Nono
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 1,543
- 661
Nono,
Ninazidi kusema, hebu sisi tuna vichwa gani hivi tusiosikia hata tukiguswa na Muumba wetu?
Ni lini tutatumia akili kidogo ili kukabiliana na changa moto zilizo mbele yetu?
Hebu kweli sisi watanzania ni Mazezeta kiasi hiki jamani?
Tusipoangalia tutaendelea kuwasindikiza CCM mpaka tutakapozikwa hiki kizazi, haiwezekani tukose mikakati na maandalizi ya 2010, tunazidi kupiga soga na wakati unazidi kusonga
Maswari ya kujiuliza :
(a) Ni kweli tumejiandaa 2010 kupambana na hawa Mafisadi CCM?
(B) Watanzania watakuwa tayari kuumpa M/kiti wetu kura ili aiongoze inchi hii? na kwa kuwa hawa mafisadi wameanza kampeni za kumchafua, ni kwa nini tusiwe na mkakati ndani ya chama kwa maslahi ya Taifa?
Ninazidi kusema, upenzi na ushabiki usiozingatia Maslahi ya Taifa ni jambo la kipuuzi sana, tunaomba watanzania wenzetu tuwe na mikakati ya 2010, hii ni pamoja na kuwapata wabunge wa upinzani wa kutosha.
Naomba mtambue hivi, CCM mikakati yao ni kuona wanayarudisha Majimbo yote ya Upinzani huku Tanzania bara, na hiyo ndiyo itapelekea kuua upinzani, tutie akili jamani.
Lakini naona kama ajenda yako ikowazi nayo ni kuiangamiza CHADEMA. Sio kweli kuwa una mikakati yakuipatia ushindi. Kwani CHADEMA imefikia hapa ilipo wakati gani?
Maslahi ya taifa unayozungumzia ni yepi? ni ya kuififisha CHADEMA, ili CCM ikose mtu wa kuikosoa na kuihoji. Vyama vinavyoitwa vya siasa Tanzania vipo vingi.
Mimi nadhani ungekuwa na hoja za msingi zingeweza kujadilika kuliko ajenda imbayo unaitumia kama vile unazungumzia maslahi ya mageuzi Tanzania kumbe kuyadhoofisha.
Mbowe kama binadamu kama wewe anamapungufu yake na pia ana strength zake, na siku zote watu wanapimwa kwa weekness zao na stregth zao. Kwanini Mbowe leo aonekane kuwa kiongozi asiyetakiwa kwenye Mageuzi wakati huu ambapo CHADEMA wanaendelea kupata nguvu na kukubalika zaidi. Kwani Mbowe ameshika nafasi ya Mwenyekiti kwa kipindi kirefu kuliko nani kati viongozi wa vyama vya siasa, achilia mbali Kikwete. Tangu amepokea CHADEMA, ni mafanikio gani yaliyoonekana.
Ndio maana nikasema katika post iliyopita kuwa naamini kuwa CHADEMA kama chama watayatafakari misukosuko kama hii unayojaribu kuudanga umma ndani ya vikao vyao, lakini sio kuja kutafuta kuungwa mkono kwa hoja isiyokuwa na nguvu kwa maslahi ambayo yako dhahiri kuwa ni against CHADEMA.
Naamini Mbowe hana sababu yoyote ya kujiuzulu. Muda wake ukiisha vikao halali vya chama vitampima kama anafaa kuendelea na kama mwenyewe atakuwa ameomba, lakini sio kwa kupandikiziwa chuki za kuidhoofisha CHADEMA. Ndio mimi sio mwanachama wa CHADEMA lakini mtizamo wangu katika mada yako ni kuwa unamikakati ile ile ya kuisukasuka ili iporomoke kisiasa.