Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Serikali iliyopo madarakani. Serikali inayoongozwa na aliyetangazwa na Tume huru ya uchaguzi kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.Wewe kweli ni fundi mchundo.
Serikali ipi na iliyochaguliwa na nani unayotaka ihudhurie msiba?
As it should be.Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche, amewasili nyumbani kwa marehemu Mzee Edwin Mtei kuongoza mazishi ya mwanzilishi wa chama hicho.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Samweli Welwel, amesema ratiba ya maandalizi kuelekea maziko ya Mzee Mtei itaanza rasmi leo, ambapo viongozi wakuu wa chama wakiongozwa na Heche watawasili nyumbani kwa marehemu kutoa salamu za pole.
Welwel amesema baada ya salamu hizo, viongozi hao wataelekea katika Hospitali ya Seliani ambako zoezi la kuchukua mwili wa marehemu kutoka mochwari na kuuleta nyumbani kwake Tengeru litafanyika, huku CHADEMA ikiongoza zoezi hilo.
Aidha, Welwel amewaomba wananchi pamoja na wanachama wa CHADEMA kujitokeza kwa wingi hospitalini kushiriki zoezi hilo, akibainisha kuwa kutakuwa na msafara utakaoanzia Hospitali ya Seliani hadi nyumbani kwa marehemu Mzee Mtei.
Kwa upande mwingine, ameeleza kuwa siku ya maziko, Jumamosi Januari 24, 2026, kutakuwa na ratiba maalum ya kumuenzi mwasisi wa CHADEMA, Mzee Edwin Mtei, ambapo muda wa saa moja utatengwa kwa ajili ya matukio mbalimbali ya kumkumbuka kabla ya ratiba nyingine za mazishi kuendelea.
Hivi bado unayo matumaini ya kuambulia chochote toka kwa waovu hawa?Serikali iliyopo madarakani. Serikali inayoongozwa na aliyetangazwa na Tume huru ya uchaguzi kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Amandla...
Ni kweli ufundi wa kumsafisha mtu sina. Ndio maana sijawahi kujaribu kumsafisha mtu yeyote.Hivi bado unayo matumaini ya kuambulia chochote toka kwa waovu hawa?
Ushauri wangu ni:ridhika na ulichopata huko nyuma wakati ukitegemewa kutumika; hapa tulipofikia sasa Samia Suluhu Hassan hana tena na mahitaji kwa watu wa aina yako.
Mahitaji aliyonayo sasa, ambayo ni ya kumsafisha uovu wake, wapo mafundi zaidi kuliko mlivyo nyinyi.
I agreeSijasikia pia mahali ambapo serikali imesema itabeba msiba huu. Kinachoendelea ni watu kutaka Samia azuiwe kushiriki katika mazishi. Kushiriki kwake hakutamaanisha kuwa serikali inaongoza mazishi hayo. Rumor hizo zinasambazwa na watu wenye chuki binafsi na Mbowe.
Amandla...