Nimekuwa Geita kikazi nikagundua CCM ilishafutika kabisa kule na Chadema inaweza shinda Jimbo lolote kule .
Kuanzia Bukombe, Geita mjini, Geita vijijini, Sengerema Buchosa hakuna kabisa kitu kinaitwa CCM..
Watu wanasema wazi walimchagua Magufuli kwa kujuwa atawaletea maendeleo na Katiba mpya baada ya kusema Magufuli for change (M4C).
Watu pia wanakazia kwa kusema baada ya kumchagua wakampa na wabunge ili hasiwe na kisingizio ila ni kama vile aliwasaliti..
Baada ya kuwachomea nyavu zao za uvuvi kisa uvuvi haramu na maelfu ya watu kukosa ajira.
Wengine wanasema maendelea yaliyopo Chato mengi hayaleti uhalisia mfano uwanja wa ndege wangapi wanapanda ndege? Hifadhi je wangapi wanapesa za kuingia kwenye hifadhi?
Wanasema kuna shule bado hazina walimu wa kutosha mkoa wa Geita, Hakuna madactari na manesi kwenye hospital ndani ya mkoa.
Pia wanasema bado Kuna tatizo la ulinzi na usalama mkoa wa Geita ambapo matukio ya watu kuuwawa kikatili yanatokea Sana huku polisi wakiwa busy na kuwafunga wakosoaji wa Magufuli na vyama pinzani.
Wanasema duka la MSD madawa yanauzwa Bei sawa na maduka ya dawa na wanufaika wakuu sio wanachi wa chato, Wazee na watoto na wamama bado wanna changamoto ya matibabu.
Wakazi wa chato wanasema sanasana gharama za maisha zimepanda Chato tofauti na zamani kutokana na watu kuamini kwamba Chato sasa Kuna pesa na kuanza kupeleka vitu kwa Bei ya juu.
Hayo ndio niliyoyaona Chato na Geita mtu wao watu wengi hawataki kabisa kumsikia.
Nikipata nauli nitaenda Kagera kule kwenye Tetemeko halikuletwa na Serikali nione uhalisia.
View attachment 1548948