CHADEMA kuteketezwa

MIMI NADHANI KWA TAARIFA YAKO HII TAYARI UMESHATUMIKA KUKIDHOOFISHA CHADEMA NA UPINZANI WOTE KWA UJUMLA.

mchawi hapa si hao uliowataja ni wewe mwenyewe! Na ni vizuri ukaweka source ili kujilinda wewe mwenyewe.

Zitto alishasema haamii CCM kwa namna yeyote ile, kama si hivyo weka source au vithibitisho mkuu!

Halafu upinzani si uaduni jamani, hata wasisalmiane duh!
 
Na bado mtalipana posho mara kumi kumi kwa kazi moja ikibidi watanzania wakae gizani na hata wafe njaa, Kidumu chama cha Mafisadi...Kibs, unapotea nshakuona!
Hilo la posho sipo sambamba nalo, ni moja ya matatizo madogo, natumai baada ya kipindi hiki cha bunge kwisha lao litakwisha tu! Ila moto upo huko Chadema na CUF, tutakutana kwenye kampeni, huyo gwiji wa upinzani mambo yake sasa yapo hadharani...
 
Hilo la posho sipo sambamba nalo, ni moja ya matatizo madogo, natumai baada ya kipindi hiki cha bunge kwisha lao litakwisha tu! Ila moto upo huko Chadema na CUF, tutakutana kwenye kampeni, huyo gwiji wa upinzani mambo yake sasa yapo hadharani...
kampaeni ya CCM ni haya yafuatayo...mengine hamna kitu...kwa wananchi mmekwisha doda..isipokuwa
a) Tume ndio inawasaidia nyinyi
b) Polisi (kupiga wananchi), wana usalama kununua kadi za kupigia kura
c) Mafisadi (pesa)
Bila hivyo kampeni tu mbona tangu 2000 mngekuwa kwenye kaburi zamani...
 
Umesahau kitu kimoja, wapinzani wote ni failure wa CCM.. Hawana jipya na hawataukuwa na jipya.
 
Umesahau kitu kimoja, wapinzani wote ni failure wa CCM.. Hawana jipya na hawataukuwa na jipya.
Kama ni failure wa CCM let the people judge by free will..hakuna uchaguzi nimeshiriki sijaona fujo
kwanza, Jeshi kubwa na matisho na hata kupigwa haswa!
Pili, tume inashirikiana kuiba kura. tatu wananchi wanahongwa kuuza kadi za kupigia kura..why all this effort kama CCM inajua jamaa ni rejects tuu..lol.
 
Kauli zako ni sawa na ule msemo wa Sungura kama "sizitaki hizi mbichi"!
 
kwani haraka ya nini?? ngoja tusubiri tutayaona tu!!! Kama zitto akiondoka na aondoke tu....kwani akina Masumbuko lamwai, Dk. ringo tenga wako wapi ....si ndo wamesaidia mafisadi kuchukua pesa za EPA?

Ninacho amini mimi ni kwamba time will tell na Tanzania haita baki hivi....lazima itabadirika tu. Mbona Angola wamukuwa ktk vita miaka karibu 20 lakini leo wanajenga uchumi wao??? Ipo siku CCM will be out .....if not dying.
 
Ningeshangaa kama CHADEMA haipigwi vita, kwa sababu kwa sasa chama hicho ndiye adui nambari wani kwa CCM hasa kwa upande wa bara, ukiacha CUF kwa upande wa visiwani. Japo CCM wanadai wanalala usingizi, sio kweli sana, maana ingekuwa hivyo wasingekuwa wanapayukapayuka juu ya vyama hivyo. Kama kiongozi wa chadema na au CUF akaikoromea CCM, viongozi wa CCM wanajibu mapigo kwa kulalama kweli. Lakini NCCR na PONA wakisema kitu utadhani CCM wameenda safari. Hiyo ni dalili tosha kwamba CUF na CHADEMA ni tishio kwa CCM. Ama kusema kweli, kama sio wizi na ufisadi wa uchaguzi, CCM wanaweza kufa kifo cha mende wakati wowote. Sasa Viongozi wa CCM kwa kutumia mgongo wa fedha za wananchi kwa serikali wanafanya kampeni nchi nzima hata kabla ruhusa haijatolewa kwa ajili ya 2010. Raisi akisimama lazima bendera za CCM na nyimbo za sifa kwa CCM huwapo. Ukiuliza wanasema anazo kofia mbili. Sasa kama Raisi anatembelea wananchi wake walio na wasio CCM, kwa nini CCM wanameza mikutano na hata anafungua matawi? Si angehimiza maendeleo tu na CCM wamwite kwa pesa yao?

Leka
 
Uwongo uwongo uwongo. Chadema inazidi kuimalika na wala CCM haiwezi kuiangamiza kwa stori za kizushi kama hii.
Kwanza kina Mwakyembe bado hawajashindwa huko CCM, bado wananyukana wao kwa wao ndani ya chama.
Jana jioni nilikuwa na makada wa CCM (wakongwe na vijana) hapa Dodoma, wao wanakiri kama chama chao hakina future.
Chadema kinazidi kuweka mizizi sehemu tofauti nchini na ni hivi karibuni tu wamefungua tawi mtaani kwangu.
Hao unaowaita usalama wengi tu ndo wanawasaidia CHADEMA.
Na zaidi CHADEMA (kwa sababu kinafyucha) kutengenezewa mizengwe na CCM si jambo jipya ila mwisho wa siku CHADEMA kitaonesha umahili wa kupangua mizange ya chama cha wazee waliokufa kimawazo, kimalengo, kiuzalendo, kimikakati na kifikra.
MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 


maharage ya mbeya yule....Njaa tupu hamna lolote! Ukimaliza kusoma rudi utakuta wapinzani wa ukweli wasio wanafki.
 
SISEM ndio caput dead. Hata CHADEMA inaweza kufa lakini kwa sasa baaaado kabisa. Halafu kwani Zito ndio CHADEMA? tafadhali tatake radhi
 

Kuna watu ndani ya JF wana kipaji kikubwa cha kutunga hadithi!
 
Lini hiyo Kibs?

Jamani mbina huku naniliu tuko strong sana na kila siku yanafunguliwa matawi?

Au naongea na mamluki?

Mmetumwa?

Nanani?

Mnalipwa nini nyie?

Kitamalizwa na kile kilichosajiliwa juzjuzi cha WAKULIMA
 



Hali Halisi umeambiwa sasa unataka ukweli upi? kwani hiyo mipango haiwezekani? Jamani tuwe tayari kutetea Taifa hili tusiwe wanyonge, wababaishaji wa Hoja. Hoja iliyo mbele yetu ni kweli yaweza kutokea sasa unachobisha ninini? Shime wana JF uwe kitu kimoja kupinga Ufisadi sasa kama tusipombinga haki yetu tunaipeleka wapi? Hizi habari ni za ndani zaidi wewe toa oni lako. Zitto kuwa makini uki badili Chama ni kama umebadili kabila.
 
Hii story yako nahisi kuna ukweli ingawa kuna mafisadi wanaikejeli kwani siri yao imefichuka.kuficha mambo siyo solution,mimi napredict machafuko ya vita Tanzania baadaye na experience inaonyesha maendeleo mara nyingi huja baada ya conflicts mfano Rwanda Burundi,Ghana.
 
Kuna watu ndani ya JF wana kipaji kikubwa cha kutunga hadithi!
Zito, inaweza kua hadith yakutunga ila mtungaji ameunganisha matukio mbali mbali na kuibuka na picha halisi ya hali ya mambo ilivyo, Kijana usiogope kivuli chako ndani ya CHADEMA, mitindo yako yamaisha inaibua maswali mengi yakutisha sana dhidi ya mustakabali wako kisiasa.
Maisha yana mengi y kujifunza, kama inavyojionesha kwenye post hiyo juu ni kua Umma wa Wanachadema baadhi umepoteza Imani, unadhani umo mbioni kuwaacha, namna unavyochangia mijadala kwenye umma , kweli inazua mijadala.
Hadithi itaendelea hadi kurasa za mwisho.
 

Kuna msemo unasema ukitaka kumwua Mbwa unampa jina baya! Siogopi kivuli changu ndani ya CHADEMA na ninaamini wenzangu pia hawaogopi kivuli cha Zitto ndani ya chama.

Siwezi kuzuia watu kusema wanchofikiri maana ndio demokrasia. Uadilifu wangu kwa chama changu hauna chembe ya mashaka.

Kwangu mimi na kwetu Kigoma CHADEMA ni zaidi ya chama cha siasa, ni movement na ndio maana wakati mikoa mingine CCM imeshinda 90%+ katika serikali za mitaa, kwetu Kigoma CCM wamepata 59% tu.

Kigoma ukitoka CHADEMA umesaliti vuguvugu hili na kwa kweli ninajipima kwa watu wangu na sio kwa watu ambao siwajibiki kwao. Napenda nieleweke katika hili vizuri na wanachama wa jf.

Wanaofikiri kuwa nitahamia CCM hawanijui vizuri na hawajui utamaduni wetu. Mwulize Kabourou aliehamia CCM kama anaweza hata kutembea Kigoma licha ya kupewa Ubunge wa EAC.

Imani ya wanachadema kwangu haijashuka hata chembe na ndio maana wamenipa heshima ya kusomba vijiji Kigoma katika majimbo yote. Hata hivyo inategemea kwako wanachadema ni kina nani. Kama ni wanachama wa kawaida wanaojua ninavyojitoa kuwatetea umenoa.

Kama ni wapinzani wangu wa kisiasa upo sahihi.

Ndani ya CHADEMA i see the future and it works!
 


Mheshimiwa Zitto hii unaweza kuielezea kuondoa utata wa majungu!
 
nashukuru kama unaweza kuhisi kua kuna namna jina lako limeguswa na jamii hata wale waliondani ya CHADEMA , kuhusu kuaminika kwako kama mwanaharakati kijana, mpenda maendeleo ya kisiasa, msomi na mpiganaji wa aina yake.
mimi naamini kua jitihada zako zimurudisha nyuma sana nguvu na kuaminika kwa CHADEMA, either kwa bahati mbaya au makusudi. kweli sielewi.
Ila huku mitaani jina lako likitajwa linaonekana kama jina la Yuda alie msaliti Yesu .
Uwezo wako wakutunza movement za wenzako ndani ya Chama zinawatisha wananchi wa kawaida kujiunga na movement zenu.
hongera kwa UCHAGUZI HUKO KIGOMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…