CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

CHADEMA kwawaka Moto! Mbowe arudi Dar!

Status
Not open for further replies.
Kalamu naona watu wanaelewa sasa kwanini kuna mtu kauziwa mbuzi kwenye gunia...

Mkjj:
Hapa kuna uwezekano wa mambo mawili. Mojawapo linaweza kuwa hilo la kuuziwa mbuzi kwenye gunia, na mnunuzi akakataa kata kata kununua, na ndio ukawa mwanzo, au mwendelezo wa mambo mengine makubwa kufahamika; ikiwa ni pamoja na ufisadi wa huyo muuzaji mwenyewe.
La pili, linawezekana likawa ni nia ya dhati ya kutaka kutafuta ufumbuzi wa kweli wa matatizo haya ya raslimali zetu za nchi kutupwa tu hivi hivi na wananchi wakibaki kuwa maskini.

Kutokana na msimamo aliouonyesha hadi wakati huu, nina imani kuwa Zitto anayaelewa vizuri yote haya. Tukubali kumpa nafasi. Wahenga husema hakuna asiyekuwa na bei, ngojea tuone kama bei hii itamtosha kumnunua Mheshimiwa (kama kweli bei ipo). Kama ananunulika mapema hivi tutakuwa pia tumetua mzigo ambao ungetuletea matatizo huko mbele ya safari, kama huu mwingine tunaoelekea tulijitwisha bila ya kujiuliza maswali mengi wakati tungali nayo nafasi hiyo.
 
Kalamu hivi unaamini kuwa Kamati ya Rais ina nguvu za Kirais... kwamba kwa vile Rais anaweza kuamuru hivi basi na Kamati aliyoiteua by extension ina uwezo wa kutoa executive orders?
 
Ninaamini hii ni njia ya kujikosha. Hata kama hiyo kamati itatoa ripoti, huenda hiyo ripoti hata siku moja haitauona mwanga wa jua hata siku moja. Lakini, kama Kabwe bei itakuwa haiko sawa... pengine siku moja tutaambulia vi-pieces vya hapa na pale ya ripoti hiyo.
 
Ninaamini hii ni njia ya kujikosha. Hata kama hiyo kamati itatoa ripoti, huenda hiyo ripoti hata siku moja haitauona mwanga wa jua hata siku moja. Lakini, kama Kabwe bei itakuwa haiko sawa... pengine siku moja tutaambulia vi-pieces vya hapa na pale ya ripoti hiyo.

Ni dalili za udhaifu pale unapoambiwa 1 + 1 = 2 halafu ukajaribu kupinga kwa kigezo cha kuwa huru kutoa mawazo yako. Kumbuka mawazo yanaweza kuwa pia hayana maana isipokuwa utaheshimiwa kwa vile tu umekuwa huru kutoa hayo mawazo.

Ni ya Rais imewekwa wazi, pamoja na mambo mengine alisema atawashirikisha wanasiasa kutoka katika vyama vingine kupitia mikataba hii ya madini na hili ni jambo lenye maslahi ya kitaifa. Hapa tunaangalia nani ataweza kulisaidia taifa katika hili.
Mh Zitto Kabwe ameonyesha kulifuatilia kwa karibu suala hili la madini kwahiyo uteuzi wake kwenye kamati hiyo inaonyesha wazi kuwa Mh Rais ana imani naye na zaidi anajua kuwa Kabwe na wajumbe wengine wataifanya kazi hiyo kwa maslahi ya Taifa.
Hii kamati si ya CCM wala CHADEMA. Ni vema basi pale tunaona kuwa maamuzi ya wengi yanatekelezwa hatuna budi kutoa ushirikiano ili suala hili la madini lipatiwe ufumbuzi tuendelee na mambo mengine.
Mimi binafsi ninampongeza Mh. Rais kwa kuunda kamati hiyo na ameonyesha kuwa tanzania ni yetu sote kila mtu ana nafasi ya kuitetea na kuijenga nchi hii.
 
Hivi Kamati ina uwezo wa kuwaapisha mashahidi? Je wao wenyewe wanaapa wanaposhika hizo ofisi kuwa neutral? Kamati Teule ya Bunge inafanya hivyo... ndiyo maana kwenye hili la madini hawakutaka kamati teule!
 
Kalamu hivi unaamini kuwa Kamati ya Rais ina nguvu za Kirais... kwamba kwa vile Rais anaweza kuamuru hivi basi na Kamati aliyoiteua by extension ina uwezo wa kutoa executive orders?

tooooooooooooo much speculations mzee !! why do things always have to go your way ?????????????????????????????? kweli unasikitisha bana saa nyingine !
 
tooooooooooooo much speculations mzee !! why do things always have to go your way ?????????????????????????????? kweli unasikitisha bana saa nyingine !

Hivi unaelewa maana ya neno "speculation"? naona unalirudia rudia sana. Things don't have to go my way, they have to go right and if it takes me or someone else to call it like it then let it be so! Kamati ya Rais haina nguvu za Rais, and that is not speculation it is a pure fact. Kamati inakuwa na nguvu zile tu ambazo Rais anaipa and in this case this committee has no legal power; it can not subpoena any individual or evidence, it can not swear in anybody to tell the truth, the whole truth and nothing but the truth; one can not commit perjury to it, and it can not exercise immunity power because it doesn't have that power; it is a pure advisory committee.. until it becomes a Presidential Commission... now you tell me what power does it have? and I allow you to speculate if you want...
 
hehee, ntakuchokonoa hadi ulewe !

the good think, I just got my new wheel chair; electronic and all fancy and everything.. and because I don't drink sina hofu ya kuanguka.. so I like challenges of the mind.. for they sharpen my intellect...
 
Kesho ni kesho CHADEMA

Na Mwandishi Wetu

MUAFAKA wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, wa kuendelea au kutoendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Kuangalia Upya Mikataba ya Madini nchini, unajulikana kesho.

Kesho ndiyo siku ambayo Kamati Kuu ya CHADEMA inakutana chini ya Mwenyekiti wake, Bw. Freeman Mbowe, kujadili pamoja na mambo mengine, nafasi ya Bw. Zitto katika Kamati hiyo iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zilisema jana kuwa huenda kikao hicho kikatawaliwa na mvutano mkali kutokana na kuibuka pande mbili zinazovutana kuhusiana na ujumbe huo wa Bw. Zitto.

Wakati Bw. Zitto alishatoa msimamo wake kuhusiana na hilo, kuwa haoni sababu ya kujitoa, Bw. Mbowe hajasema lolote, huku muasisi wa chama hicho, Bw. Adwin Mtei, akisimamia upande wa wanaotaka mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini aendelee na ujumbe.

Ingawa kuna wakongwe wengine ndani ya Kamati hiyo, lakini kinachotegemewa katika hili ni busara atakayotumia Mwenyekiti Bw. Mbowe ambaye amekuwa mwangalifu sana katika hili kwa kukaa kimya, kuamua mvutano wa wanaompinga Bw. Zitto na yeye mwenyewe.

Hata hivyo, mmoja wa wanachama wa CHADEMA alisema, kwa kuwa Bw. Mbowe ni mpinzani wa kwelikweli wa Serikali iliyoko madarakani, hajisikii vizuri kumwona Bw. Zitto akiwa katika Kamati iliyoundwa na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.

Habari zinasema kuwa kikao hicho muhimu kwa CHADEMA, kitatawaliwa na wasiwasi baina ya baadhi ya wajumbe, kutokana na kwamba Bw. Zitto ameonekana kuwa mashuhuri zaidi ya chama hicho, hata kuhatarisha ugombea wa viti vya juu kwa baadhi ya viongozi ndani na nje ya chama.

Kugawanyika pande mbili ndani ya CHADEMA kutokana na uteuzi wa Bw. Zitto, kunaweza kuhatarisha mustakabali wa chama hicho, iwapo karata za kesho hazitachezwa vizuri baina ya Bw. Mbowe na Bw. Zitto, kwani ndio wanaoonekana kuwa 'vinara' ndani ya chama hivi sasa, licha ya kuwapo Katibu Mkuu, Dkt. Wilbroad Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lissu.

Zipo tetesi pia kuwa huenda Mwenyekiti wa CHADEMA akamwekea masharti magumu Bw. Zitto, kuhusiana na ujumbe wake na ambayo itakuwa rahisi kukubaliwa kiitifaki na Kamati hiyo.

"Ndiyo, sisi tunaamini kunawezekana kuwekwa masharti magumu ambayo yatakinzana na msimamo na imani ya Bw. Zitto katika kutetea maslahi ya wananchi na hivyo kusababisha ajiondoe ndani ya chama...wako wapi akina Kabourou (Walid), huwezi kujua," alisema Bw. Joachim Malaga, ambaye alijitambulisha kuwa mfuasi wa TLP.

Hata hivyo mtu muhimu katika kikao hicho anayetarajiwa kuweka mambo sawa, ni muasisi wake, Bw. Mtei, ambaye ana ushawishi mkubwa katika chama hicho, kutokana na kwanza na uasisi huo lakini pia na uhusiano wake wa karibu na Mwenyekiti.

Source: Majira.

Kama hizi zinazoitwa tetesi za kuhofia umaarufu wa Zito ndani ya CHADEMA ni za kweli, nina ushauri wa bure kwa wana-CHADEMA. Wawe waangalifu, sana. Wakiendeleza upuuzi huu wataua chama chao sasa hivi, wallahi. Hivi kuna mantiki gani kuita kikao kujadili uteuzi wa Rais, ambao watu wengi tunauona ni wa nia njema? Au walitaka Rais awaombe ruhusa kabla ya kumteua Zito kwenye Kamati hiyo? Ina maana wanahoji madaraka ya Rais kumteua mwananchi wake mmojawapo katika kamati anayotaka ishughulikie maslahi ya nchi? Ni kweli Rais ni mwenyekiti wa CCM, lakini ni Rais wa watanzania wote including hao wa upinzani, na ameamua kutumia nafasi hiyo kupanua wigo wa kuwashirikisha wapinzani katika suala hilo ambalo ni maslahi ya taifa. Kama CHADEMA hawataki hilo wanataka nini? Au ndio wameshavamiwa na kidudu cha "mtafaruku"? Pole yao, nasema pole we!
 
watu walivyokuwa wajinga, watauliza hilo gazeti gani ? afu wakisikia majira wataanza kusema ohh ohh........................
 
Ni vizuri kujihami mapema..... maana hata mmoja wa waananchi aliyeko eneo la Mabibo Bi. Zainab Mtumbuka alisema kuwa "mimi naamini kuwa mipango ilifanywa na CCM ili kuwatibua wapinzani". Mkazi huyo ambaye alijitambulisha kuwa ni mwanachama wa CCM alisema hawezi kushangazwa na hali hiyo kwani CCM imekuwa ikijihusisha na mambo hayo.
 
natamani miti ikuwe niwe na mbao za kutosha !

Kuwa na miti peke yake haitoshi kwani ni lazima uwe na nyenzo za kukata miti hiyo na kuifanya iwe mbao. Hata hivyo utakapoamua kukata mtu kumbuka kupanda mti vinginevyo magogo yatakapokamatwa usianze kulalamika.
 
hayo mambo ya nyenzo baadae, lakini first priority ni kuwa na miti mingi !
 
TAARIFA KWA UMMA

Maoni yangu Binafsi kuhusu Kamati ya Madini iliyoteuliwa na Rais Kikwete

• Napinga Muundo, Mfumo na Mamlaka ya Kamati; nahoji dhamira ya Rais Kikwete
• Sijawahi kupinga, sipingi na sitapinga Zitto Kabwe kuteuliwa kwenye Kamati
• Zitto aingie kwenye Kamati kuendelea kuhoji na kutuwakilisha
• Kupinga Kamati si maslahi binafsi, ni maslahi ya Taifa- kupinga kwa nia ya kitaifa ni uzalendo.
• Gazeti la Mtanzania na Rai nipeni haki ya kunisikiliza; chukueni maoni yangu toka kwangu mwenyewe kuondoa kupotosha na kunichafulia jina.


Toka Rais Kikwete aunde Kamati ya Madini Novemba 13 na kumteua Zitto Kabwe kama mmoja wa wajumbe, sijawahi kujitokeza hadharani kutoa maoni yangu kuhusu suala hilo hata nilipotakiwa kufanya hivyo na vyombo kadhaa vya habari. Nilikwepa kutoa maoni yangu kutokana na sababu mbili: Mosi, tayari nilishatoa maoni yangu kuhusu kamati hii ya Rais toka Novemba 4 mara baada ya Kauli ya Rais katika mkutano mkuu wa CCM. Pili; Mara baada ya Novemba 14 Viongozi mbalimbali wa CHADEMA walikuwa wametoa maoni yao kuhusu suala hili na kwa kiasi wengine maoni yalitofautiana na baadhi ya vyombo vya habari vikatafsiri kuwa ni mgogoro- hivyo sikutaka kuongeza jina langu katika orodha ya watoa maoni kuepusha kuendeleza hisia za kwamba tunamgogoro-nilinyamaza kimya na kuyawasilisha maoni yangu katika vikao vya chama chetu. Hata Novemba 17 ambapo Kurugenzi ya Vijana tuliandaa Kongamano la Wasomi ambapo suala la Kamati hii pia lilijadiliwa, sikutoa maoni yangu yoyote kuhusu hii kamati kwa sababu ambazo nimezieleza.

Hata hivyo, nalazimika kwa shingo upande kuyatoa maoni yangu kwa umma. Sababu mbili zimenisukuma nitoe kauli yangu leo. Mosi, habari za gazeti la Mtanzania ambalo katika matoleo kadhaa ya wiki hii limekuwa likinitaja na mara moja ukurasa wa mbele kwamba napinga Zitto Kabwe kuwepo kwenye Kamati(gazeti limewasilisha kwa niaba yangu kitu ambacho sijakisema) na Gazeti la Rai toleo la Jana(22/11/2007) ambalo si tu limerudia maoni ya gazeti lake dada kwa niaba yangu- bali pia limenihukumu natunguliza mbele maslahi yangu binafsi badala ya maslahi ya Taifa. Katika hali hii ya kutolewa maoni kwa wiki nzima, nikinyamaza wasomaji na watanzania wenzangu wanaweza kudhani kwamba hayo ndiyo maoni yangu. Nimeamua nitoe taarifa hii kutoa wazi maoni yangu. Pili; kikao cha Kamati kuu ya CHADEMA kinakaa kesho Jumamosi 24/11/2007- kwa vyovyote vile, katika kikao hicho chama kitatoka na msimamo mmoja wa chama baada ya kupokea maoni mbalimbali, hivyo baada ya kikao hicho mimi kama kiongozi zitaweza tena kuwa na fursa ya kuwasilisha maoni yangu binafsi kuhusu suala hili. Nitawasilisha msimamo wa chama kama sehemu ya uwajibikaji wa pamoja hivyo sitapata wasaa tena wa kukanusha na kutoa maoni yangu binafsi tofauti na yale yaliyoandikwa na magazeti ya Mtanzania na Rai. Napaswa kusema sasa, ama ninyamaze milele.


Novemba 4, 2007 nilitoa msimamo wangu pale tu Rais alipotangaza kuunda kamati hii- kwa ujumla katika msimamo huo nilihoji dhamira ya Rais kuunda kamati mpya wakati ya Masha aliyoiunda pindi alipoingia madarakani na ikatangazwa kuwa imempatia ripoti yake Septemba 2006 hatujaelezwa ilibaini nini na imeshindwa kubaini nini ili iwe sababu ya kuundwa kwa kamati nyingine. Pia nilisema wazi kwamba wapinzani hawapaswi kunyamaza kwa kuwa tu watahusishwa kwenye kamati, wapinzani wanapaswa kuendelea kutetea maslahi ya taifa popote walipo na umma wa watanzania unapaswa kuendelea na mjadala kuhusu madini na rasilimali zingine za taifa. Na kwa ujumla nilieleza kwamba katika mazingira hayo suala sio kuundwa kwa kamati, suala ni kutekeleza matokeo ya kamati, na suala hili linahitaji kitu kimoja tu- Dhamira ya kisiasa ya kuchukua hatua. Huu ni msimamo wangu ambao sikuhitaji tena kuutolea maoni baada ya Rais kuunda kamati mpya Novemba 13, 2007.

Mara baada ya Rais kuunda Kamati ya Madini na kumteua Zitto Kabwe Novemba 13, (narudia tena)- sijawahi kutoa msimamo wangu kwa chombo chochote cha habari.Kwa waraka huu; nawasilisha rasmi maoni yangu kwa umma kuhusu Rais kuunda Kamati ya madini:

Napinga Muundo, Mfumo na Mamlaka ya Kamati na nahoji dhamira ya Rais Kikwete katika kuunda kamati yenye muundo, mfumo na mamlaka kama kamati hii chini ya Mwenyekiti Jaji Msaafu Mark Bomani. Baadhi ya masuala ya kujiuliza yaliyopelekea niwe na maoni haya nimeyadokeza kwenye ujumbe wangu niliowapatia baadhi ya wahariri Novemba 19 mwaka 2007. Sijawahi kupinga, sipingi na sitapinga Zitto Kabwe kuteuliwa kwenye Kamati. Zitto aingie kwenye Kamati kuendelea kuhoji na kutuwakilisha. Kupinga Kamati si maslahi binafsi, ni maslahi ya Taifa- kupinga kwa nia ya kitaifa ni uzalendo. Gazeti la Mtanzania na Rai nipeni haki ya kunisikiliza; chukueni maoni yangu toka kwangu kuondoa kupotosha na kunichafulia jina.

Kwa maoni yangu: Muundo wa Kamati unazua mjadala- Rais aliahidi kwenye mkutano Mkuu wa CCM kwamba angeunda kamati itakayoshirikisha jamii kwa upana zaidi ikiwemo asasi za kiraia-lakini kamati iliyoundwa imejaa watendaji wa serikali na makada wa chama tawala huku asasi za kiraia zikiwa hazina mwakilishi hata mmoja tofauti na ahadi ya Rais. Katika hotuba yake Rais alizungumzia uwakilishi-lakini katika uteuzi wake Rais amefanya uteuzi wa watu binafsi ingawa wanatoka katika taasisi mbalimbali ikiwemo vyama vya upinzani. Katika Lakini hili ni suala dogo. Kubwa zaidi katika muundo wenyewe ni Rais kuwahusisha baadhi ya wajumbe wenye tuhuma za ufisadi ambazo Rais alikuwa anazifahamu kabisa toka wakati akiwa Waziri katika serikali na wengine wanamgongano wa kimaslahi ambao uko bayana. Kama aliwahujua watu hawa, nini dhamira ya kuwateua? Je, hakuna watanzania wengine ikiwemo toka katika chama chao ambao uadilifu wao hautiliwi mashaka ya kiasi hicho?

Mfumo wa Kamati unazua mjadala-Hadidu rejea za kamati zimetogezwa lakini katika hadidu rejea zilizotajwa masuala ya haki za binadamu katika maeneo ya migodi na ya uchafuzi wa mazingira hayajaguswa. Nini cha pekee ambacho kamati hii itafanya ambacho Kamati ya Masha iliyokamilisha kazi yake mwaka jana haijafanya? Imani yangu ni kuwa suala hili litatazwa vyema- ripoti ya Kamati ya Masha itawekwa wazi kwa umma, Kamati ya Bomani itafanya kazi yake kwa uwazi na kuwa na vikao vya masikilizano na umma(public hearings) na ripoti yote itawekwa wazi kwa umma.

Mamlaka ya Kamati yanaibua mjadala- Uamuzi wa Rais Kikwete kuunda Kamati badala ya Tume unanifanya nihoji dhamira yake. Rais Kikwete anafahamu kabisa kuwa Kamati haina mamlaka ya kutosha ya kuita mashahidi na kuwataka kutoa ushahidi wa kiapo kama ambavyo Tume ya Rais inavyo. Uamuzi wa kuunda Kamati unafanya dhamira ihojiwe, je masuala ya madini ikiwemo sheria na mikataba hayana masuala nyeti yanayohitaji mamlaka ya Tume kuweza kuyafuatilia? Kwa vyovyote vile- kamati ya Jaji Bomani pamoja na kuundwa na Rais kwa mujibu wa sheria za nchi yetu haiwezi kuwa na mamlaka makubwa(executive authority). Kama Rais Kikwete aliweza kuunda tume kadhaa haraka katika kipindi kifupi cha utawala wake, ni vipi suala hili ameacha kuliundia tume na badala yake ameunda kamati? Suala la Mamlaka ni nyeti kwa kuwa ikumbukwe kuwa suala alilolitaka Zitto Kabwe bungeni ni kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge ambayo ni wazi ingekuwa na mamlaka yanayoshabihiana na yale ya Tume ya Rais.

Ukitafakari masuala hayo kiundani utaoana suala la kujadiliwa si kuwepo au kutokuwepo kwa Zitto Kabwe kwenye kamati- Hoja ni Kamati yenyewe na dhamira ya Rais Kikwete katika kuiunda Kamati hiyo. Katika muktadha huo basi; maoni yangu ni kuwa kama serikali haitarekebisha kasoro hizo zilizopo kuhusiana na hiyo kamati, Zitto Kabwe kama mmoja wa wajumbe bado anapaswa kuendelea kushiriki ili kuwasilisha na kuwakilisha fikra mbadala katika kamati hiyo. Zitto akawe hamira ya kuumusha na kuchachusha hoja na mchakato wa kamati ya Bomani. Na kuendelea kumjadili Zitto Kabwe badala ya kuendelea kujadili masuala hayo ni kukwepesha mjadala wa msingi.

Kwa maoni yangu, CHADEMA kama chama cha demokrasia na maendeleo kimefanya uamuzi wa busara mpaka sasa kuruhusu mjadala huu. Maoni tofauti baina ya baadhi ya wanaCHADEMA yamewasaidi kuimulika kamati na kufahamu undani wake- utamaduni huu wa kuhoji na kutoa fikra mbadala ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu na unapaswa kuendeleza. Imenisikitisha kwamba Gazeti la Mtanzania na Rai wamemua wazi kusambaza ujumbe kwamba kwa kuwa na maoni hayo mimi(na wamenitaja kwa jina) kwamba natanguliza maslahi binafsi badala ya maslahi ya Taifa. Na wamehusisha maoni yangu na kuchunguzana nani atagombea urais 2010 kupitia CHADEMA mintaarafu umaarufu wa Mbowe na Zitto. Kwa maoni yangu, huu ni mkakati mwingine wa wakagawe uwatawale (divide and rule); haya mambo ya Urais yanatoka wapi tena wakati Zitto hata miaka 40 ya kugombea Urais atakuwa hajafikisha wakati huo? Bahati njema, naamini viongozi wa CHADEMA hawawezi kuchonganishwa na habari za magazetini.

Kwa maoni yangu mimi, hoja zote zinatetea maslahi ya taifa na ni za kizalendo. Wanaotaka kamati iwe na muundo, mfumo mzuri na mamlaka zaidi wanatetea maslahi ya taifa na ni wazelendo kama ambavyo wenye mtizamo tofauti nao ni wazalendo. Ni kupitia fikra hizi mbadala ndipo tunapata kilichobora zaidi na kukiendea kama taifa. Hivyo, kama ambavyo itikadi ya CHADEMA inaamini katika siasa zilizojuu ya vyama zinazosimamia ziadi maslahi ya taifa. Hivyo hivyo, wanaopinga muundo, mfumo na mamlaka ya kamati, hawafanyi hivyo kwa manufaa ya kisiasa ya CHADEMA, wanataka CHADEMA itumike kama chombo tu cha kutumika kusimamia fikra hizi mbadala na matokeo yoyote mazuri ya fikra hizi yatasimamia rasilimali za taifa na matokeo yale yatanufaisha watanzania wote bila kujali itikadi. Wazalendo hawakai kimya wanapoona jambo lolote katika taifa lao linakwenda tofauti na hoja zao ama za makundi ya kijamii ambayo wanayawakilisha. Maoni ya pande zote ni mazuri kufanya watchdog function kwa kamati; kwa mfano mijadala kama hii inaweza kupelekea kamati kuacha kufanya kazi kwa kificho; kamati kufanya kazi kwa undani zaidi na pengine hata kufanya matokeo ya Kamati hii kutekelezwa kwa sababu ya ufuatuliaji wa karibu wa wa vyombo vya habari na umma. Mambo haya ni muhimu yakajadiliwa wakati kamati inaendelea kufanya kazi kwa sababu kazi ya kamati miezi mitatu inagharamiwa na walipa kodi watanzania; fedha hizi zingeweza kutumika kujenga madarasa- hivyo kama kamati haitafanya kazi kwa kadiri ya matakwa ya umma matokeo yake ni hasara kwa taifa kwa ujumla bila kujali itikadi. Ifahamike mjadala kuhusu ufisadi na hatma ya rasilimali za Tanzania ni suala pana kuliko Kamati ya Bomani. Nikumbushe kauli niliyoitoa mwaka 2005 wakati wa uchaguzi- “Tanzania ni yetu sote; SIASA SIO UADUI”.

Naamini Kamati kuu ya kesho baada ya kupokea maoni mbalimbali italipokea na kulitolea msimamo wa chama suala hili na PAMOJA TUTAFIKA.

Nautoa waraka huu leo Ijumaa 23 Novemba mwaka 2007:


John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa(CHADEMA)
0754694553
mnyika@yahoo.com

PS: Natarajia Gazeti la Mtanzania la 24/11/2007 na Gazeti la Rai la Wiki ijayo mtachapa maoni yangu kama sehemu ya maadili ya vyombo vya habari ya kutoa fursa kwa mhusika kutoa maoni yake kabla ya kuandika habari inayomhusu. Naamini mtachapa ufafanuzi wangu kuhusu suala hili.


Kwa maelezo zaidi na rejea(tazama viambatanisho):

Sehemu ndogo ya maoni yangu ya 4 Novemba 2007 Kama yalivyonukuliwa Na Tanzania Daima 5 Novemba, 2007(maoni baada ya Mkutano Mkuu wa CCM)

Ujumbe kwa baadhi ya Wahariri nilioutoa 19 Novemba, 2007
 

Attachments

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom