Uchaguzi 2020 CHADEMA mfungeni Speed Governor Boniface Jacob

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Kuna tatizo kubwa lipo kwa mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo Mh.Boniface Jacob.
Siasa za upinzani sio za kushambuliana wenyewe kwa wenyewe, lakini anachofanya huyu kitapelekea tatizo kubwa kwa vyma hivi viwili CHADEMA na ACT.

Kwanza kabisa, kuwekewa pingamizi sio kosa bali ni utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria.
Pili, mbali na kuwa wote yeye Boni na Renatus pamba ni wapinzani, lakini wanaweza kuwa na matatizo yao wenyewe binafsi .

Boniface Jacob anakituhumu chama cha ACT kumuewekea pingamizi lakini anasahau kuwa hata kule jimbo la isimani mgombea wa CHADEMA Mh. Ole Sosopi amemuwekea pingamizi mgombea wa ACT ila hakuna sehemu ACT wamekishutumu chama cha CHADEMA.

Hivyo ni wazi ndugu Boni Jacob ana siasa ambazo hazina ustaarabu ndani yake dhidi ya wengine.
Wemgi mtakumbuka kipindi mchakato wa kura za maoni jimbo la Ubungo hali ilivyokuwa na kupelekea wanachama wengi kufukuzwa sababu tu walikuwa hawamuungi mkono huyi Boni Jacob.

Anasahau kuwa haiwezekani kila mwanachama akuunge mkono. Ndugu Boni Jacob akafanya kila namna ya kufukuzwa uanachama hawa watu. CHADEMA linisuru jimbo la Ubungo kwa kukaa chini na huyu jamaa aache siasa anazokwenda nazo.
 
Jacob haibiwi kura na huyo ndie mbunge mpya wa Ubungo, wacheni kelele zenu.
 
Good advice hope watafanyia kazi.

"YUNAJENGA NYUMBA MOJA TUSIGOMBANIE FITO"
 
Mnaumana wenyewe baadae mseme ooh tumeibiwa form ooh tunaonewa yaani miaka 5 hamjiandai na lolote mnakalia majungu uchaguzi ukija mnalalama na Amsterdam and Partners mwaka huu mtakua na madiwani 14 na mbunge 1 ha ha haaa
 
zaidi ya kulalamika sijaona hoja yako , kwani wewe ndio Renatus ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…