CHADEMA na Makamanda wajifunze Mbinu za Medani?
Una maana hadi hapa walipofikia hawajui hata adui yao ni nani?
Huenda unataka kukumbushia na kukazia tu wasipoteze lengo.
Ushahidi sasa upo wazi kabisa ni jinsi gani adui alivyo 'frustrated' na mbinu za CHADEMA wanazozitumia, iwe ni kwa bahati tu au kwa mpangilio maalum.
Adui amefanya kila kitu kuwachokoza CHADEMA ili waangukie kwenye mtego ili awamalize, lakini imeshindikana. Sasa imebaki adui anahangaika na kutapatapa, huku waTanzania wakiendelea kuelewa adui mkubwa wa nchi hii ni nani.
Kwa hiyo, wakati huu si wakati tena wa kujuwa adui ni nani. Anafahamika, na wananchi wanazidi kumfahamu adui huyo kwa sababu kafunuliwa wazi na CHADEMA.
Mbinu za kupambana na adui? Kutapatapa kwingi kunakofanywa na adui wakati huu ni ishara bora zaidi ya kujuwa kwamba mbinu wanazozitumia CHADEMA zinafanikiwa. Wanachotakiwa kukifanya ni kuziendeleza hivyo hivyo na kuzi'refine' ziweze kumweka uwazimu zaidi adui azidi kujitoa uchi uchi hadharani.
Kwani wanaCHADEMA kukaa mahabusu ni adhabu ya kifo? Ingetakiwa kila eneo sasa watu waendelee kujitokeza na kujitoa mhanga kukaa mahabusu bila ya kuvynja sheria yoyote. Hiyo ni beji ya heshima kubwa katika ukombozi wa taifa hili kutoka kwa hawa maadui wa nchi yetu.