Kamati Tendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Serengeti imelitaka Jeshi la Polisi kutoa maelezo ya wazi na ya kina kwa umma kufuatia uamuzi wake wa kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanawake wa chama hicho na waumini katika eneo la Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma mkoani Mara wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Katika tamko rasmi lililotolewa leo, Machi 17, 2026, Mwenyekiti wa Kanda hiyo, Lucas Ngoto, amesisitiza kuwa matumizi ya nguvu yaliyoshuhudiwa tarehe 8 Machi yanahitaji majibu ya kuridhisha kwa jamii, kwani yalihusisha uvamizi wa eneo la ibada na ukiukwaji wa haki za kikatiba za wananchi kukusanyika kwa amani.
Kamati hiyo imebainisha kuwa kuna haja ya polisi kuelezea mantiki ya kurusha mabomu ya machozi wakati ibada ikiwa inaendelea, jambo ambalo limeonekana kama dharau kwa taasisi za dini na imani za wananchi.
"Kamati Tendaji ya Kanda ya Serengeti inalitaka Jeshi la Polisi kutoa maelezo ya wazi kwa umma kuhusu tukio la matumizi ya mabomu ya machozi dhidi ya wanawake waliokusanyika kwa amani", amesema Lucas Ngoto.
Mbali na kutaka maelezo ya operesheni hiyo, CHADEMA imelaani vikali kile ilichokiita "njama za makusudi" za polisi kuwatisha viongozi wa kanisa siku moja kabla ya tukio. Kamati imeeleza kuwa vitisho hivyo vililenga kuzuia viongozi wa dini kutoa nafasi kwa wanawake wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) kuadhimisha siku yao kimataifa.
Mwenyekiti Ngoto ametoa pole kwa Baba Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma, mapadri, na waumini wote waliojikuta katika taharuki hiyo.
Ameongeza kuwa kitendo cha polisi kuingilia eneo takatifu la ibada ni kielelezo cha ukosefu wa utu na unyeti wa kijinsia.
Aidha, CHADEMA Kanda ya Serengeti imewapongeza wanawake na viongozi wa BAWACHA Taifa waliofika Musoma licha ya vizuizi na kashfa, ikisisitiza kuwa haki ya kukusanyika haiwezi kuzimwa kwa vitisho wala mabomu.
Kamati imetoa rai kuwa amani ya kweli itapatikana tu pale serikali itakapoacha kutumia nguvu na kuanza kusikiliza sauti za wananchi wake.
Soma pia Musoma: Polisi Wawatawanya kwa Mabomu ya machozi BAWACHA
Chanzo: Jambo TV