CHADEMA kukwama kwa maridhiano wa kulaumiwa siyo nyie

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kudai haki, demokrasia, mabadiliko nk kwa njia za amani siyo kosa kokote kule duniani.

Zaidi sana Chadema mmekuwa mkidai kuheshimiwa kwa katiba ya nchi iliyopo. Kwenye madai hayo mkakubali hadi kuingia kwenye maridhiano Ili kuiweka nia yenu hadharani.

Kila mwenye macho au kujali amemwona aliye mshari haswa kwenye hili ni nani.

Kufanya mikutano ya kisiasa ni haki yetu ya kikatiba. Kujaribu kuizuia mikutano hii kwa njia yoyote ni ukiukwaji mkubwa wa katiba usiokubalika.

Aliyeshupaza shingo, mwenye kutaka kuisigina katiba anajulikana.

Chadema mmefanya sehemu yenu.

Tunachosubiri sasa ni kusikia deadlines na hatua za kuchukua.

Chonde chonde mwaka mpya na mambo mapya.

Aluta continua!

Soma, Pia: Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini
 
Way back chadema ilikuwa na ushawishi sana sizani kama wataweza kuiludisha chadema Ile....
 
Ukweli mchungu wengi wenye uelewa wanataka mabadiliko. Hakuna asiyejua kuwa katika wote,CDM angalau wamedhamiria.

Hali ni hivyo hivyo hata huko kwa mambuzi ukweli huo unajulikana.

Hayupo wa maana mwenye appetite ya kuhamia kwingine au kuanzisha harakati mpya.

Tutabanana hapa hapa!

Ukweli huu utaiacha CDM hai na tishio kwa siku nyingi bado.
 
Chadema wapambane, na mapambano hayo lazima yabadilike kimbinu kuendana na muda, lakini kususa kusiwe moja ya hizo mbinu.
 
Ipo tofauti baina ya kusitisha na kususia mazungumzo. Mazungumzo yasiyokuwa na faida ni ya nini?

NInakazia:

"Tunachosubiri sasa ni kusikia deadlines na hatua za kuchukua.

Chonde chonde mwaka mpya na mambo mapya.

Aluta continua!"
 
Anayeendelea kuzuia Mikutano ya Hadhara iliyoruhusiwa na KATIBA ni DICTETA.

Tusipindishe maneno, Kweli yetu iwe KWELI, na HAPANA yetu iwe HAPANA.
 
Ipo tofauti baina ya kusiitisha na kususia mazungumzo. Mazungumzo yasiyokuwa na faida ni ya nini?

NInakazia:

"Tunachosubiri sasa ni kusikia deadlines na hatua za kuchukua.

Chonde chonde mwaka mpya na mambo mapya.

Aluta continua!"
Kama Chadema wakichukua hatua ya kusitisha mazungumzo hapo watakuwa wameendelea kuifuata mbinu ya kuwazubaisha inayotumiwa na CCM, unless wayasitishe huku wakiendelea na mipango yao ya mikutano ya hadhara nchi nzima kama walivyopanga.
 
Tumuite Jina analostahili DICTETA, jinsia haibadilishi Hilo.
 
Kama Chadema wakichukua hatua ya kusitisha mazungumzo hapo watakuwa wameendelea kuifuata mbinu ya kuwazubaisha inayotumiwa na CCM, unless wayasitishe huku wakiendelea na mipango yao ya mikutano ya hadhara nchi nzima kama walivyopanga.
Maridhiano yaendelee na mikutano iendelee sababu ni kuwa Imeruhusiwa KIKATIBA, na anayejaribu kuwa juu ya KATIBA ni DICTATOR.
 
Angalia hii:

--------
"Tunachosubiri sasa ni kusikia deadlines na hatua za kuchukua."
----------

Mazungumzo au maridhiano yasiyokuwa na mwisho, maana wala maendeleo ni ya nini? Tuweke tarehe kamili zenye kutaka matokeo kama yale ya "big results now."

Kama utekelezaji ni sifuri lazima msimamo wetu kwao ujulikane. Options mbona ziko nyingi?

-------
Chonde chonde mwaka mpya na mambo mapya.
--------

Leo wana uhalali wa kupata picha na kina Biden wakijinadi kuwa tunaongea tunaowapa sisi. Hatunayo haki ya kukinukisha kama ndiyo lugha pekee wanayoweza kuielewa?

Aluta continua!"
 
Maridhiano yaendelee na mikutano iendelee sababu ni kuwa Imeruhusiwa KIKATIBA, na anayejaribu kuwa juu ya KATIBA ni DICTATOR.

Maridhiano na katiba havihusiani. Katiba si sehemu ya maridhiano.

Maridhiano kwa maana ya kujumuisha mazungumzo yoyote hata kama ya Simba na Yanga, awaye yote anaweza kuendelea nayo.

Ikumbukwe Kuna ndugu zetu mikononi mwao. Wako wapi akina Ben, Azory, Lijenje na wengine? Nani waliotaka kumdhuru Lissu?

Hata hivyo mazungumzo yasiyo tija, mwisho wala faida au yenye kutupotezea muda kama chama ni ya ñini?

Ninawaelewa sana PAC South Africa. Hawakuwa wakicheka na nyani:

"One Settler? One bullet!"
 
Maridhiano yaendelee na mikutano iendelee sababu ni kuwa Imeruhusiwa KIKATIBA, na anayejaribu kuwa juu ya KATIBA ni DICTATOR.
Hii inapendeza, kwasababu wale jamaa wanawaona wengine wajinga kwa kuwaambia wasubiri huku kina Kinana na Chongolo wakiendelea kuzunguka nchi nzima, sasa ni wakati wa Chadema nao kuzunguka kama wakina Chongolo na Shaka.

Haya yafanyike huku maridhiano yakiendelea, Mbowe akakae nao, huku makamnda wengine wanazunguka nchi nzima.
 
Na ndicho Mbowe anasisitiza.

Chama kiendelee na harakati zake kama kawaida.
 
Back
Top Bottom