PreGE2025 Chadema kugomea kusaini maadili ya uchaguzi wamelenga nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Busara ingekuwa kususia uchaguzi na sio kusitisha uchaguzi, maana kuna vyama vinaona kuwa chaguzi ziko sawa na kuna watu hawana vyama kabisa. Kwanini Lissu anataka kutunyima haki yetu kwa kuzuia uchaguzi, who is he?
Nitajie mahali vyama zaidi ya 10 vinapofanyia shughuli zao ili nijue hoja ya kuna vyama vinaona uchaguzi uko sawa. Cdm tunaona uchaguzi una walakini mkubwa, na ushahidi wa hilo upo. Cdm wana haki ya kuzuia chaguzi za kihuni, kama ww ni mfaidika wa chaguzi hizo za kihuni hiyo ni kimpango wako.
 
Tatizo liko hapo, mnadhani watu wote ni chadema, na mnadhani watu wote wahawajui na hawaoni kile CCM wanachofanya kusalia madarakani. Narudia tena kukujuza kuwa kila mtu ana threshold (uwezo wake wa kusubiria) yake; CCM bado hawavuka mistari myekundu ya watanzania ya kuvumilia. Yaani kama ni deni tunasema bado ni himilivu; msitake watanzania wooote waone kama nyinyi.

Watanzania wengi wana akili na uwezo wa kufanya benchmarking (kulinganisha na kujilinganisha) na mataifa mengine Afrika na duniani; kuna baadhi ya mambo wanajiona wako juu sana kuliko mataifa mengine; pia wanajua chanzomama (basic cause/route cause) cha umaskini wao sio CCM, bali mfumo wa dunia wa kinyonyaji uliowekwa na mabepari kupia WB, IMF, WTO, na mahusiano mengine ya kinyonyaji. Mfano, cdm wanakwenda mikoa ya kusini kusema bei ya korosho chini ya CCM lakini hawasemi wao chadema watafanya nini ili bei iwe kubwa, watakwenda kuuza wapi korosho ili wakulima wapate bei kubwa ya kiasi gani. Hawasemi watafanya nini kwenye pembejeo za korosho tofauti na wanavyofanya CCM. Wanadhani wananchi hawana akili kabisaaa ila wao tu.

Mchungaji Mtikila ndiye aliyekuwa mpinzani wa kweli kwasababu alikuwa anakwambia tatizo halisi linalomtafuna mwananchi na namna atakavyolitatua kama akishika dola. Chadema muda mwingi wanaongelea katiba, tume huru na muungano, vitu ambavyo havina maana kwa mwananchi wa kawaida. Yaani tuwe na Katiba mpya nzuri kama ya nchi gani? Je, hiyo nchi gani wananchi wake wameendelea kiasi gani?. Yaani Tundu Lissu akienda Ikulu wananchi watapata nini kizuri tofauti na CCM ikiwa Ikulu?. Hayo ndiyo maswali ambayo wananchi wanajiuliza vichwani mwao ambayo wapinzani hawawapi majibu yao.

Wananchi wamezoea chini ya CCM watafanya biashara hata kwenye njia za magari, waenda kwa miguu na mwendokasi bila bughudha, wanavua popote na vyovyote bila shida, wanauza bila kutozwa kodi, bodaboda wako juu ya sheria, wanaweza kujenga vijumba vyao bila maneno mengi ya kikodi na kiufundi popote, nk, yaani "present is known and secure", hivyo ni juu yako wewe kusema nao kwa upole kuwaonyesha gap kati ya ilivyo sasa na itakavyokuwa chini ya cdm/ACT/UDP/NRD, nk.
 
Hata kwenye siasa kunahitajika kufanya tafiti ili kujua njia rahisi na muda sahihi wa kufanya nini. Fanyeti tafiti za kina kwanini watanzania ni wagumu kudai demokrasia ikibidi hata kwa nguvu. Badala ya kudhani tu kuwa ni waoga, wanatishwa au nini na nini.

Rais Samia alikuwa na nia thabiti ya kuleta demokrasia kamili nchini, na alikuwa akigombana hata na wahafidhina ndani ya CCM kuhusu jambo hili la kuifanya Tanzania kama mali ya CCM tu. Lakini baada ya kuruhusu vyama vifanye kazi zao za siasa. Lakini sasa hivi bila shaka wahafidhina wanamsuta kwa dhamira yake ile ya kuifanya nchi kuwa ya kidemorasia. Amefungulia matusi, kejeli na harakati kwa watu ambao wana hasira za kutoka awamu zilizopita; hawana busara wala hekima na staha majukwaani. Wanasahau kwa Katiba yetu inampa Rais nguvu nyingi za kuamua na kutenda.
 
Vyote hivyo tumeshashema ndio maana tunataka box la kura liheshimiwe ili ukweli ufahamike wananchi wanaamini chama gani. Maelezo meengi lakini hutaki kipimo halisi cha wananchi kuelewa kiheshimiwe. Team nzuri itaonekana kwenye mchezo wenye VAR.
 
Ni waoga sio nje ya hapo, labda nifane tafiti kwa hadida za rejea toka kwako ili nipate majibu uyatakayo.
 
Wananchi ni results oriented. Wanchojali wao ni amani, utulivu, hospitali, shule, barabara, mwendokasi, pembejeo, reli, internet (bando), ku-bet hata kule vijijini, uhuru wa biashara bila kujali nani anavileta. Hata wabunge wa upinzani wanawaona wakiwa na magari makubwa (VX, hammar), majumba, mahoteli, mashamba makubwa, nk kama wale wa CCM tu; there is no difference. Wanafahamu hata kije chama gani maisha yao yatagegemea nguvu zao zaidi kuliko mtawala. Ndio maana hata kiongozi wa upinzani akipigwa risasi, kupotea au kufungwa wao wanaendelea na maisha yao.
 
Ni waoga sio nje ya hapo, labda nifane tafiti kwa hadida za rejea toka kwako ili nipate majibu uyatakayo.
Sio waoga kaka. hao wananchi ndio hawahawa walifunga maduka yote Kariakoo, waliogoma kuendesha madaladala, mabasi na malori kupinga hili na lile, hawa ndio wale waliopinga gesi yao kwenda dar es salaam bila wao kunufaika kwanza. Kaka watanzania wana akili ni balaa ila CCM bado haijakanyaka mpira wao wa kupeleka oxygen kwao.
 
Hao waliopinga gas walizuia isitoke? Kuna mkataba wowote wa gas wameuona kwa macho hadi leo?
 
Zimefanyiwa reforms?? Na tume ambayo haijafanyiwa reforms? Ikisimamia sheria na kanuni zinazohitaji reforms?
Acheni mazingaombwe
 
Zimefanyiwa reforms?? Na tume ambayo haijafanyiwa reforms? Ikisimamia sheria na kanuni zinazohitaji reforms?
Acheni mazingaombwe
piiiipoooos!!! twendeni tukamtoe mwenzetu nae akalale kitandani kwake, where is the peoples power?
 
mwenye kujua content ya maadili ya uchaguzi plz ailete hapa tuone kuna ukweli au uongo uongo usio tekelezwa.
Maswali haya ni copy and paste ya miaka yote tangu enzi za Mkapa. Maswali ni hayahaya yaliyowapeleka akina sugu, prof J, lissu, mdee, zito, mnyika, lema, mbowe na wabunge wengine wa upinzani bungeni siku zilizopita. Shida ni kwamba maswali haleyale mbona sasa hayawapeleki bungeni tena, what happened. Nijuavyo mm wananchi wqnatumika tu .
 
Hayo maadili yamefuata sheria kama inavyotaka au yamefuata maneno ya ccm ndio watu wafuate?
Nadhani Kailima ameisaidia chadema kwenye agenda yao ya no reforms no election baada ya kuiondoa kwenye kushiriki uchaguzi kuatia kutosaini maadili. Lakini kwa kelele hizi za akina Nshala inaonekana kama vile cdm walikuwa wanatishia tu kuzuia uchaguzi, yaani walikuwa wanatishia nyau. Lissu alibeep Kailima akampigia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…