CHADEMA kuweni wakomavu, tofauti zenu zisiwe uadui

CHADEMA kuweni wakomavu, tofauti zenu zisiwe uadui

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,203
Reaction score
35,840
Wakuu,

Tunafahamu kumekuwa na minongono kuwa ndani ya CHADEMA kuna tofauti juu ya maridhiano yanayoendelea na CCM. Pamoja na Mh Mama Samia kukiri kuna wahafidhina Chadema na CCM wanaokataa mabadiliko, Pia tumemsikia Tundu Lissu akishangaa wenzake kuchekacheka kwa ahadi za ubunge.

Kuna kasumba ndani ya Chadema ambayo imepelekea think tanks wengi kuondoka ni pale unapokuwa na mawazo tofauti hasa na matakwa ya Mwenyekiti unaonekana ni msaliti. Hizi ni kasumba za kitoto tunategemea kwa ukomavu wenu huo utoto usiwepo tena.

Tumeona CCM wakitofautiana waziwazi hata na Mwenyekiti pamoja na mikiki inayotokea lakini wanakuja kuafikiana na kusahau tofauti zao ikifika kipindi cha kusaka dola. Chadema uadui huwa ni wa kudumu na kazi ya propaganda za uongo huendeshwa hata nyakati ambazo pengine ilifaa kuungana.

Hili la kutofautiana kwenye maridhiano si uadui na msiruhusu likae kiadui. Bila kutofautiana kimawazo mtajenga vipi chama imara? Sioni tatizo hayo makundi mawili kusigana hadi upatikane muafaka utaoridhiwa na pande zote.

Kama alichogusia Lissu ni sehemu ya majadiliano basi kinachoendelea kinatia shaka sana. Mimi binafsi nasimama na wahafidhina wa Chadema.
 
Kinachokosekana ni uwazi.

Haiwezekani Mchungaji Msigwa hajui kinachoendelea kwenye Maridhiano lakini Halima James Mdee anajua.
 
CHADEMA itakuja kuharibu Tanzania yetu kama inavyojulikana Duniani.

Nchi yenye Amani Utulivu na Mshikamano usiopatikana katika Nchi yeyote Afrika na naamini Duniani kote!

Hatuwezi kukubali kuja kuchezewa na Viongozi wenye visasi binafsi na kuingiza ubinafsi huo katika ulingo wa Siasa. Hilo, halikubaliki. Binafsi nakataa vinyongo kuingizwa, na nitayapinga kwa nguvu zote nilizobarikiwa na Muumba.

Mazingira waliyojenga miaka ya nyuma(uadui) yasikubalike...Kuna pande mbili za Shilingi..kwenye mazingira husika, ila Dola haichezewi. Wanajua hivyo.

Vuta nikuvute zao sio Demokrasia, sikubali kuhadaiwa na hadaa ya Maneno yao. Sikubali Ng'o! Wasituingize Watanzania na Tanzania yetu iliyoshikamana, yenye Amani na Utulivu kwenye dhoruba.

....Ili Tanzania ibaki kama kinara na Kiongozi wa Mapambano ya Kumkomboa Mwafrika kutoka makucha ya Mabeberu, tuna budi ya Kuwachagua wale wanojua maana ya Uhuru na Umoja na siyo wale wanaotaka Kupasuana kwa majimbo na ubinafsi na Uhuru bandia.

We are the Frontline State. And should Remain So.

Chagua kwa Uangalifu 2025

Aluta Continua
 
Kuwa na mawazo tofauti na kiongozi sio kosa ndani ya Chadema, na wala halijawahi kuwa kosa, huo ni MTAZAMO wako tu.

Muhimu ni kujua kama hayo mawazo yako unayatolea sehemu sahihi, uhakikishe unafanya hivyo ili kujiepusha kuleta mvuragano kwa wanachama pale ambapo itaonekana mawazo ya mmoja, yanatofautiana na msimamo wa chama.
 
Back
Top Bottom