Uchaguzi 2020 CHADEMA mkimsimamisha Lissu najiunga na chama chenu

Natamani sana ningekuwa na muda na akili imetulia tujadili mkuu, maanake naona una mambo kadhaa ya muhimu sana kuyajadili.

Bahati mbaya sina muda na akili tulivu kwa sasa hivi.

Lakini nimeona jambo moja lililonishangaza kidogo kukuhusu wewe:

CCM ilianza kukuharibikia 2016?

Una maana zile CCM za akina Mwinyi, Kikwete zilikuwa sawa na ile CCM ya 1978 uliyojiunga nayo?

Nikubali, ni dhahiri CCM ya Magufuli ni tofauti na hizo za akina Mwinyi/Kikwete, lakini utofauti wao haufanyi pawepo na unafuu kati ya hizo CCM.

Kwa hiyo wewe unajitambulisha kuwa ni CCM "Huyu ni Mwenzetu?" Nikiri, kuna unafuu wa aina fulani kwa hiyo CCM kuliko hii aliyojibinafsishia Magufuli.

Mwisho, niungane nawe kuhusu Tundu Lissu au mgombea mwingine yeyote mbali ya kumrudisha miaka mitano mingine Magufuli.
 
Sijui kwanini huwa nakereka Sana na propaganda dhaifu namna hii.
 
Na sio Mimi pekee, wenye kadi wengi za ccm lakini ni watumishi wa umma, wastaafu, wanafunzi na vijana wasomi walio maliza elimu za juu bila serikali hii kuwajali hakika KURA ZOTE KWA LISSU
Itashangaza sana hawa uliowataja hapa wakienda kupiga kura kuendeleza yaliyowapata miaka hii mitano kwa miaka mingine mitano au zaidi!

Nadhani hata kuku na mtama, kuna wakati akili itamtuma kujua kuna hatari juu ya maisha yake.
 
N
Naunga mkono hoja,Mh.Lissu for Presidency.Huyu ni aina ya Viongozi wabobevu na mwenye unyenyekevu lakini thabiti na imara katika maamuzi ya haki.Tunamhitaji kuja kuponya majeraha iliyoyapata Tanzania baada ya 5th Regimen kuingia madarakani kama alivyoyatibu matundu ya risasi >16.
Watanzania wengi wanamsubiri Mh.Lissu waonyeshe uwezo wa kura zao kwa mtu sahihi.Tukihitaji kuiondoa CCM madarakani ,mgombea wa Upinzani awe Mh.Lissu na wapinzani wote wa kweli wamuunge mkono.Wizi wa kura hauwezi kushindana na nguvu ya umma hata siku moja.CCM wamejipanga kushinda uchaguzi kwa kishindo wakitumia mbinu chafu kwa kutumia vyombo vya umma kama NEC,POLICE,TISS nk.Hawana hata haja ya kuwabembeleza wapiga kura bali wanawamuru cha kufanya.Aina hii ya demokrasia inapatikana Tanzania tu,wanaamini Watanzania ni wajinga?
Kila kura inatakiwa kuthaminiwa,tuachwe tuongee kupitia kura zetu na chaguo la wananchi liheshimiwe katika ngazi zote za uongozi na Mh.Lissu ni chaguo sahihi.
 
Mshangai
Umenena vyema.......

Yafaa Umma wa watanzania wakuunge mkono, ili tuuondoe utawala huu wa mkono wa chuma, ambao umeleta mgawanyiko mkubwa kwa Taifa, kutokana na siasa za ubaguzi na kujaa chuki miongoni ya wananchi
 
Mimi huu mwaka napiga kura kwa lissu for the first time.

Sijawahi piga kura.

Eeh, Mungu jibu maombi Tundu Lissu awe Rais wa jamuhuri ya muungano Tanzania. Amen!
 
Ni kuchanganyikiwa kudhani Lissu anaweza shinda uchaguzi haahaha
 
Hakuna wa kumlinganisha na Dr slaa hapo chadema kwa Sasa, alisimamia ukweli aliouamini na misingi ya chama hadi pale wenzake wote walipomsaliti kwasababu ya matumbo yao
Kama alisimamia ukweli vipi alipokosa nafasi ya kugombea tena akaukana huo ukweli?
Huwezi kuwa kuwa Alhaji lakini ukikosa ushehe wa msikiti ukaanza kufakamia kitimoto.
 
Nakushukuru sana kwa kunielewa. Ukipata nafasi njoo tujadili tuu kistaarabu kama nikuonavyo Mara kwa Mara ukijadili kwa hoja nzito.
Labda kwa kifupi nijibu tuu kuwa wakati wetu wa JK kwenda nyuma CCM ilikuwa chama na kama tulifanya mazuri au mabaya kwa kweli ni yetu sote kwani yalikuwa maamuzi ya vikao. Hiyo ni tofauti na sasa hakuna maamuzi ya pamoja Bali amri na ubabe tuu.
Mkuu hata haya maamuzi ya sasa ya so called "wajumbe" nikama salamu kwa mwenyekiti kuwa wanachama haturidhiki na maamuzi yake.
Anyway, ukiwa na nafasi tutajadili kwa undani jambo hili. Lakini kwanza mpeni bendera Lissu apeperushe alete mabadiliko
 
Lakini kwanza mpeni bendera Lissu apeperushe alete mabadiliko
Nilichepuka kidogo, nikarudi, nikakuta bado upo, na michepuko yangu inaendelea, sijatulia.

Ni hivi: tofauti ninayoiona kati yako na mimi ni hii moja tu, ambayo kwa bahati mbaya hujanitambua niko wapi, kutokana na mstari huo ulioweka hapo.
Siambatani na chama kama ulivyoambatana na CCM wewe. Mwambata wangu pekee na wa kudumu ni Tanzania pekee. Hiyo ndio tofauti yangu na wewe.
Niliwahi kuambatana sana na CCM wakati fulani pamoja na kwamba sikuwa mwanachama. Sasa hivi natamani wapinzani, bila kujali Lissu yupo au hayupo, watusaidie kutuondolea hili zimwi ambalo linajigeuza kiasi kwamba linataka hata kuzuia njia ya kuliondoa. Hii itakuwa balaa kubwa kwetu.

Wapinzani wakiingia, miaka mitano wakivuruga, watakuwa hawajajiimarisha hadi waweze kutuzuia kuwaondoa tukiamua kufanya hivyo.
Hiyo ni tofauti kubwa sana na kuiacha hii CCM ya mtu mmoja kuendelea kujiimarisha kutunyonga.
 
Nchi gani umewahi kuona ina rais mlemavu.?
Hakuna kazi katika private company shareholders wanaweza kumpa u-MD mtu kama Lissu.
Taifa lina watu mil 60 hakuna mwenye uwezo wa kuongoza mpaka tumpe mtu ambaye atakuwa anashinda kitandani?
Ungejuwa kuwa mwenyekiti wetu ni kilema zaidi ya kawaida nadhani usinge kufuru hivyo unavyo kufuru.
Wajua kwa nini hawezi kupiga picha za x-ray au Ultra sound?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…