CHADEMA maridhiano yenu na CCM yanadhoofisha mchakato wa kudai Katiba Mpya

Wewe uliona wapi Kikosi Kazi cha Prof Mkandala kinadai katiba kivyake na Mbowe anadai kivyake na Wote wako chini ya Mwenyekiti wa CCM [emoji1][emoji1][emoji1]
Acha UONGO hilo halikuwa Jukumu la Mkandala punguza ujuaji
 
CCM wala haijaridhiana na CHADEMA.

Ni Rais Samia pekee yake labda ndiye karidhiana nao.

Ikitokea Samia siyo Mwenyekiti wa CCM leo, hakuna mwanaCCM anayeyatambua.

Maalim Seif aliporidhiana na Karume 2009,paliundwa kamati ya Maridhiano chaired na Mzee Moyo,Hoja binafsi ikapelekwa baraza la wawakilishi Jan 2010 na Abubakar Khamis Bakari (CUF) iliyopendekeza SUK,VPs wawili na mgawanyo wa nafasi za uwaziri.

Seif hayupo na Karume yupo benchi lakini maridhiano yapo.
 
Siamini na sikubaliani kuwa suluhisho la matatizo ya utawala wa nchi hii na utendaji kazi wa watawala ni mapungufu katika Katiba. Tatizo ni usimamizi wa Katiba, Sheria, Kanuni na Taratibu kwa dhati na uzalendo.

Watawala karibu wote hawana utashi wa kisiasa na wengi wao ni wanasiasa maslahi na ndio hao wanaaminisha wananchi kuwa tatizo ni Katiba. Awamu ya Tano walidai Demokrasia kwa kuwa milango ya maslahi yao ilifungwa wakituhumu utawala wa kidikteta
 
Kwanini maridhiano ya Chadema na CCM yawazuie wengine kuidai Katiba Mpya?

Mnaonesha vile mlivyoweka matumaini yenu yote kwa Chadema, huu ndio wakati wenu kuamka, kwasababu hiyo Katiba Mpya haitakuwa ya Chadema peke yao.
Exactly mkuu why utegemee watu wengine wakupiganie?,fight back kwa haki yako ,kama unaona unahitaji katiba mpya ,pigana usitegemee wengine wakupiganie otherwise shut up, miaka kibao iliyopita huko Nordic country mwanamke mmoja alipanda farasi uchi hadi katikati ya market ili kuwapigania wakazi wasipandishiwe kodi, na respects alizopata wakazi walijipanga barabarani na macho yao chini, hadi leo kuna sanamu yake na kodi haikupanda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…