CHADEMA itakuja kuharibu Tanzania yetu kama inavyojulikana Duniani.
Nchi yenye Amani Utulivu na Mshikamano usiopatikana katika Nchi yeyote Afrika na naamini Duniani kote!
Hatuwezi kukubali kuja kuchezewa na Viongozi wenye visasi binafsi na kuingiza ubinafsi huo katika ulingo wa Siasa. Hilo, halikubaliki. Binafsi nakataa vinyongo kuingizwa, na nitayapinga kwa nguvu zote nilizobarikiwa na Muumba.
Mazingira waliyojenga miaka ya nyuma(uadui) yasikubalike...Kuna pande mbili za Shilingi..kwenye mazingira husika, ila Dola haichezewi. Wanajua hivyo.
Vuta nikuvute zao sio Demokrasia, sikubali kuhadaiwa na hadaa ya Maneno yao. Sikubali Ng'o! Wasituingize Watanzania na Tanzania yetu iliyoshikamana, yenye Amani na Utulivu kwenye dhoruba.
....Ili Tanzania ibaki kama kinara na Kiongozi wa Mapambano ya Kumkomboa Mwafrika kutoka makucha ya Mabeberu, tuna budi ya Kuwachagua wale wanojua maana ya Uhuru na Umoja na siyo wale wanaotaka Kupasuana kwa majimbo na ubinafsi na Uhuru bandia.
We are the Frontline State. And should Remain So.
Chagua kwa Uangalifu 2025
Aluta Continua