Mpango wa kuchangia ni mzuri. Naomba Chadema iwe wazi kujulisha wapenzi wake kuwa imepata michango kiasi gani mpaka sasa na michango hiyo imesaidiaje kwenye kampeni zinazoendelea. Hilo linaweza kuwapa moyo zaidi wapenzi watakapotambua kwamba michango yao kidogo kidogo ina manufaa makubwa.