jijiletublog
Member
- Jul 23, 2020
- 31
- 74
Anaandika Mhenga wa Wahenga, Kaskazini
Kuna baadhi ya nyaya katika bongo za wenzetu CHADEMA zimelegea na tusipowaangalia vizuri nyaya hizo zitalipuka.
Chadema wameamua kuwafanya Watanzania ni maamuma wa sheria kiasi cha kufikia hatua ya kuwadanganya hata katika mambo ambayo yapo kwa mujibu wa sharia na yapo kwenye katiba.
Huu ni mfano wa Chadema kuwahadaa Watanzania kuwa wakishika dola watafanya lakini mambo hayo yalifanyika, yamefanyika na yanaendelea kufanyika kwani yako kwenye katiba hivyo yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.
Katika Ilani yao ya Uchaguzi ya mwaka huu, ukurasa wa 16, wanasema: Kwa kuwa Chadema inapigania haki, usawa na ushirikishwaji wa jamii pamoja na mifumo huru ya sheria na utoaji haki; na kwa kuwa Chadema inatambua kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria.
Na kwa kuwa Chadema inapenda kila mtu atendewe haki; na kwa kuwa Chadema inakusudia kujenga jamii yenye uadilifu na tabia njema ambapo vitendo vya kihalifu vinapunguzwa au kutokomezwa; hivyo basi, Serikali ya Chadema itafanya mambo yafuatayo katika eneo la utoaji haki:
a. Itawachukulia na kuwahesabu
watuhumiwa wote kama watu wenye haki hadi hapo mahakama itakapowatia hatiani.
Ufafanuzi: Kwa mujibu wa Sheria, Ibara ya 13(6)b ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977; Ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo’’
Hiyo ni sheria imetamka hayo, sasa Chadema wanatuaminisha kuwa watafanya hayo wakati sheria iko wazi na mahakama zetu zimekuwa zikitenda haki bila kuingiliwa na mtu yeyote.
b. Itahakikisha kwamba mhimili wa mahakama unakuwa huru na kwamba hauingiliwi na mtu, chombo au taasisi yoyote katika kutoa uamuzi wake ili kuhakikisha kwamba, haki inatolewa bila upendeleo wowote.
Ufafanuzi: Kimsingi mahakama ina kazi ya kutumia sheria zilizopo na kuamua juu ya matumizi yao.
Mfumo wa Mahakama nchini umeundwa na mahakama za ngazi mbalimbali na haiingiliwi na Serikali wala mtu mwingine yeyote.
c. Itahakikisha kuwa, Magereza yote yanatumika kama vituo vya kurekebisha tabia na kujenga mahusiano mapya badala ya kuwa sehemu za kuadhibu na kutesa wananchi.
Ufafanuzi: Suala hili nalo lipo kwa mujibu wa katiba ambapo Sheria ya Magereza ya mwaka 1967 ilitungwa mahsusi kwa kuzingatia zaidi nia ya Sheria za Kimataifa za kujali haki za msingi za binadamu kwa.
Katika hilo ndipo yalianzishwa magereza ya mashamba ya mazi katika maeneo ya vijijini yaliyoteuliwa yawe vituo vya umahiri kwa kuelimishia stadi za kilimo kwa wafungwa na kueneza huduma hiyo kwa jamii zinazozunguka.
Sheria hiyo ilitungwa baada ya uhuru ambapo sera mpya ya Magereza ilitayarishwa na kutumika kwa kuzingatia kuwatendea wafungwa ubinadamu na haki kuwa ni maadili makuu ya sera ambapo madhumuni yalikuwa urekebishaji wa wahalifu kama mchango kwa usalama wa jamii kwa vitendo, mabadiliko haya ya mwelekeo wa kifalsafa.
Katika hilo, ndipo vikaanzishwa vituo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi katika mikoa ya Mbeya na Morogoro kwa mafunzo ya stadi kwa wafungwa. Mafunzo haya yamehusishwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ya Taifa ili vyeti vya wahitimu vitambuliwe.
Kwa kifupi tu ni kwamba hadi sasa Magereza ina taasisi 122, ofisi za mikoa 21, Vyuo vya Mafunzo ya Watumishi viwili, Vituo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi vinne na Makao Makuu.
Chadema wasifikiri Watanzania wataokotwa kwa kauli chonganishi dhidi ya CCM na mgombea wake Dk. Magufuli, watambue kwamba Watanzania wa sasa si wale wanaowafahamu, Watanzania wa sasa wanajitambua na wanajua thamani ya Dk. Magufuli, wasihadaiwe.