Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kinaanza mchakato wa kudai katiba mpya katiba pendekezwa ya wananchi kwani ndio suluhu ya mambo yote yanayoendelea na figisufigisu zilizoendelea huko nyuma hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA huko Mkuranga Pwani kwenye Harambe ya Ujenzi wa ofisi ya CHADEMA.
Katibu Mkuu Dkt. Mashinji kwa niaba ya ofisi yake amechangia sh. 3,000,000 (milioni 3) cash kuchangia ujenzi wa ofisi ya Chadema wilaya ya Mkuranga.
Jumla ya ahadi ya fedha katika harambee ya kuchangia ofisi ya Chadema wilaya ya Mkuranga ni Tsh. 9,900,000
Pesa Taslim (Cash) 4,700,000
1) Naona mmeishiwa hoja zote na sasa mnarudi nyuma kudai yale ambayo mmeshashindwa.
2)Kipindi cha uchaguzi mlichangisha fedha kwa njia ya mtandao.Zilipatikana shilingi ngapi ?