CHADEMA kuanza mchakato wa Katiba Mpya

CHADEMA kuanza mchakato wa Katiba Mpya

wewe ndugu nakuonea huruma maana suala la katiba mpya linakuhusu hata WEWE ikiwa CDM wameona vema kupigania basi Mwenyezi Mungu yupo atabariki uaminifu.

lakini wewe unafanya kana kwamba KATIBA MPYA ni suala la UPINZANI tu, hii katiba ya sasa hivi inayolinda wachache itakuumiza hata WEWE mwananchi unayeleta ushabiki wa kisiasa usiokuwa na manufaa kwa nchi yetu. labda kama wewe ni mmoja wa hao wachache wanaolindwa na hii katiba ya sasa lakini kama wewe ni "msakatonge" basi nakushauri achana siasa UCHWARA zinduka akili!
Kuzinduka akili ni kuachana na Siasa za Wadanganyifu UKAWA period!
 
Kuzinduka akili ni kuachana na Siasa za Wadanganyifu UKAWA period!

kwahiyo chama tawala ndo wasema ukweli? mimi sifungamani na chama chochote kile lakini on the measure of truth nafikiri siasa za udanganyifu zinatoka chama tawala kwasababu katika miaka 45+ waliyoshika nchi ni mengi yameahidiwa lakini hayajatimizwa au yanatimizwa nusu inaishia hapo.

sisemi kuwa upinzani ukishika nchi hali itabadilika kwasababu moja tu; HAWAJAPATA NAFASI YA KUTAWALA. watakapoweza kushika hatamu za urais ndipo tutaweza kuona kama nao ni wadanganyifu au la ila for the moment, CCM ndo chama tawala na so far, udanganyifu kwa kiasi kikubwa unawadondokea wao kama chama tawala.

hata ilani ya chama yenyewe imekuwa ikibezwa na baadhi ya wanachama wa CHAMA TAWALA sasa si udanganyifu huo? siasa sio mpira; UPINZANI sio UADUI; kuna haja ya kuachana na chuki zisizo na maana na kushutumiana kusiko na faida kwa nchi yetu na kupambana kwa hoja nzito zenye mashiko na ueledi.
 
Back
Top Bottom