the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara kimetangaza msimamo wake wa kutoshiriki uchaguzi hadi pale masuala kadhaa yahusuyo haki na usawa wa uchaguzi yatakapotatuliwa.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Mashauriano la Chadema Mkoa wa Mara kilichofanyika wilayani Butiama, Mwenyekiti wa CHADEMA wa mkoa huo, Chacha Heche, amesisitiza kuwa chama hakina imani na mfumo wa sasa wa uchaguzi, ambao amedai umejaa upendeleo na ukiukwaji wa haki za wagombea.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
"Kwa azimio hili, tumejiridhisha pasina shaka kwamba tukienda kwenye uchaguzi tutaenda kupoteza watu. Kabla polisi hawajatuambia kwanini wanawapa watu kesi kwenye uchaguzi, hatutaenda kwenye uchaguzi," amesema Heche.
Ameongeza kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ni wasimamizi wa uchaguzi wamekuwa wakiwabagua wagombea wa CHADEMA kwa kuwaengua majina yao bila sababu za msingi, hali inayosababisha hasira kwa wananchi na hata vurugu.
"Kabla Wakurugenzi hawajatuambia ni kwanini wanaengua watu wetu majina na kusababisha mpaka watu wanakasirika na kutembea na mapanga, ni kwanini twende kwenye huo uchaguzi?" amehoji.
Kutokana na hali hiyo, Heche amesema kuwa CHADEMA Mara inasimamia kauli mbiu ya "No Reform, No Election", ikisisitiza kuwa bila marekebisho ya msingi katika mfumo wa uchaguzi, chama hakitashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.