Elections 2010 CHADEMA iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee

Elections 2010 CHADEMA iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee

Status
Not open for further replies.
Inasikitisha sana na kwa kweli inaumiza sana kuyasikia hayo, hii inazidi kuipa nguvu ile dhana ya kuwa upinzani wa Tanzania ni vurugu mechi, yawezekanaje watu walioshinda waenguliwe na walioshindwa wapite?

Mwawafanya wale scores of wanachama waliowapitisha kuwa hawana akili ila nyie kikundi kidogo cha watu ndo mna jua zaidi? CHADEMA wanaanza kukiuka misingi ya de mokrasia ilhali hawajapewa nchi sasa wakipewa nchi watafanyaje?

kama watafanya haya chadema watadhihirisha wao si chama cha kidemokrasi, angalia sakata la marehemu chacha wangwe na mgawanyo wa viti maalum ulivyokuwa umeegemea kanda moja ya nchi badala ya kuwa equal kwa nchi nzima, kumbuka suala la zito kugombea uenyekiti na mbowe, angalia uchaguzi wa viti maalum ulivyoahirishwa kisa tu baadhi ya notable figures hazikuchaguliwa na sasa tukio la washindi halali kuenguliwa na badala yake wasiotakiwa na watu kupita, im very disappointed with chadema ,please waacheni wananchi wachague maana hiyo ndiyo demokrasia ya ukweli, a leadership of the people by the people and for the people
 
Mwanakijiji,

Hayo tisa, yanayoendele kwenye teuzi za viti maalum ndio kichefuchefu kabisa!. Baada ya wapendwa wa "wazee" kushindwa vibaya kwenye mchujo halali wa BAWACHA, Mwenyekiti Mbowe kaamua uteuzi utafanywa na kamati "maalum" na sio kupitia uchaguizi wa BAWACHA tena.

Ikumbukwa miaka 5 iliyopita uteuzi wa viti hivi ulileta malalamiko sana hususan ya ukabila na udini kwa maana ya uchaga na ukristo. Ili kuondokana na hilo ikaamuliwa kuwa teuzi zifanywe na zisimamiwe na BAWACHA wenyewe. Uchaguzi umefdanyika na kwa bahati mbaya wabunge wote kasoro Lucy Owenye wameshindwa. Lakini kigugumizi kimeshaanza kwa Mbowe kukumbatia makabrasha ili akachague mwenyewe awatakao.

Chadema hakuna u-badala wowote ni wababaishaji, wakabila na wadini period!
 
Good move, ninapoona watu wanaichambua Chadema huwa nafarijika sana kumbe sasa Chadema imekua, kwenye nchi yeyote ukiona vimejitokeza angalau vyama viwili au vitatu jua demokrasia inakua.

Lakini nikukumbushe MMKJ uliwahi kusema CCM iwaache wapiganaji waingie bungeni hata kwa gharama yeyote wala isiwasumbue na kweli inavyoonekana CCM wanamfanyia Bashe kama ulivyowahi kusema ni upi msimamo wako mbona Chadema wamefanya yale yale uliyoshauri una argue differently.
 
...ndani ya week hii ulishawahi kusema kwenye post yako kuwa "angalau CCM wangewarudisha wapiganaji kama vile Selelii, Kimaro" ili wakapambane vizuri, wakati huo hukuona umuhimu wa kura ya maoni na leo hii unaona umuhimu wa kura ya maoni.
Jamaa ni shabiki, anaenda na upepo wa anachojisikia siku hiyo kitanufaisha upande wake. Akiwa anampenda Selelii atasema NEC wamrudishe, akimpenda Mtema atasema CHADEMA wasimwondoe. Ovyo, na ndio mwandishi wa CHADEMA, mshauri, mpiga debe.

ban.kijiji.jpg

M. M. Mwanakijiji

jumatano, 4 agosti 2010

Wabunge waliogongana Richmond warudishwe

JUZI Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walipiga kura ...ni hatua ya awalikabla ya majina ya washindi kufikishwa kwenye vikao vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) ambavyo vina uwezo wa kupindua matokeo kwa kadiri ya utashi wao.

Tayari matokeo yanaonyesha kwamba baadhi wameanguka kama Lucas Selelii, James Lembeli, Alocy Kimaro na wengine. Hili kundi ambalo lilijikuta linakipasua Chama Cha Mapinduzi kufuatia sakatala la kashfa ya Richmond na masuala mengine ya ufisadi.

Wana CCM kwenye kura za maoni wamefanya makosa makubwa kuamua kuwaondoa wachezeaji uwanjani badala ya kuja na kumaliza kipindi cha pili ati kwa vile wameonewa na kufungwa mabao mawili.

Ni kwa sababu hiyo ninaamini wabunge wafuatao warudishwe bungeni ili wakamalizie mechi yao kwani katika Tanzania ya leo

...Peter Serukamba (Kigoma Mjini), Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), Lucas Selelii (Nzega), Aloyce Kimaro (Vunjo) na Said Juma Nkumba (Sikonge).

NEC ifanyie taifa hisani kwa kurudisha kundi hili zima bungeni ili wakamalizie mechi waliyoianzisha.
 
Kama mambo yenyewe ndiyo hayo ya kuenguliwa baada ya kushinda kura za maoni, kwanini kulikuwa na kura za maoni at the first place?. Ni bora hivyo vikao vya juu vya Chadema na CCM vikachagua wagombea wake bila ya kuwasumbua wananchi kupiga kura za maoni. This is rubbish 100%
 
Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao. Chadema haiwezi kuendelea kusubiria viti vya vijana au wanawake ili kuwapa nafasi za kugombea.

Tunahitaji vyama vya upinzani viongeze idadi ya wabunge ili kuweka balance of power bungeni, na mpaka sasa wagombea wa vyama vya upinzani katika majimbo mengi ni dhaifu sana kuweza kuleta upinzani wa maana kwa wagombea wa CCM.

Ili wapinzani wapate wabunge wengi, hawatakiwi kupeleka tu watu wa kushiriki kwenye uchaguzi na kuweka historia bali kupeleka wagombea wenye uwezo wa kujenga imani ya wananchi na kushinda uchaguzi.

Naiunga mkono Chadema katika hili.
 
Lakini kama ukiambiwa kwamba kuna ushahidi kwamba hao R walipewa pesa na CCM na walitumia pesa na pia pesa haramu kushinda, utasema nini?
Hata mimi sikuelewa kabla sijapewa sababu za kuwang'oa...na kama ni watoa rushwa, tena imetolewa CCM basi bora tu wadondoshwe!
 
Hayo tisa, yanayoendele kwenye teuzi za viti maalum ndio kichefuchefu kabisa!. Baada ya wapendwa wa "wazee" kushindwa vibaya kwenye mchujo halali wa BAWACHA, Mwenyekiti Mbowe kaamua uteuzi utafanywa na kamati "maalum" na sio kupitia uchaguizi wa BAWACHA tena.

Ikumbukwa miaka 5 iliyopita uteuzi wa viti hivi ulileta malalamiko sana. Uchaguzi umefdanyika na kwa bahati mbaya wabunge wote kasoro Lucy Owenye wameshindwa. Lakini kigugumizi kimeshaanza kwa Mbowe kukumbatia makabrasha ili akachague mwenyewe awatakao.
!

Katika hili Chadema iige utaratibu wa CCM kuwapata wabunge wa Viti Maalum, katu wasirudie makosa ya 2005.
 
Binafsi nasikitika sana kama CHADEMA wanaweza kuwadidimiza wadada kama Regia na Rachel:shocked:!

Bahati nzuri Rachel namfahamu na nimeona the great potential that she has siyo kwa vile ni mwanamke bali kwa vile ni kijana anayejiamini sana na mwenye kila sifa na mvuto wa kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi.Nilifarijika kuona kaweza kuwabwaga wapinzani wake kwenye kura za maoni na nilikuwa na matumaini makubwa mno kwake.Kuwapoteza watu kama hawa kwa vile wenye maamuzi humo chamani wana watu wao wanaotaka kuwazawadia kwa sababu wazijuao wenyewe ni utawala mbovu wa kiwango cha juu!!
Kwa hili nawapa ZIIIIIII chadema!:A S angry:
 
ban.kijiji.jpg

M. M. Mwanakijiji

jumatano, 4 agosti 2010

Wabunge waliogongana Richmond warudishwe

Wana CCM kwenye kura za maoni wamefanya makosa makubwa kuamua kuwaondoa wachezeaji uwanjani badala ya kuja na kumaliza kipindi cha pili ati kwa vile wameonewa na kufungwa mabao mawili.

Ni kwa sababu hiyo ninaamini wabunge wafuatao warudishwe bungeni ili wakamalizie mechi yao kwani katika Tanzania ya leo

...Peter Serukamba (Kigoma Mjini), Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), Lucas Selelii (Nzega), Aloyce Kimaro (Vunjo) na Said Juma Nkumba (Sikonge).

NEC ifanyie taifa hisani kwa kurudisha kundi hili zima bungeni ili wakamalizie mechi waliyoianzisha.
Asante sana Tindikali nilikuwa natafuta makala hii niibandike.

MMKJ anasema wanaCCM wamefanya makosa kuwaondoa wapiganaji warudishwe hata kama hawakushinda, kwa CCM ni sawa, likifanywa na Chadema the same MMKJ anasema 'Chadema iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee' kama si kutafuta angalau kadosari kokote ndani ya Chadema ili aiseme ni nini.

Infact i dont understand this guy nowdays, toka ajichanganye na CCJ ame lose control ya kufikiri he is not the same again. Anajitahidi sana asionekane kijani kwa kujifanya yeye nuetral kama yupo kama hayupo red(Chadema).

Nilisha mwambia asipoangalia atapoteza credibility yake lakini yeye he doesn't care anasema hatafuti umaarufu ni sawa basi uwe consistent na mambo yako uta lose kote kote. This is another grave mistake to you like that of CCJ.
 
Binafsi nasikitika sana kama CHADEMA wanaweza kuwadidimiza wadada kama Regia na Rachel:shocked:!

Bahati nzuri Rachel namfahamu na nimeona the great potential that she has siyo kwa vile ni mwanamke bali kwa vile ni kijana anayejiamini sana na mwenye kila sifa na mvuto wa kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi.Nilifarijika kuona kaweza kuwabwaga wapinzani wake kwenye kura za maoni na nilikuwa na matumaini makubwa mno kwake.Kuwapoteza watu kama hawa kwa vile wenye maamuzi humo chamani wana watu wao wanaotaka kuwazawadia kwa sababu wazijuao wenyewe ni utawala mbovu wa kiwango cha juu!!
Kwa hili nawapa ZIIIIIII chadema!:A S angry:

Imekuchukua muda mrefu kuwajua hao viongozi wako, uliambiwa hao ni wababaishaji tu hiyo ni NGO ukaona umefika. Usilie stahamili ndio ukubwa huo..
 
kwanini mpendazoe asiende kishapu, mimi namuona amekurupuka kufanya maamuzi. je chadema kishapu kuna nani
na kama hakubaliki kishapu then kuna kitu wrong about him
 
kwanini mpendazoe asiende kishapu, mimi namuona amekurupuka kufanya maamuzi. je chadema kishapu kuna nani
na kama hakubaliki kishapu then kuna kitu wrong about him

Kwanini aende Kishapu kama anaona kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kushinda Segerea?naamini alijipima kabla ya kufikia uamuzi huo.
 
Mwenyekiti inaonekana wewe nawe ni mwepesi sana wa kusahau maana ndani ya week hii ulishawahi kusema kwenye post yako kuwa "angalau CCM wangewarudisha wapiganaji kama vile Selelii, Kimaro" ili wakapambane vizuri, wakati huo hukuona umuhimu wa kura ya maoni na leo hii unaona umuhimu wa kura ya maoni.
Jaribu kutafakari kuhusu kauli zako mkuu maana zinakingana.

hukuelewa nilichoandika labda uitafute ile sredi uisome tena.
 
Kwamba wagombea kama Regia Mtema (kilombero) na Rachel Mashishanga (Segerea) wameombwa kuachia nafasi zao kuwapisha watu wengine (wote wanaume) ni jambo la kufanya watu kutikisa vichwa vyao.

Moyo wa ujasiri uliooneshwa na kina dada hao hata wakaamua kugombea kwenye majimbo na kuonekana kuwa wako tayari kuhukumiwa na wapiga kura wote ni jambo ambalo Chadema inapaswa na ilipaswa kulitetea na kuwapigania hadi dakika ya mwisho. Kina dada hawa wameonesha ujasiri na utayari ambao haupaswi kubomolewa kwa sababu Makao Makuu wanataka watu fulani.

Mpendazoe na huyo wakili wa Kilombero wote walikuwa na nafasi ya kugombea toka mwanzo kama wangetaka. Lakini haya ya kuonekana kubebwa na chama kwa sababu yoyote hayaoneshe "demokrasia" bali ukiritimba wa mfumo dume ambao utawasumbua Chadema baadaye. Ni kweli kuwa katika nafasi karibu zote za juu za Chadema zinashikiliwa na wanaume lakini sitaki kuamini kuwa hilo pekee linaweza kuwafanya wasione umuhimu wa kuwalinda wagombea wake waliojitokeza.

Kina R n R wasikate tamaa kwani hata kama wataenguliwa ukweli unabakia umeandikwa kuwa walishinda kura za maoni na walienguliwa na chama si kwa sababu ya rushwa au tuhuma za kukiuka maadili bali kwa sababu walikuwa ni aidha ni wanawake au hawakuwa tayari kupiganiwa na chama hadi ushindi.

Binafsi nasikitika sana kama CHADEMA wanaweza kuwadidimiza wadada kama Regia na Rachel:shocked:!

Bahati nzuri Rachel namfahamu na nimeona the great potential that she has siyo kwa vile ni mwanamke bali kwa vile ni kijana anayejiamini sana na mwenye kila sifa na mvuto wa kuchaguliwa kuwawakilisha wananchi.Nilifarijika kuona kaweza kuwabwaga wapinzani wake kwenye kura za maoni na nilikuwa na matumaini makubwa mno kwake.Kuwapoteza watu kama hawa kwa vile wenye maamuzi humo chamani wana watu wao wanaotaka kuwazawadia kwa sababu wazijuao wenyewe ni utawala mbovu wa kiwango cha juu!!
Kwa hili nawapa ZIIIIIII chadema!:A S angry:

Siiungi mkono Chadema katika uchaguzi mkuu ujao, lakini kulifanya hili kuwa ni sababu ya mfumo dume ni upotoshaji wa kiwango cha juu.
 
Lakini nikukumbushe MMKJ uliwahi kusema CCM iwaache wapiganaji waingie bungeni hata kwa gharama yeyote wala isiwasumbue na kweli inavyoonekana CCM wanamfanyia Bashe kama ulivyowahi kusema ni upi msimamo wako mbona Chadema wamefanya yale yale uliyoshauri una argue differently.

Hapana sijawahi kusema hivyo; ninachagua maneno yangu vizuri.
 
Asante sana Tindikali nilikuwa natafuta makala hii niibandike.

MMKJ anasema wanaCCM wamefanya makosa kuwaondoa wapiganaji warudishwe hata kama hawakushinda, kwa CCM ni sawa, likifanywa na Chadema the same MMKJ anasema 'Chadema iwaachilie walioshinda kura za maoni wagombee' kama si kutafuta angalau kadosari kokote ndani ya Chadema ili aiseme ni nini.

Infact i dont understand this guy nowdays, toka ajichanganye na CCJ ame lose control ya kufikiri he is not the same again. Anajitahidi sana asionekane kijani kwa kujifanya yeye nuetral kama yupo kama hayupo red(Chadema).

Nilisha mwambia asipoangalia atapoteza credibility yake lakini yeye he doesn't care anasema hatafuti umaarufu ni sawa basi uwe consistent na mambo yako uta lose kote kote. This is another grave mistake to you like that of CCJ.

someni maelezo yangu kwenye ile thread.. maneno hayo mekundu ya kwanza si ya kwangu; ni ya mhariri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom