Hivi chadema wamerogwa???? Mbona Mnaanza ubishi wa simba na yanga?@^$#$%#.
Naanza kupata wasiwasi kuwa Chadema wanaogopa kuumbuka!! Kwamba wasiwasi wao Sio kuwa kamati haitafanya kazi vizuri, bali ikifanya kazi yake vizuri itapelekea umma wa watanzania kujua ukweli kuwa maswala ya madini si tatizo la kitaifa kama chama hicho kinavyojaribu kuwalisha wananchi. Kina mzee slaa kila wakiangalia ni kuwa wameshakula kingi ya watanzania wengi kwamba madini ni janga la kitaifa ambalo innji imeingizwa na serikali ya CCM, kwa hiyo kwa kujulikana ukweli waTZ watang'amua uzushi wao.
Unajua wale jamaa wanasema nini moyoni kwa ubishi wa Zitto kung'ang'ania kamati HUYU BWANA MDOGO HAJUI MADHIRA YATAKAYOTUPATA CHADEMA KAMA CHAMA CHA SIASA UKWELI KUHUSU MIKATABA YA MADINI UTAKAPOKUWA WAZI KWA WA-TZ, NDIO TATIZO LA KUSHIRIKISHA WATOTO KTK SIASA!!!
Nawashauri watu wanaoweka mbele maslahi ya vyama vyao vya siasa, kuepukana na utumwa huo na badala yake walitumikie taifa.
ZITTO endelea dogo wangu, kesho unaweza usiwe chadema lakini siku zote utakuwa Mtanzania!!! MASLAHI YA TAIFA KWANZA!!!