Zitto lazima aende ktk kamati ili alitumikie taifa, muhimu kwake ni kuwa makini na muadilifu kwa taifa. Kwa kujitoa itakuwa kama mchezo wa kina zembwela tu!!!
Akiona kuna uzushi hapo ndipo anatakiwa ajitoe na kuweka mambo hadharani!! nafikiri hiyo ndio move inayohitajika! si mwakumbuka hata mzee ndesa aliachia ngazi!!!
Zitto lazima aende ktk kamati ili alitumikie taifa, muhimu kwake ni kuwa makini na muadilifu kwa taifa. Kwa kujitoa itakuwa kama mchezo wa kina zembwela tu!!!
Akiona kuna uzushi hapo ndipo anatakiwa ajitoe na kuweka mambo hadharani!! nafikiri hiyo ndio move inayohitajika! si mwakumbuka hata mzee ndesa aliachia ngazi!!!
Mzee Ndesa alipata faida gani, na uamuzi wake uliisaidia vipi Kamati hiyo?
Mzee Ndesa alipata faida gani, na uamuzi wake uliisaidia vipi Kamati hiyo?
Kumbe kuna Ulaji? Chadema wamesema wanafanya mkutano wao Jmosi.....wale wanachama walioko humu wanaweza wakatupa brief.Kuteuliwa kwa Zito si sawa na kama angeteuliwa Mwafrika wa Kike,Kada Mpinzani,Mchambuzi kwenye Tume ile? mbona imekuwa big deal saaana?Kidumu Chama cha Chadema!
Wanaoneana wivu nini kwa "ulaji" wa Zitto?! kwi kwi kwiiiiii
Hivi kweli watu nyie mnakaa na kuanza kubishana na Kada ? Kada is the guy ambaye yeye ni kushabikia na kungojea kasoro za Upinzani aseme . Hana mwelekeo wala si mkata issue ila huleta vijineno vya kitoto siku zote .Yeye ni nazi na mnazi wa CCM kwisha kazi yeye tanzania na watanzania si kitu kwake . Kwa mara ya kwanza ama pili naona kaleta mada ya ku copy magazetini huku akiwa anajua kwamba CCM wanataka pa kutokea so the way forward ni kujaribu ku create chaos kwa gharama yeyote ile . Hili halitafanikiwa .
Kada na wanazi wenzie wanashangaa kuona CHADEMA wanaitana kujadili mawazo yao tofauti kinyume na walivyozoea ndani ya CCM ambako wale miungu watu wakishatamka kitu ndio imetoka hiyo hakuna kupingana kimawazo. Kuleta tofauti ya mawazo kwao ni kuwa "SIO MWENZETU".
Jambo hili la Zito na kamati ya madini jinsi linavyochukuliwa ndani ya CHADEMA ndio njia sahihi inayotakiwa kwani kila mtu ndani ya kamati kuu atatoa mawazo yake kisha watatoka na msimamo mmoja. Huu ndio ukomavu unaotakiwa na inaonyesha hakuna mwenye miliki binafsi ndani ya hicho chama kuweza kuagiza atakacho kifanyike.
Tunakitakia kheri kikao chao,na kama ilivyo kawaida ya CHADEMA tunajua busara na maslahi ya taifa ndiyo yatakayopewa kipaumbele.
KADA MPINZANI! Acha uvivu wa kufikiri, tazama dunia kwa mapana na marefu, jifunze namna ya kusoma alama za nyakati, Jivunie kuwa mzalendo wa nchi yako na uwe tayari kuitetea na kuipigania, usikubali kupewa kipande cha muhogo ukatoa maamuzi yenye kuangamiza jamii yako!!
Gday!
Mimi nafikiri hakuna haja ya Zitto kujitoa kwani upinzani unaitaji kushirikiana na serikali kuokoa mali za Watanzania wao wakiwa msitari wa mbele.
Sioni tatizo la final report ikisuport mikataba kwani Zitto kama Zitto kama hakubaliani na final report anaweza kuwasilisha ya kwake nafikiri taratibu zinaruhusu kufanya hivyo.
Hii ni nafasi ya pekee kwa Wapinzani kuonyesha jinsi gani wanaweza kutetea Watanzania.
Sidhani kama Mheshimiwa Zitto ana njaa ya posho za vikao, ila ansukumwa na masilahi ya Tanzania.
Kada mpinzani yeye amebobea kwenye CCM anasahau hata watanzania wenzake, kwa kuleta ubishi ambao haujengi nchi yetu.
... and guess what ? i did it by switching sides peke yangu and later on watu wakaanza kuongezeka na sasa mnaona changes mnaanza kunilalamikia, je hii ni haki kweli ?? nilipokuwa napiga kelele siku zote mlikuwa wapi ??
anyway sitaki kuharibu mada, so lets keep the flow of the thread flowing !
Hivi chadema wamerogwa???? Mbona Mnaanza ubishi wa simba na yanga?@^$#$%#.
Naanza kupata wasiwasi kuwa Chadema wanaogopa kuumbuka!! Kwamba wasiwasi wao Sio kuwa kamati haitafanya kazi vizuri, bali ikifanya kazi yake vizuri itapelekea umma wa watanzania kujua ukweli kuwa maswala ya madini si tatizo la kitaifa kama chama hicho kinavyojaribu kuwalisha wananchi. Kina mzee slaa kila wakiangalia ni kuwa wameshakula kingi ya watanzania wengi kwamba madini ni janga la kitaifa ambalo innji imeingizwa na serikali ya CCM, kwa hiyo kwa kujulikana ukweli waTZ watang'amua uzushi wao.
Unajua wale jamaa wanasema nini moyoni kwa ubishi wa Zitto kung'ang'ania kamati HUYU BWANA MDOGO HAJUI MADHIRA YATAKAYOTUPATA CHADEMA KAMA CHAMA CHA SIASA UKWELI KUHUSU MIKATABA YA MADINI UTAKAPOKUWA WAZI KWA WA-TZ, NDIO TATIZO LA KUSHIRIKISHA WATOTO KTK SIASA!!!
Nawashauri watu wanaoweka mbele maslahi ya vyama vyao vya siasa, kuepukana na utumwa huo na badala yake walitumikie taifa.
ZITTO endelea dogo wangu, kesho unaweza usiwe chadema lakini siku zote utakuwa Mtanzania!!! MASLAHI YA TAIFA KWANZA!!!
Hongera kwa kazi ngumu na ya kuonesha mfano!! sikujua ulifanya mambo haya peke yako... it must be very lonely and hard sometimes.. but keep on fighting!!
Mwenzetu tunakuvumilia mawazo yako lakini haya unayoandika yanaonyesha ushamba wako. Lazima ujue kuwa kutofautiana mawazo ni sehemu nyeti na ya msingi katika jamii ya kidemokrasia. Wewe unawaza kutokana na athari za uzoefu wa uozo wa CCM waliolishwa wananchi wengi.
Mbowe kurudi kufanya kazi yake ni jukumu lake, na huo ndiyo unaitwa uongozi. Ulitaka JK ndiye aje kuongoza vikao vya kamati kuu ya Chadema? Usisahau pia kwamba JK alipomteua Zitto alikuwa na sababu zake za kisiasa, ndiyo maana wapo wanaosema Zitto ameingizwa mkenge ili aumbuke...Tazama muundo wa kamati yenyewe...CCM watupu (na Cheyo ni mmoja wao), isipokuwa Zitto. Haya ndiyo maslahi ya taifa?
Wako wapi wataalamu na wanasheria wa madini walio independent? Yako wapi mashirika yasiyo ya kiserikali? Wako wapi wawakilishi wa madhehebu ya dini? Mbona kamati nzima na CCM tu? Kwa nini wananchi washindwe kuona kwamba Zitto kawekwa ili kusindikiza na kupiga mhuri maamuzi ambayo huko mbele ya safari akiyapinga yatatumika kummaliza?
Hivi kuzingatia maslahi ya taifa ni kufanya kazi katika kamati yenye muundo wa kiutata eti kwa vile imeundwa na rais?
La msingi, tujpe muda tuone matokeo ya kikao cha kamati kuu ya chadema. Hii inaonyesha chama kinaendeshwa kwa vikao sio matamko ya barabarani...[/QUOTE]
great ! ni vizuri kwamba umeweza kuona yooote muhimu uliyoandika !