SI KWELI PreGE2025 CHADEMA kufanya maandalizi ya wagombea Ubunge na Udiwani kwa Siri

SI KWELI PreGE2025 CHADEMA kufanya maandalizi ya wagombea Ubunge na Udiwani kwa Siri

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Wakuu, JamiiCheck hii barua ni ya kweli.

Maria CHADEMA Hawaaminiki.jpg
Chadema Siri.jpg


​
 
Tunachokijua
Madai

Kuanzia Julai 1, 2025 kumekuwa na barua inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikielezwa kuwa imetolewa na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ikiwa na kichwa kinachosomeka;

“YAH: MAELEKEZO YA KUFANYA MAANDALIZI YA WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI KWA SIRI KUBWA - UCHAGUZI MKUU 2025”

Pia kuna grafiki zenye nembo ya chombo cha habari cha Mwannchi kikiwa na ujumbe kuwa “Maria Sarungi Asema: CHADEMA Hawapaswi Kuaminika Tena”.

Grafiki hiyo imeambatanishwa na barua iliyotajwa hapo juu pamoja na kinachoonekana kuwa ni ‘screenshot’ ya ujumbe aliouchapisha Maria Sarungi kupitia ukurasa wake wa X. Tazama hapa

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli. Barua inayosambazwa ikiwa na nembo ya CHADEMA ni ya kughushi kwani haijatolewa na chama hicho.

JamiiCheck imebaini kuwa barua hiyo ni ya kughushi kwani ina baadhi ya mapungufu kadhaa ikiwemo utofauti wa mwandiko (fonts) aina ya nembo ya CHADEMA iliyotumika ni tofauti na inayotumiwa katika machapisho mengine ya chama hicho.

Picha ya skrini inayoonesha kuwa Sarungi alichapisha taarifa akiwatuhumu CHADEMA kuwa ni wasaliti kutokana na barua hiyo, ni ya kughushi kwani haikuchapisha yeye hivyo haipo katika ukurasa wake rasmi wa X.

Aidha grafiki inayotumika kusambaza taarifa hiyo haijachapishwa wala kutolewa na Mwanchi. Grafiki hiyo ina mapungufu kadhaa ikiwemo makosa ya kiundishi, pamoja na mpangilio.
jamani mbona HAMUELEWI hata mkifoji barua #NOREFORMSNOELECTION
 
Back
Top Bottom