PreGE2025 CHADEMA Mbeya washiriki Ibaba kumuombea Mdude Nyagali, wadai ukimya wa kutoweka kwake haukubaliki

PreGE2025 CHADEMA Mbeya washiriki Ibaba kumuombea Mdude Nyagali, wadai ukimya wa kutoweka kwake haukubaliki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Viongozi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya, Jana Jumapili Mei 11,2025 wameshiriki ibada maalum ya maombi kumuombea mwanachama na mwanaharakati Mpaluka Saidi Nyagali maarufu kama “Mdude” ambaye hajulikani alipo tangu alipovamiwa nyumbani kwake Iwambi na kupelekwa kusikojulikana Mei 2, 2025.

Ibada hiyo imefanyika katika moja ya kanisa jijini Mbeya, lakini jina la kanisa hilo limehifadhiwa kwa mujibu wa masharti ya kibali walichopewa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Baada ya ibada, viongozi na wanachama hao wa CHADEMA walikusanyika katika kambi maalum iliyowekwa kwenye Ofisi za chama hicho Kanda ya Nyasa, wakisisitiza kuwa wanahitaji majibu juu ya kupotea kwa Mdude wakiwa na matumaini ya kumpata akiwa hai, lakini pia wakiwa tayari kukabiliana na ukweli wowote.

"Tunahitaji kujua alipo Mdude. Yu hai au amepoteza maisha, lakini tusipate ukimya." Alisema mwanachama moja.

Kimya SIku ya 19 ,Si TLS Mwabukusi,Si Mwenyekiti wa kanda ,Si wanachadema wakimpambania Sumu ya nyigu....Wanaharakati ndiyo muone kwamba hakuna atakayekupigania sako kwa bako ,aliokuwa anawapambania wote wamekaa kimya sasa wanafanya mambo yao....inayoteseka kwasasa ni familia ya Mdude.
 
Watajiju.
 
Watajiju.

Ben Saanane -> Soka --> Mdude.

Siasa za kiharakari ni hatari sana kwasasa kwa Bavicha ambao hawapo vizuri kiuchumi kuweza kuwa na nyumba za kisasa zenye ulinzi 24/7(CCTV+Electric Fense) ,kutembea na walinzi muda wote ,kuweza kumiliki BOMBA aka mguu wa kuku kwa ajili ya kujihami in case of anything.
 
Back
Top Bottom