CHADEMA kuteketezwa

Hilo la posho.... ni moja ya matatizo madogo, natumai baada ya kipindi hiki cha bunge kwisha lao litakwisha tu..
Makubwa yatakuwa yepi?
Nyie CCM kwa "saundi" hamuwezekani bana!!
 

I thought usalama wa Taifa is far much more than just politics, should we believe kwamba maelezo yako ni ya hiyo taasisi au ni some individuals wenye political motives!!? If it is true, probably you are a frustrated version of them !!!
 
Unatuzuga nini? mbona uko huko siku nyingi? Mchana Chadema usiku sisi m.
Nani uliwahi kusikia anamkana mama yake kwa sababu ni kilema?
Mkuu ni mawazo yako kwa sababu mimi sii kiongozi wala mshabiki wa chama chochote..Na itakuwa vigumu kwako kuelewa kwa sababu huko Chadema hakunipeleka Zitto wala Mbowe isipokuwa kwa sababu chama hicho kinafuata mrengo ninao ukubali. Nimesoma ilani zao, Sera zao na hata malengo yao na kuyakubali.. Na labda nikuffahamishe tu mapenzi yangu kwa Zitto yanatokana na kitu gani... Zitto kwa kuelewa kwangu ndiye aliyependekeza mrengo huo kwa Chadema na nipo naye toka siku hiyo..Na ilimchukua kazi kubwa hata ndugu Kitila kuniweka ktk mstari kwani imani yangu ya mrengo inatangulia vitu vyote..

Hivyo kusikia Zitto anahamia CCM haikunipa shida ila kumpongeza. Tumaini langu linaweza kutokana na kushawishika kwamba Zitto anaweza kuleta mabadiliko ndani ya chama hicho akiwa karibu na wazee kina Salim, Warioba na Malecela..Na simpimi Zitto kwa matakwa na manufaa yangu ila ya wananchi walio wengi..I will always respect anyone decision ikiwa mtu huyo atawakilisha watu wengi zaidi yangu, mkuu mimi natazama mbali sana zaidi ya Chadema na CCM.

Mkuu matatizo ya ndani Chadema kusema kweli yalinivunja nguvu, nimemsoma vizuri Zitto na kufahamu kwamba vita yake sii tu nje ya chama hicho ila anapigwa marungu nje ndani..For that nimemlaumu yeye kwa kuendekeza vita hiyo (upande wake) nikizingatia kwamba wapo wengi sana ndani ya chama hicho wanaomba Zitto aondoke kesho (maelezo ya Omarilyas) na kweli vita hiyo nimeiona hapa JF kwa muda tena watu wa juu ndani ya chama..Hivyo, kwa mtazamo sikushangaa kusikia Zitto anaondoka wala sintaweza kumlaumu kwani kushindwa tumeisha Shindwa..2010 ni matokeo tu kutangazwa ikiwa hali ya kisiasa ndani ya chama ndio hiyo..
Pili, I do careless na litakalotokea hasa baada ya kugundua kwamba azma yangu haiwezi fanikiwa.. Kama unakumbuka hata kabla UFISADI haujapata sura nchini, mimi ndiye mtu wa kwanza hapa JF kutamka kwamba Tanzania bila kukomesha GRAND CORRUPTION hatuwezi kwenda kokote.. this was APRIL 2007 na baada ya hapo ndipo tukaanza kusikia habari za Ujenzi wa BoT twin tower, EPA, Richmond na mengineyo yakipewa nguvu kubwa.

Zitto sii mtume wala hana fimbo ya Mussa, ameshindwa swala la Buzwagi kwa sababu kasukumiwa yeye, Na ufisadi wakauvamia wasiojua hata mwanzo wake.. matokeo yake tumekwama kote.Leo hii maswala hayo yote CCM wamebeba vibwebwe, kesi ya nyani leo ipo kwa ngedele na kwa hali yoyote ile watashinda, kuna haja gani ya kufikiria vinginevyo?...
Yote haya yametokana na upumbavu wa baadhi ya watu wachache sana wanaokusudia kuhakikisha kundi la Dr.Slaa, Zitto, Mwakyembe, Mama Kilango, Sitta, Shelukindo na wengineo hawafanikiwi... na YES! dalili zote zimekwisha jitokeza..

Na mwisho mkuu wangu nilivunjwa nguvu kusikia Chadema wamebadilisha mtazamo wao ktk mrengo....wamesogea na kuwa chama cha mrengo wa kati kushoto, jambo ambalo sina mapenzi wala ushabiki nalo..Na nitakukumbusha tena kwamba nimewahi kusema hivi, ikiwa kesho CCM watakuwa Conservative, mimi Mkandara nitahamia CCM kwa sababu simfuati Kikwete, Mbowe, Zitto, Dr.Slaa wala Maalim Seif..ila imani yangu ya mrengo utakao tuwezesha Tanzania na hasa Watanzania wazawa kuwa na nafasi kubwa ktk maendeleo ya nchi yangu..I'm Conservative first, kutokana na WATU na MAZINGIRA tupo karibu sana na ukweli wa hali halisi ya mbadiliko ya Tanzania na tupo sawa kinamna na UJAMAA wa mwalimu Nyerere.
Ukiweza kunielewa hapo mkuu wangu wala hutapata taabu na hoja zangu..
 
Mkandara,
Sijakuelewa unaposema Conservative. Katika mtazamo wangu hivi leo CCM ni kama Republican wa Marekani, a conservative movement. Wao wako karibu zaidi na matajiri na wanachukia matajiri kutozwa kodi. Mimi kwa siasa za Marekani ni Demokrat. Ndio maana nilimpigia kura Obama. Wademokrat wako karibu zaidi na wafanyikazi na watu wa tabaka la chini. Kwa mtazamo wangu leo CCM ni conservative wa kimagharibi.
 
Zitto akihamia CCM amekwisha ingawaje ana hiyo haki lakini myself nitachangia whatever i can kwa mpinzani wake ili kumchapa chini...i'm more than serious in this maana sio pesa chafu za mafisadi tuu zinaweza fanya kazi hata zetu zina uwezo,lakini naamini hes smart enough kufanya move ya kipuuzi kama hiyo!
 
Jasusi,
Shukran sana kwa kuleta hili swala kwa sababu watu wengi sana huutazama mrengo wa Conservative kwa kuifuatia Marekani au UK au nchi nyengine yoyote za Ulaya..tatizo la wengi ni kutofahamu Principal zake...That's important, na kwa sababu ya mazingira yetu, tofauti kati ya Conservative wa Marekani na sisi ni kubwa sana kiasi kwamba kwetu U conservative unaweza kuingia ktk Ujamaa wa mwalimu.

Ni kweli Conservative hatupendi kodi kubwa kwa Matajiri - tunawabeba kwani wao ndio msingi wa utajiri wa nchi (sio Mafisadi) na hakika pia Conservative hatupendi Uchumi wa nchi kumilikiwa na wageni. Umeona hapo jinsi tulivyogongana?..

Hivyo, ikiwa tutaweza kuwa na matajiri wazawa na kodi nafuu hii sio tu inainua uchumi wetu bali tutawawezesha wananchi wetu kumiliki utajiri wetu badala ya wageni. Kuunda kina Bakhresa 200 ni maendeleo makubwa kwetu kuliko kuwa na Barricks 10...

Tofauti kubwa ya CCM na Conservative wao wamewapa wageni msamaha wa kodi lakini kuwatoza kodi kubwa wananchi jambo ambalo ni kinyume kabisa cha principal zetu... halafu ukitazama kwa undani zaidi tunawachukia Conservative kwa sababu sisi ni wageni nchini mwao lakini kwa Wazungu wenyewe wazawa wa nchi hiyo kina Lou Dobbs na Fox huwezi kuwaambia lolote.

Yes, nakubali kabisa ni mfumo wa ubaguzi kwa namna lakini ukweli siku zote utabakia ukweli...Hakuna nchi tajiri hata moja inayojenga uchumi wake kwa kutumia wageni zaidi ya wageni hao kuwa cheap labour wa kusukuma gurudumu la uchumi huo. Hata hao ma King fahad na waarabu na kadhalika walioweza kuinvest Marekani basi kinachotoka Arabuni kurudi US ni kikubwa zaidi (mafuta). Americans have a huge chunk of share in Arab countries..

Kwa nini unaitazama Republican kutokuwa karibu zaidi na wananchi ni kwa sababu ni hao hao Demokratic wanaolegeza sheria kwa immigrants.. kura zao nyingi zinatokana na immigrants ambao hupenda vya bure na kudandia (welfare)..CCM hawawezi kuwa conservative ikiwa leo Tanzania imejaa wakenya wakichukua kjazi za watanzania, wamejaa mataifa ya kila aina pasipo hata masharti magumu kiasi kwamba unakuta machinga wa Kichina.

Kweli Conservative wanaonekana kutokuwa karibu sana na wananchi kwa sababu ya mgongano huo, lakini laiti Marekani ingekuwa nchi ya wazungu na Conservative ndio wapo madarakani basi ungeona jinsi wanavyowapenda watu wake.

Marekani wakati wa Bush wameingiza wazungu toka nchi za East Europe kuliko wakati wowote ule kwa sababu tu hesabu zao ni kwamba Aliens (kina sisi) tutakuja kuwa majority in the next 20 yrs. Sisemi hiyo ni sifa ila ni kuelewa kwamba kila mzazi anamweka mwanae mbele ya viumbe wote...

Leo hii Tanzania chini ya CCM mtu kama wewe unaitwa MKIMBIZI na huna uraia ila mzungu anayekuja kuoa tanzania ana haki kuliko hata wewe, tena watampa uraia haraka sana pasipo kufuatilia uraia wake nje. Wahindi wangapi nchini wana Uraia wa nchi mbili, lakini chini ya CCM anayeadhibiwa ni wewe Mtanzania unayejulikana umezaliwa wapi, mtoto wa nani lakini maadam uliamua kwenda Ulaya ukaoa mke mzungu, ukachukua uraia basi wewe ni mzungu..

Ni mambo mengi tu mkuu wangu..Ningekuomba sana usome Principal zao, U conservative ni kitu gani kisha pima mawazo hayo ktk kuitazama tanzania na sio marekani au Uingereza..apply same Principal nyumbani zitafanya kazi vipi.
 

Mkandara,

Mimi naona kuwa tafsiri yako inafiti uconservative wa chama cha DP na kiongozi wao Mchungaji Mtikila.
 
Ni kweli lakini tatizo la Mtikila ni kwamba huchanganya mambo mengi isijulikane kama ni Conservative kisiasa au mtu wa dini zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…