Makada watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefungua shauri katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma wakilalamikia kitendo cha kuvuliwa nafasi zao za uongozi kiholela na bila kupewa fursa ya kusikilizwa, kinyume na katiba ya chama hicho.
Akiashiria msingi wa shauri hilo mbele ya waandishi wa habari leo, Agosti 20, 2026, wakili anayewawakilisha makada hao, Jonathan Mndeme aliyeambatana na Wakili Joseph Kipeche ameeleza kuwa hatua ya wateja wake kwenda mahakamani inalenga kuomba idhini ya kufanya mapitio ya kisheria dhidi ya maamuzi yaliyochukuliwa dhidi yao.
Wakili Mndeme amefafanua kuwa walalamikaji katika shauri hilo: Barnabas Okola, Joseph Mwakidasi, Mathias Cosmas, Abubkadi Mashambo, na Lembrus Mchome waliondolewa madarakani kwa barua bila kufuata taratibu za kikatiba zinazomtaka kila mwanachama au kiongozi kuitwa na kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua.
“Kumekuwa na sintofahamu ya uamuzi wa wateja wetu kwenda mahakamani. Katika katiba ya chama chao, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua hadi aitwe kwenye kikao ajieleze. Kama unakuwa na taasisi ambayo watu wanaamka tu na kufukuza viongozi, kuna shida sehemu na ndio maana wapo mahakamani kuomba idhini ya mapitio,” amesema Wakili Mndeme.
Pamoja na ufafanuzi huo, Mndeme amekanusha vikali madai yanayosambazwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA kuwa wateja wake wana nia ya kuzuia mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho, akisisitiza kuwa hakuna maombi au amri yoyote ya aina hiyo iliyowasilishwa mahakamani.