Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche ametaja maazimio matano ya chama hicho, akisema wataandika barua kwa jumuiya za kimataifa wakiziomba zitume waangalizi kuja kukagua mifumo ya uchaguzi inayolalamikiwa kuunganishwa na CCM ili kukipa ushindi.
Madai ya mifumo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuunganishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kuiba uchaguzi, yalitolewa hivi karibuni na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, lakini yalikanushwa na viongozi wa mamlaka hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 27 kupitia mtandao wa Zoom, Heche amesema pia watauandikia Umoja wa Mataifa (UN), Marekani (US), Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Afrika na Mahakama ya Afrika kuomba watume waangalizi kukagua mifumo hiyo wanayoilalamikia.
Pia amesema wataandikia viongozi wa majeshi nchini na viongozi wa dini kuwaeleza malalamiko yao kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu.