CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
Zitto Kabwe adai wanaopinga uteuzi wake wanatumiwa
Na Mwandishi Wetu

ao zaidi kuliko Watanzania.


�Nadhani baadhi yetu tunatumiwa na maadui zetu bila kujua, tunatumiwa na makampuni ya uchimbaji madini bila kujua, wao hawataki mikataba yao ichambuliwe kwani inawanufaisha wao zaidi kuliko sisi,� alisema Zitto.

labda, but i hope not..





Hapa kuna makosa, Urais hauna extension na nguvu za Rais haziwi extended to proxies... na ni kwa sababu hiyo siyo kila mtu anayeteuliwa na Rais ananguvu za Uraisi. Kamati ya Rais haina nguvu za Rais isipokuwa nguvu zile tu ambazo Rais anazipa, so far hajawapa nguvu yoyote ile. Hawana nguvu zaidi ya kuwa Kamati ya Ushauri na kukusanya maoni, period.
 

Angepunguza kuongea na hawa jamaa wa habari ingemsaidia sana. Halafu hii kasumba ya kufikiria mtu hawezi kuongea mawazo yake hadi atumwe sijui inatoka wapi katika ile nchi yetu? Sasa wale wanaounga mkono wametumwa na nani? We need to change our attitudes, tuheshimu mawazo ya watu bila kuwapachika majina!
 

No problem; ahsante sana kwa kunikumbusha, maana siku hiyo natoa hiyo speech hiyo ilikuwa kazi ngumu sana pale Nkrumah. Wanafunzi walikuwa wamefuraha usoni sio mchezo, ilibidi nitulize mzuka maana sikuona haja ya kuandamana siku ya Ijumaa saa 10 wakati nilikuwa na uhakika hela inapatikana benki jumatatu yake. Umenikumbusha mbali sana, one of those challenges..
Thanks again.

Hii debate haina neno kabisa, debating ni sehemu ya utamaduni wa CHADEMA. We are always happy to engage in constructive debates.

Naona kada kaweka ingine, anainjoi sana vitu kama hivi!
 

Asante pia mkuu,

NO, Kada anashangaa demokrasia ndani ya CHADEMA namna watu walivyohuru kutofautiana na viongozi wao tofauti na huko ccm ambako kila kitu kinaamuliwa na watu wachache tu na wengine wote wanafuata.
 
CHADEMA kama chama kina haki ya kujadili jambo lolote la kisiasa linalohusu bongo, same applies to CCM naona hakuna jipya hapa ni spinning tu. Acha wakutane then tutasikia wanayoyajadili kama yataleta sokomoko kwenye maslahi ya nchi.
 
Nafikiri tatizo kubwa kwenye chama chetu huwa tunaona ajabu wanachama kuwa na mawazo tofauti na wakasema hadharani kwani tumezoea kulazimishana kuzungumza "vikaoni" ndio maana watu kama kina Butiku wanapozungumza hadharani inakuwa habari kubwa kweli.. Hatujazoea kuona mgongano wa mawazo kwenye chama chetu..
 

ha ha ha ha aha hha,

Mwanakijiji wewe umenyimwa kadi ccm bado unakiita chama chako. Itabidi ubadili jina ujiite jina la "mjini" maana hilo la mwanakijiji linawatisha wazee mtaa wa Lumumba
 
kumbe siri imekufikia na wewe.. mwenyewe najibaraguza nipewe Kadi lakini ati "kuna mchujo" na "tabia yako ya kukosoa viongozi hadharani haifai kwa mwanachama wetu"... ati wanataka nipange foleni ya majaribio!! LOL
 
Kamati ya Rais haina nguvu za Rais isipokuwa nguvu zile tu ambazo Rais anazipa, so far hajawapa nguvu yoyote ile. Hawana nguvu zaidi ya kuwa Kamati ya Ushauri na kukusanya maoni, period.

Maneno mazito hayo mkuu, na ndio authority as far as the powers za hiyo kamati.
 

Hayo mazoea ya kulazimisha/ kulazimishwa yametokea wapi, chanzo chake ni nini, nani aliyaanzisha? Maana kila kitu kina mwanzo...
 
Wanabodi,
Mtanisamehe maanake nimekuwa mzito sana kuelewa kinachoendelea hapa. Kwa maana hiyo nitawarudisha nyuma kidogo na kuaomba kuelemishwa ktk hili. - Hivi hii kamati imeteuliwa kwa madhumuni gani haswa?

Nilivyofahamu mimi toka mwanzo ilikuwa kamati ya kupitia upya sheria za mikataba yetu ya madini ili tuweze kuinufaika zaidi lakini kila naposoma hoja na maelezo ya baadhi viongozi inaonyesha kuwa kamati hii itafanya UCHUNGUZI wa mikataba iliyopita ktk kutafuta kitu gani sielewi!.. madai mengi yameoinyesha wazi kuwa kushiriki kwa Zitto ni ktk kuwatafuta wabaya wetu jambo ambalo kidogo linanichanganya kwani nakumbuka kuwa Zitto mwenyewe aliweka msisitizo wake kuwakilisha sera ya chama chake Chadema kuwa atahakikisha kuwa Tanzania inapata asilimia 30 ya hisa zote za madini..

Navyofahamu mimi nia yake ni kuhakikisha kuwa sera hii ya Chadema inakuwa sheria ya nchi na itatumika kama sheria ya taifa kikatiba na hata kama CUF wakichukua Uongozi wa nchi bado mikataba itakuwa na sheria hiyo hiyo..

Sasa naona kuna maswala ya Buzwagi humu na sijui uchunguzi na hao mafisadi hivi kamati hii imewekwa kuchunguza wahusika/maswala ya mikataba iliyopita ama kuitazama upya sheria ya madini na kuwasilisha mapendekezo mapya. Nafikiri Kushirtiki kwa Zitto kunaweza kuwa na sura tofauti kama tutaweza tenganisha kwanza mambo haya mawili... maanake nimeshindwa kabisa kuchangia mada hii kwa sababu sielewi kinachoendelea.
 
Kama alivyosema mzee wa Kiraracha kuhusu kamati hii,na pia Mkandara alipouliza madhumuni haswa ya kamati hii.Hatusemi kwamba CHADEMA wamzuie Zitto kuendelea kuwapo kwenye kamati hiyo bali tunaunga mkono hatua yao ya kujadili madhumuni hasa... sio tu ya "kamati hiyo" hiyo bali pia ya" uteuzi uo"Ili aliyosema mzee wa kiraracha na wapenda demokrasia wote yasitokee(ikiwemo mgawanyiko)ni muhimu kufanya kikao hicho na kufikia makubaliano ambayo yatazidi kuimarisha demokrasia.Mh Rais alitakiwa awashirikishe wapinzani tangu mara ya kwanza alipoingia madarakani.Nilibahatika kuzungumza na baadhi ya wadau muhimu wa siasa nchini na niliwaeleza msimamo wangu kuwa Kikwete ili kumalizia ile hali yake ya kukubalika na wananchi wengi pamoja na kuonyesha nia yake ya kushirikiana na wadau wengine wa siasa bila ya kujali itikadi zao,bado alitakiwa afanye kwa vitendo;na nilishangazwa sana kwanini hakufanya hivyo.Kama wadau hao nilioweza kuzungumza nao wana access na makala hii hapa jf then wanaweza kuona kwamba nilichokuwa nikifikiri kilitakiwa kifanyike sasa kinaanza kufanyika.Tatizo kubwa ambalo sisi wanadamu ambalo tunalo ni kuwa tuna kasumba ya udadisi.Sijui kama ni tatizo ama..Ila sikutaka kukurupuka na kufurahia uamuzi wa uteuzi wa Mh Zitto kwenye kamati ya Rais,sababu kubwa ni "TIMING"Tumeshakutana kwenye makala mbalimbali siku si nyingi zilizopita ambapo pia nilihusisha timing ya kashfa binafsi zilizokuwa zikiibuliwa dhidhi ya viongozi wa upinzani wakati ambapo kulikuwa na mada nzito ya
'UFISADI"Kama unafuatilia kwa makini,Mrema ameweka wazi kabisa kwamba hiyo mikataba ni ya muda mrefu na haiwezi kufutwa,naelewa Zitto anajua hilo..nadhani pia kuna mambo mengi zaidi ambayo anaya consider au ameya consider kabla hajaamua kubaki kamatini.Usalama wake ni jambo moja ambalo hatutaki kulielewa.Hii issue ni nzito!Kikwete ameamua kumonyesha ajionee mwenyewe.Wadau wanaposema kuwa wanataka kuelewa mamlaka ya kamati na nguvu za utendaji wake kwa ujumla wana haki ya kuwa na kilio hicho!kamati zilishaundwa kibwena!Tunataka tujue utofauti wa hii ya sasa!hicho kikao kijadili hilo pia!Je mikataba ambayo imeshasainiwa(ambayo inasemekana ni ya muda mrefu)itarekebishwa?NINI HASA KIINI NA MDHUMUNI YA KAMATI HII?Hilo lazima lijadiliwe na liwekwe wazi otherwise hatari ya migawanyiko inaweza kunyemelea!Dondoo ziandaliwe ambazo zitajibu hoja za pande zote mbili,yenye kukubali uteuzi na yenye kupinga.Nafikiri KULITAKIWA KUWE NA KIKAO CHA UTANGULIZI kabla ya hicho cha jumamosi,hii ni kama bado kuna nia ya kuendelea kukiimarisha chama!Watu waeleweshane kuliko kufanya maamuzi na kutegemea kuwa huo upepo wa haya mambo utapita!Lazima wakubali kuwa Kikwete na CCM wamecheza Dume kama ni karata,wanachotakiwa ni kukaa pamoja na wao wajue ni karata gani ya kucheza ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye duru ijayo,nasema duru ijayo kwasababu duru hii Kikwete kashinda,duru ijayo sasa itategemeana na perfomance ta Zitto humo kamatini,kwasababu Zitto lazima aelewe kuwa tutajua tu kinachoendelea muda si mrefu!Kikwete hivi sasa ametulia tulii na ngoma ndo' inachezwa uko upinzani!Zitto pia ajue kuwa nafasi yake ndani ya kamati ina matter,nafasi yake inamatter kwani ndiyo itakayo determine matokeo ya performance yake.Zitto awe exteremelly carefully kuhusiana na usalama wake!kama kweli hatua yake ya kwenda kamatini ni ya maslahi ya taifa then awe makini na uslama wake!Amuulize mzee wa Kiraracha"USALAMA WA TAIFA"Sasa kama hiyo mikataba ya muda mrefu haitabadilishwa then Zitto atathubutu kukomaa kichwa kweli.Naposema usala wake sina maana kwamba serikali ndio itamdhuru,ila lazima aelewe kwamba there is too many interests kwenye hii issue,na yeye alichukua upande wa wazawa,walalahoi,inahitaji "balls"kubaki upande huo.Bado ana nafasi ya kutuonyesha kuwa bado yuko upande huo!NAWATAKIA KILA LA KHERI ZITTO,CHADEMA,NA WAPENDA MAENDELEO WOTE!
 
Asante pia mkuu,

NO, Kada anashangaa demokrasia ndani ya CHADEMA namna watu walivyohuru kutofautiana na viongozi wao tofauti na huko ccm ambako kila kitu kinaamuliwa na watu wachache tu na wengine wote wanafuata.

nashangaa eeh ? kumbe unajua hisia zangu just like wangu wa ubani !wewe upo kwenye hiyo kamati ya ccm ambako unasema vitu vinaamuliwa na hao uliowataja na unashoboka tu ?
 

NARUDIA TENA JAMANI NILIYOYASEMA HAPO JUU!TUNASUPPORT KWA NGUVU ZOTE ZITTO KUSHIRIKI KWENYE HIYO KAMATI,LAKINI KIKAO CHA JUMAMOSI NI VERY IMPORTANT,NYOTA NJEMA UONEKANA ASUBUHI..MATOKEO YA KIKAO YANASUBIRIWA KWA HAMU NA TUNAWAOMBEA MUNGU KIWE CONSTRUCTIVE!
 
jmushi1,
Ndugu yangu bado hujanipa mwanga kabisa kuhusu swali langu na unaposema unaunga mkono Zitto kujiunga na kamati hiyo nachukulia kuwa unafahamu kazi ya kamati hiyo teule. Je, ni kitu gani hasa watakacho kifanya hadi wewe umeafikiana uchaguzi huo.
1. Kupitia Upya sheria za uwekeshaji.. au
2. Kutazama Ufisadi ulokwisha tendeka ndani ya mikataba ya madini.
Kipi ni kipi?...
Jamani tuelemishane hapa nashindwa kuelewa kuelewa kinachoendelea hapa maanake bado hoja zote mbili zinatumika.
 
"SHALOM MAKES SENSE"
HUYU BWANA AMEANDIKA MANENO MACHACHE AMBAYO NAFIKRI UKIYACHABUA YANAWEZA KUJAA KURASA KIBAO!HONGERA KWA SUMMARIZATION YENYE KUMAKE SENSE NA KUBEBA UJUMBE MZITO!
 
Ndio hapo sasa inabidi tumuulize Zitto atueleze kama anajua anachokwenda kufanya humo kamatini,ndio maana nikasema ni muhimu watumie kikao hicho kuulizana maswali muhimu kama hayo.Binafsi nilisema sipingi uamuzi wake wa kuamua kufanya kazi na kamati hiyo kwasababu naamini amechukua uamuzi huo baada ya kutafakari vya kutosha"hopefully"Ila awe makini asije kujiunga na viini macho kwani ndo mwanzo wa kuporomoka kisiasa!Kama nilivosema before atakachokwenda kufanya huko ndicho tutakachokitumia kuujudge uamuzi wake kiunagaubaga,kwamba je nia yake ya kujiunga na kamati hiyo ilikuwa nzuri,ninaposema "nia nzuri"nina maanisha kuwepo upande wa wananchi na maslahi ya taifa.Kama anasisitiza kwenda huko tumshauri lakini bado tumwache aende na tumpe ushirikiano wa kutosha huku tukimfuatilia kwa karibu utendaji wake umo kamatini kama bado unaendana na utendaji wa Zitto yule tunayemfahamu,mwenye kutetea maslahi ya taifa na wananchi wote kwa ujumla!kama Zitto ame consider mambo yote hayo kabla ya kuchukua uamuzi wake huo then basi ni wazi kwamba anajua anachikwenda kukifanya!? hivyo ni wazi anatakiwa awe very very carefull na kile atakachokwenda kukifanya uko!Na ndo maana nasema ni muhimu majadiliano yafanyike ili kuweza kujua kazi halisi na madhumuni halisi ya kamati hiyo.Kama ulivyosema hapo juu,suala la kutazama ufisadi uliopita sidhani kama hilo watalifuatilia zaidi!Zitto atawaeleza wenzake jumamosi!
 
MWANZO
CHAMA</SPAN>
SERA
KATIBA
TUUNGE MKONO
UCHAGUZI
TUWASILIANE


Hoja Binafsi ya kuunda kamati teule ya Bunge kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini Karamagi ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais

Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB)​

MHESHIMIWA Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa na Bunge lako tukufu, nilisimama mahala pangu na kutoa taarifa ya kukusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge. Nilisema kama ifuatavyo (kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za mijadala ya Bunge), ninanukuu ‘…naomba kutoa taarifa rasmi… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba ya madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Disemba, 2005.’ Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, nimeshawasilisha hoja yangu hii kwa maandishi kwa Katibu wa Bunge na sasa nawasilisha rasmi katika kikao hiki cha Bunge kwa uamuzi. Nimezingatia kanuni 104 (2) katika kuwasilisha hoja yangu.
Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu niliyowasilisha bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini siku ya tarehe 16/7/2007, nilihitaji maelezo kutoka serikalini katika masuala makuu mawili yafuatayo:
  1. Kuondolewa kwa kipengele katika sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako tukufu.
  2. Kusainiwa kwa mkataba mpya wa madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London, Uingereza, na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja zangu Waziri wa Nishati na Madini alijenga hoja zake kama ifuatavyo: a. Kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema, ninanukuu: “…kwa hiyo pamoja na kwamba ninamheshimu sana Mheshimiwa Kabwe Zitto na sote tunamheshimu ni msomaji mzuri, lakini wakati mwingine lazima kuangalia vitu gani unasoma. Ni kwamba kipengele hiki cha sheria kililetwa hapa bungeni mwaka 2001 kwenye bajeti kikabadilishwa…” Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, katika kuandaa hoja yangu hii, ilinibidi kupitia upya kumbukumbu za majadiliano ya Bunge ili kujiridhisha na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, maelezo ambayo mimi nililitaarifu Bunge lako tukufu tarehe 16/7/2007 kuwa sio sahihi.
Mheshimiwa Spika, Kumbukumbu hizo zinaonesha kwamba, sheria ya fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No.14 ya 2001) ilifanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya sheria ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha kifungu cha 87 kiliongezwa. Kifungu kidogo hicho kinasema, ninanukuu:
‘(3) The provisions of subsections (1) and (2) shall not apply to any person who, immediately before the first day of July, 2001 was not the holder of a mineral right granted under this Act.’
Mheshimiwa Spika, kifungu cha 87 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 (No.5/1998) kinazungumzia mrahaba wa madini (Remission and deferment of royalties). Hivyo, kama sheria ya fedha ya mwaka 2001 haikubadili kipenge hiki, Mheshimiwa Waziri ametoa wapi jibu aliloliambia Bunge?
Mheshimiwa Spika, suala hili linahusu haki, kinga na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa sheria namba 3 ya 1988.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe 13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Basili Mramba.
“Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures:
(v) I propose to reinstate the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998.” Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002, nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya madini haitajwi.
Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe?
Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya waziri ni ya kweli. Je, kwa nini makampuni ya madini ambayo yameingia mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato?
Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini, unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati Teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya serikali na ufisadi.
b. Kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi (Mradi) wa Buzwagi.
Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja yangu kuhusiana na suala la mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi, Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya migodi, mgodi wa Buzwagi ni marginal mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya sasa ya bei ya dhahabu, uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani.’ Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, mapitio ya mikataba ya madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa, ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya na makampuni yote ya madini yaliyopo nchini na yatakayokuja kuwekeza.
Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya, ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je, waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu?
Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini aliliambia Bunge lako tukufu kuwa Buzwagi ni marginal mine. Vile vile waziri anasema kuwa Kampuni ya Barrick inamiliki migodi mitatu tu kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals Limited Tulawaka. Kwa maelezo haya ya Waziri Karamagi, Buzwagi sio mgodi.
Mheshimiwa Spika, hoja hii ya kuwa Buzwagi sio mgodi inashabihiana kabisa na hoja ya Kampuni ya Barrick kwamba Buzwagi ni Project. Taarifa ya kampuni hii ya Barrick Gold Corporation-Global operations-Africa- Buzwagi, inaonesha kuwa Buzwagi ni mradi. Taarifa hii ninaiambatanisha katika hoja hii.
Mheshimiwa Spika, taarifa ya Barrick, Annual Review 2006 inasema ifuatavyo katika ukurasa wa 23, ninanukuu. ‘A major milestone was reached in February 2007 when we signed a mineral Development Agreement (MDA) with the Tanzanian government. In 2007, we expect to complete a detailed construction design and receive EIA approval.’
Mheshimiwa Spika, suala ambalo vile vile linanisukuma kuomba Bunge lako tukufu kuunda Kamati Teule ni kwamba, iwapo Buzwagi sio mgodi bali ni mradi, ni kwa nini tumesaini Mineral Development Agreement (MDA) mpya? Kwa kuwa Pangea Minerals Tulawaka ndio inaonekana kumiliki mradi huu, je, serikali imefanya marekebisho tu ya MDA na Kampuni ya Barrick? Naomba Kamati Teule ichunguze ni nini kilichosainiwa, marekebisho ya mkataba wa Tulawaka au MDA mpya ya Buzwagi?
Mheshimiwa Spika, Buzwagi inashika nafasi ya pili kwa uwekezaji wa Barrick katika migodi hapa nchini. Wakati kampuni hii inawekeza dola za Kimarekani 400 milioni katika Buzwagi, imewekeza dola za Kimarekani 600 katika Bulyanhulu. Je, ni kwa vipi Buzwagi iwe marginal mine wakati uwekezaji wake unashinda uwekezaji wa Tulawaka na North Mara?
Mheshimiwa Spika, chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 (Na.5/98), pamoja na mambo mengine kinataka leseni yoyote isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa na kuruhusu mgodi kuendelea na kazi.
Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini ameweka saini mkataba wa Buzwagi juma la mwisho la mwezi Februari 2007, Baraza la Mazingira nchini limetoa kibali (Environmental Impact Assessment- EIA approval) tarehe 11 mwezi Mei 2007. Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Nazir Karamagi alisaini MDA ya Buzwagi na Kampuni ya Barrick kabla Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) halijatoa ruhusa?
Mheshimiwa Spika, sheria ya madini, niliyoitaja hapo awali, imeunda Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining advisory Committee). Kabla ya waziri kusaini mkataba wowote ni lazima apate ushauri kutoka kamati hii. Kwa taratibu za kiserikali, kama kamati ikimshauri waziri na waziri akakataa ushauri huo, inampasa waziri atoe sababu ni kwa nini anakataa ushauri. Je, waziri alifuata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini kuhusiana na wakati mwafaka wa kusaini mkataba huu?
Mheshimiwa Spika, inawezekana kabisa MDA ya Buzwagi kusainiwa Uingereza sio tatizo. Kwa mfano, mwaka 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mikataba kadhaa. Ni mingapi kati ya mikataba hii imesainiwa nje ya nchi? Nini madhara ya kisheria kwa mkataba kusaniwa Uingereza? Je, mkataba umeandikwa “signed in London...” au “signed in Dar es Salaam...? Kamati Teule ya Bunge ndio chombo pekee kitakachoweza kutoa majibu ya maswali haya.
Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Ninaamini wabunge wataamua kwa maslahi ya taifa letu. Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi yatatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.
…………………………….
KABWE ZUBERI ZITTO (MB)
 
MH ZITTO,SALAAM,NINA MASWALI KADHAA..
JE KAMATI ITACHUNGUZA KWA NINI WAZIRI HAKUFUATA USHAURI WA MINING ADVISORY COMMITTEE?JE KAMATI ITACHUNGUZA KWANINI WAZIRI ALISAINI HIYO MIKATABA LICHA YA KUSHAURIWA ASIFANYE HIVYO KUTOKANA NA UDAHIFU NA UBOVU WA SHERIA ZAKE?JE HIYO MIKATABA AMBAYO IMESHASINIWA HUKO LONDON AND SO ON ITAPITIWA UPYA AU TUSAHAU?JE TUME HIYO INACHUNGUZA MAZINGIRA YA UTIWAJI SAINI AMA NI YA MAPENDEKEZO YA MABADILKO YA SHERIA ZA MADINI?TAFADHALI TUWE WAZI NA KAZI HALISI YA HIYO KAMATI AMBAYO UNAKWENDA KUFANIA KAZI MH ZITTO!
 
jmushi1:
Shukrani kwa kutuwekea hapa hiyo hoja ya Mhe. Zitto kuhusu uundwaji wa kamati teule ya bunge, ambayo hadi sasa hatuelezwi ni kwa nini ilishindikana kuundwa.

Na je, hii kamati mpya iliyoundwa na Kikwete ndio sasa itakayochunguza hizo hoja alizoziibua Zitto Bungeni?

Mkandara, bila kupata jibu la maswali yako hapo juu sidhani kamwe kuwa tutakuwa na ufahamu wa kazi ya hii kamati mpya iliyoundwa na Kikwete. Labda wajumbe wanazifahamu bayana hadidu za rejea za kamati hiyo; na ndio sababu Zitto naye hana wasiwasi na utendaji wa kazi wa kamati hiyo.

Kutokana na hoja aliyoikwakilisha Bungeni kama inavyosomeka hapo juu, Mbunge Kabwe ni raslimali, ni tunu ya taifa letu. Tumwombee Mungu azidi kumpa busara na hekima la kuitumikia nchi yetu. Ninashawishika kusema kwamba hakuna wabunge zaidi ya 10 (tokea tupate uhuru) walioweza kujenga hoja kwa kulifanyia kazi na utafiti jambo kama alivyoonyesha hapa. Matumaini yangu ni kwamba huu utakuwa ni mfano wa kuigwa na wabunge wengineo.

Kabwe, ninakuheshimu kwa michango yako hii.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…