GE2025 CHADEMA kanda ya kati yalaani utekaji wa kiongozi wa kata ya Ikungi na mwendesha Bodaboda

GE2025 CHADEMA kanda ya kati yalaani utekaji wa kiongozi wa kata ya Ikungi na mwendesha Bodaboda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
TAARIFA KWA UMMA​

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kati tunatoa taarifa kwa umma na kulaani kitendo cha utekaji wa kiongozi wa kata ya Ikungi anayejulikana kwa jina la Issa Hamis Kaudo na kijana wa boda boda Ndugu Paul Veslas.

Jana tarehe 03.10.2025 mnamo saa 12 jioni Issa Hamis ambaye ni fundi wa kuchomelea mageti (grill) alipigiwa simu na mtu aliyetambulisha kuwa mfanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi kuwa aende kuna kazi, walipofika maeneo hayo ya halmashauri. Kwa maelezo ya Mlinzi wa Halmashauri ya Ikungi alisikika kelele na kushuhudia watu zaidi ya watano wakiwavuta na kuwaingiza kwenye gari jeupe aina ya Land Cruiser lililokuwa limesimama maeneo hayo ya halmashauri. Tangu jana baada ya kukamatwa huko hawajaonekana.

Polisi pamoja na kupokea taarifa hiyo wako kimya hadi sasa. Kwa mkoa wa Singida hili sio tukio geni la kuteka na kuua, yamekuwa yakitokea na jeshi la polisi haliji na majawabu.

Chama Kanda ya Kati kwa kushirikiana na viongozi wa mkoa, wilaya na ndugu tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu kujua hatima ya ndugu zetu.

SHUJAA S. EVARIST
Afisa CHADEMA Kanda ya Kati.
Imetolewa tarehe 4 Oct 2025.

1759642855318.png
 
Back
Top Bottom