa wenzetu huko nje (Marekani na Ulaya) unaweza kusema ni sawa. Kiongozi anaweza akatukanwa hadharani na mtu akasema ni uhuru wa mawazo. Labda ndio maana huko kwa wenzetu pia leo wanaume wanaoana wenyewe kwa wenyewe na wanaona sawa. Huku kwetu ni tofauti.

Sasa tunapozungumzia utengamano wa kitaifa pamoja na mapendekezo yaliyotolewa tusisahau mambo ambayo yanaweza kuonekana ni madogo ila ni sababu ya mikwamo tunayoweza kuwa tunakutana nayo kila mara.

Kitabu kimoja kinaitwa “Tipping Point: How Little Things Can Make a Big Difference” na mwandishi Malcolm Gladwell kinaelezea vizuri sana dhana hii ya mambo madogo ambayo kwenye maisha ni rahisi sana kutoyatilia maanani. Kama hakutakuwa na dalili za wazi kwamba lengo ni utengamano na sio njia ya kutafuta hatua za kisiasa (political mileage) basi itakuwa vigumu.

Natambua kuongoza chama kama CHADEMA sio jambo rahisi hasa linapokuja suala la ‘compromises’ kwa manufaa ya nchi. Mh. Freeman Mbowe anaweza kuitwa kila jina. Na hata kuwashawishi tu kwamba ni jambo jema kufanya hivyo itakuwa sio rahis kama ilivyokuwa wakati wa kuhudhuria sherehe za Uhuru.

Ila ni muhimu [na lazima] CHADEMA kuchukua hatua na kuwaelekeza viongozi wote kusitisha uhamasishaji unaondelea dhidi ya nchi yetu. Haiwezekani kukaa kwenye majadiliano ya aina yoyote ile wakati kama nchi tunalalmikiwa IPU, European Union, World Bank, kwenye mabalozi mbalimbali nk.

Pili CHADEMA iandike barua kumtambua rasmi Rais Dkt John Pombe Magufuli hata kama ni mwaka wake wa tano madarakani kuondoa dhana ya kutokumtambua. Wazungu wanasema ‘better late than never’ (heri uchelewe kuliko kutokufanya kabisa). Wanachama wa CHADEMA na baadhi ya viongozi ambao wanajulikana waache tabia ya kudhihaki mamlaka.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni Serikali halali iliyopo madarakani. Kama Chama, CHADEMA itoe tamko kuelekeza hivyo ili basi nia njema iweze kuonekana kwenye walichoandika na sio njia ya kufikia uchaguzi 2020 ambao tayari CCM imeshajiandaa vya kutosha kushinda kwa kura za wananchi.
 
Nianze kwa kumpongeza sana Mh. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA, kwa mambo mawili. Kwanza kitendo chake cha kuhudhuria sherehe za Uhuru mwezi Disemba, 2019 kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike. Pili kwa kitendo chake cha kumuandikia barua Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitoa mapendekezo kuhusu ya kurejesha utengamano wetu kama taifa. Kufungua milango ya majadiliano kwenye siasa ni jambo jema haswa kwa nchi kama yetu ambayo miaka yote tumeepuka machafuko ya kisiasa huku tukibaki kuwa kisiwa cha amani Afrika na dunia nzima.



Ila kuna mambo machache naona ni muhimu Mh. Freeman Mbowe akayatizama na kuona ni namna gani anaweza kuyafanyia kazi. Kwanza kabisa, kurudi hatua chache nyuma mpaka mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Sote tunafahamu kwamba CHADEMA walikataa matokeo ya uchaguzi na walitamka kutomtambua Rais, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli. Wakati Rais anahutubia Bunge kwa mara ya kwanza CHADEMA walitoka nje na Mbunge pekee aliyebaki Bungeni [kwa bahati mbaya] alikuwa Ndugu Zitto Zuberi Kabwe! CHADEMA hawajawahi kumtambua rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ingawaje muda ulivyozidi kwenda ni wazi wamemtambua na ndio maana hata barua imeandikwa kwa kumtaja kwa nafasi hiyo. Hili linaweza kuonekana ni jambo dogo na hakuna sababu ya kulishikilia bango. Lakini ukiangalia mambo mengine utaona sio jambo dogo. Nitatoa mfano wa tukio la karibuni kabisa ambalo ndio linasababisha suala hili niliangalie tofauti.



Mh. Freeman Mbowe ameandika maneno haya kwenye barua yake kwa Mh. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli



“CHADEMA, kama Chama Kikuu cha upinzani kinaamini kuna kila sababu sasa kuanza kuchukua hatua za makusudi na shirikishi kukabiliana na changamoto hizi; na wewe kama Rais, una mamlaka yote ya kuanzisha mchakato wa kurudisha utengemano wa nchi yetu”.



Wakati huo huo barua hiyo ilipoandikwa Mh. Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA amesambaza ujumbe wenye maneno haya kwa wabunge wa CHADEMA,



“Ushauri wangu ni kwamba Wabunge wetu wote ambao wameathiriwa na vitendo hivi wawasilishe malalamiko yao kwa IPU ili yachunguzwe. Kufanya hivyo kutaongeza shinikizo kwa utawala huu wa mabavu, pamoja na uongozi wa Bunge. Angalau wananchi wetu, na Serikali ya Magufuli na Bunge la Spika Ndugai, watajua kwamba vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu na za Wabunge wa upinzani zinamulikiwa taa na dunia”.







Ukisoma ujumbe wa Mh. Tundu Lissu ni wazi yeye njia ya kupata suluhu ni IPU (Inter-Parliamentary Union). Huko ndio litatoka shinikizo kwa utawala wa mabavu! Pia serikali ni ya Magufuli na bunge ni la spika Ndugai. Namna mtu anavyoandika mwenye kuelewa anaweza kujua fikra, mawazo au hata heshima mtu aliyonayo dhidi ya mamlaka, serikali na bunge.



Najaribu kuwaza ni namna gani Mh. Rais anaweza kuanzisha mchakato wa kurudisha utengamano nchini wakati huo huo kiongozi wa juu wa CHADEMA anahamasisha wabunge wa chama hicho watumie vyombo vya nje kuweka shinikizo dhidi ya nchi yetu? Mh. Rais anawezaje kuona ‘nia njema na ya dhati’ kwa upande wa CHADEMA wakati kiongozi wa juu wa CHADEMA anaendelea kusambaza ujumbe kwamba serikali yake ni ya mabavu? Najaribu kufikiria kwa sauti.



Mh. Freeman Mbowe ameandika kwa busara kubwa kabisa maneno haya,



“Nina hakika tunahitaji maridhiano ya Kitaifa. Kama viongozi tuna wajibu huo mbele ya wananchi wenzetu na hata mbele ya Mungu; na wewe kama Kiongozi Mkuu wa nchi yetu una turufu na wajibu wa kipekee kuwezesha matamanio haya ya haki kupatikana”.



Lakini Mh. Tundu Lissu, kwa mujibu wa ujumbe wake, kama wabunge wa CHADEMA wakikubali anaahidi,



“niko tayari kuwasaidia kuandaa hoja za kupeleka IPU au, bora zaidi, kuwaomba mawakili wangu wa London, yaani Amsterdam & Partners, kufanya hivyo kwa niaba yetu wote”



Kwa mfano huu wa alichokisambaza Mh. Tundu Lissu kwa wabunge wa CHADEMA wakati huo huo ambao Mwenyekiti wake Mh. Freeman Mbowe ameandika barua kwenda kwa Mh. Rais, Dkt John Pombe Magufuli aanzishe mchakato wa kutafuta utengamano wa kitaifa unaweza kuona kwa nini ni vigumu kufika huko ambako Mh. Freeman Mbowe anasihi tufike. Sio kwamba Mh. Tundu Lissu hapaswi au hana haki kutafuta haki yake sehemu yoyote anayoona inaweza kupatikana, la hasha. Ila hatua hizo kwa kiasi kikubwa sana zinaondoa uhalali au zinatia shaka kuhusu nia ambayo imeonyeshwa vizuri tu kwenye barua ya Mh. Freeman Mbowe. Na zaidi ya hilo, ni pale ambapo baadhi ya viongozi wa CHADEMA pamoja na Ndugu Zitto Zuberi Kabwe wanaendelea kushawishi mataifa ya nje wahisani pamoja na taasisi za fedha kuinyima nchi yetu misaada na kuifanya ionekane inakiuka haki za binadamu na utawala wa sheria kwa kiasi kikubwa. Hoja ambazo Mh. Tundu Lissu anaahidi kuwasaidia wabunge kupeleka IPU ndio hizo hizo zinazotumika kushawishi nchi yetu inyimwe misaada!! Majadiliano yanaanzia wapi?



Nimalizie kwa kusema wazi kabisa kwamba mara baada ya uchaguzi mpaka leo CHADEMA (na baadae ACT Wazalendo) wamekuwa wakitoa maneno ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa na lengo la kumdhalilisha na kumfedhehesha Rais. Hapa zinaweza kuibuka hoja nyingi tu kwa mfano, lugha zilizotumika sio matusi au za fedheha ndio kazi ya upinzani, ukiwa kiongozi lazima ukubaliane na matusi au fedheha nk.

Lakini ukweli utabaki kwamba kauli na majina kama 1. Dikteta uchwara 2. Mshamba 3. Muuaji 4. Jiwe 5. Meko na mengine mengi kamwe hayawezi kuwa ni maneno ya kufurahisha. Hata kama mtu akikaa kimya ni lazima tutambue kwamba kila mwanadamu ana moyo. Kwa wenzetu huko nje (Marekani na Ulaya) unaweza kusema ni sawa. Kiongozi anaweza akatukanwa hadharani na mtu akasema ni uhuru wa mawazo. Labda ndio maana huko kwa wenzetu pia leo wanaume wanaoana wenyewe kwa wenyewe na wanaona sawa. Huku kwetu ni tofauti.



Sasa tunapozungumzia utengamano wa kitaifa pamoja na mapendekezo yaliyotolewa tusisahau mambo ambayo yanaweza kuonekana ni madogo ila ni sababu ya mikwamo tunayoweza kuwa tunakutana nayo kila mara. Kitabu kimoja kinaitwa “Tipping Point: How Little Things Can Make a Big Difference” na mwandishi Malcolm Gladwell kinaelezea vizuri sana dhana hii ya mambo madogo ambayo kwenye maisha ni rahisi sana kutoyatilia maanani. Kama hakutakuwa na dalili za wazi kwamba lengo ni utengamano na sio njia ya kutafuta hatua za kisiasa (political mileage) basi itakuwa vigumu. Natambua kuongoza chama kama CHADEMA sio jambo rahisi hasa linapokuja suala la ‘compromises’ kwa manufaa ya nchi. Mh. Freeman Mbowe anaweza kuitwa kila jina. Na hata kuwashawishi tu kwamba ni jambo jema kufanya hivyo itakuwa sio rahis kama ilivyokuwa wakati wa kuhudhuria sherehe za Uhuru.



Ila ni muhimu [na lazima] CHADEMA kuchukua hatua na kuwaelekeza viongozi wote kusitisha uhamasishaji unaondelea dhidi ya nchi yetu. Haiwezekani kukaa kwenye majadiliano ya aina yoyote ile wakati kama nchi tunalalmikiwa IPU, European Union, World Bank, kwenye mabalozi mbalimbali nk. Pili CHADEMA iandike barua kumtambua rasmi Rais Dkt John Pombe Magufuli hata kama ni mwaka wake wa tano madarakani kuondoa dhana ya kutokumtambua. Wazungu wanasema ‘better late than never’ (heri uchelewe kuliko kutokufanya kabisa). Wanachama wa CHADEMA na baadhi ya viongozi ambao wanajulikana waache tabia ya kudhihaki mamlaka. Serikali ya Jamhuri ya Muungano ni Serikali halali iliyopo madarakani. Kama Chama, CHADEMA itoe tamko kuelekeza hivyo ili basi nia njema iweze kuonekana kwenye walichoandika na sio njia ya kufikia uchaguzi 2020 ambao tayari CCM imeshajiandaa vya kutosha kushinda kwa kura za wananchi.
Labda wewe mwenzetu unasaidie, je, hicho kinachozungumzwa na hao wapinzani kina uhalisia? Wanalalamika watu kupotea, kupigwa risasi, na kukatazwa kufanya shughuli za kisiasa za kutafuta wanachama pahali popote Tanzania lakini wanazuiwa. Je, hayo malalalamiko ni ya kweli?
 
Kuna kitu Lissu anawaza kukifanya kwa unyama aliotendewa na JIWE.
 
Labda wewe mwenzetu unasaidie, je, hicho kinachozungumzwa na hao wapinzani kina uhalisia? Wanalalamika watu kupotea, kupigwa risasi, na kukatazwa kufanya shughuli za kisiasa za kutafuta wanachama pahali popote Tanzania lakini wanazuiwa. Je, hayo malalalamiko ni ya kweli?
Kajiunga JF nov 2019, tia akili kichwani hiyo ni new recruit ya polepole
 
Kajiunga JF nov 2019, tia akili kichwani hiyo ni new recruit ya polepole
Sasa how would you recruit an individual of empty head like this? For what purpose? Shame on them.
 
Uzi wako summary yake ni kwamba mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na kulia!

Yaaaani mtu akimbaka mkeo, nenda na wewe mume ukabakwe!

Akili matope kweli....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom