CHADEMA kukubali kupokea ruzuku na kupeleka wabunge wengine wa viti maalum?

CHADEMA kukubali kupokea ruzuku na kupeleka wabunge wengine wa viti maalum?

Hayo mengine ni maelezo baada ya habari.

Ila hawa ndio werevu wa ccm.
IMG_20211231_191325.jpg
 
Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, kipo njiani kupigilia msumari maamuzi ya kuwatimua uanachama akina Mdee na wenzake, Kisha kupeleka wabunge wengine wa viti maalumu bungeni.

Pia CHADEMA ipo tayari kupokea ruzuku, ikumbukwe kuwa CHADEMA wanatakiwa kupata ruzuku ya zaidi ya milioni 100 Kwa mwezi na takribani miezi 17 Sasa hawajachukua ruzuku toka uchaguzi mkuu wa 2020, hivyo wanadai zaidi ya Bilioni 1.7 za Kitanzania kutoka hazina

Source: Raia Mwema
Hili likifanyika ni jambo jema, hivi ndivyo nilivyoshauri hapa katika uzi huu.
P
 
Hili likifanyika ni jambo jema, hivi ndivyo nilivyoshauri hapa katika uzi huu.
P
Huko ndio kurejesha kwa jamii kweli kweli
 
Hili likifanyika ni jambo jema, hivi ndivyo nilivyoshauri hapa katika uzi huu.
P
P nimekusifia Bure wewe hurejeshi Kwa maslahi ya taifa unarejesha Kwa maslahi yako na chama chako, uchaguzi Gani ulikuwa huru na wahaki na ukiwa na dosari ndogo ndogo ni chama kipi kati ya chichiemu kilichogaragazwe kwenye chafuzi, Chadema kilifanya vyema kwenye uchaguzi ilhali ccm iligaragazwa, ila Sasa chadema iligaragazwa kwenye uchafuzi ulioratibiwa na Wana ccm Kwa msaada wa policcm na tume ccm🤔.
 
Makamanda uchwara wa ufipa hawana akili.
Akili zipo hadi zinwagika, kiasi Cha kutuoneeni wivu hata wengine mnaamua kuwaficha Kwa kuhofia wingi wa akili zao zitawafuteni kwenye ramani pamoja na nyenzo zote mnazozimiliki🏋️
 
Hapa issue ni survival, mwanzo waligomea matokeo na kusema hawautambui uchaguzi, hawayatambui matokeo na hawamtambui mshindi na wakagoma kuteua wabunge viti maalum.
Sasa wametambua na kukubali matokeo, mbele ya survival, hakuna mkate mgumu mbele ya chai, lazima utalainika tuu!.

P
 
Akili zipo hadi zinwagika, kiasi Cha kutuoneeni wivu hata wengine mnaamua kuwaficha Kwa kuhofia wingi wa akili zao zitawafuteni kwenye ramani pamoja na nyenzo zote mnazozimiliki🏋️
Njaa zimewazidi hadi wamekubali yaishe ili wapate ruzuku.
 
Njaa zimewazidi hadi wamekubali yaishe ili wapate ruzuku.
Mliamuwa kuwanunua COVID 19,kwa kuwapa rushwa Tena kwakuwatisha, kwa msaada/mgongo wa mzee wa bakora, tumempa shinikizo hatimae ameona aibu akabwaga manyanga, na hivi Sasa tunalia na COVID-19, na tartiibu COVID 19 inaelekea kusarenda . Lengo letu tuokoe Kodi ya mlala hoi inayofujwa Kwa kutoa hongo kwa COVID-19. Sasa mnalia mipango yenu ovu imeshindwa na kuparaganyika. Mungu ni mwema kila wakati. Hasta magumu kwake siichochote.
 
Back
Top Bottom