Uchaguzi 2020 CHADEMA mkimsimamisha Lissu najiunga na chama chenu

Mkuu Kalamu1 sio kuwa sijakuelewa unamaanisha nini. Ni hivi hata mie naamini katika Utanzania lakini tambua kuwa bado ni mwanachama wa CCM na kama tungesimamisha mtu makini na mwenye kujali utu na kusikiliza ushauri pengine hata hii mada nisingeandika.
Kama chama, nakubali CCM tulifanya makosa mengi huko nyuma lakini tulikuwa twaweza kukaa na kujadili wenyewe na hata wakati mwingine Rais aliwaita think tank wa upinzani kubadilishana mawazo.
Hakupata MTU kushambuliwa kimwili au kupotezwa. Lakini why Lissu? Kwa vile ndiye pekee anayeonekana anaweza leta mabadiliko, kuheshimu katiba, kutokuwa na visasi au chuki. Wengine ni yaleyale tuu na twaweza kurudi nyuma kwa kasi zaidi
 
 
Huko CCM kungekuwepo hata robo tu ya watu wa msimamo kama wako, taifa letu lisingekuwa na hatihati yoyote wakati huu.

Acha tusubiri kuona itakuwaje.
 
Mko wangapi kwanza? lol
Sina shaka wapo wengi sana huko CCM wakati huu kama huyu ndugu.

Tatizo ni moja tu, maslahi binafsi yanayotokana na kuwa ndani ya CCM ---, bila CCM watakula wapi!

Lakini ukiniambia sasa hivi kwamba mtu kama Kinana, mtu kama Warioba, Butiku, na hata akina Kikwete siku ya siku hiyo Oktoba watatoka kwa moyo mkunjufu na wafuraha kabisa kwenda kuipigia kura CCM iendeleze haya yaliyoonekana tokea 2015, itakuwa vigumu kwangu kukuamini mkuu 'Rebecca.'

Hali ipo hivyo, wengi watafumba tu macho na kusema, watafanyaje?
 
Kwa misimamo hii ya baadhi ya wanaccm Nina mashaka sana na ugumu wa kampeni kwa Magu utakavyo kuwa.
Kuna maasi makubwa sana ndani ya ccm, "wajumbe" wametuonyesha kuwa yale atakayo magu sio wayakayo wanaccm na wamemfundisha maana ya neno KA-TAA
 
Inasikitisha sana kusikia mtu aliyesababishiwa ulemavu kwa makusudi. akitolewa lugha chafu na mtu ambae hata hajawah kupitia changamoto kwenye familia yake...tl for president
 
hakika umeongea vyema. nakuunga mkono
 
Kwa wale wanaccm wanaojitambua, Leo mchakato wa kuwapatia mumpendae unaanza. Tutawapeni Lissu kwa ajili ya kura zenu.
MUHIMU;
Huna haja eti ya kutafuta kadi ya Chadema, kitambulisho chako cha mpiga kura tuu kinatosha kukuletea maisha bora yasiyo na mashaka kama ya sasa kwa kumnyima Jiwe kura.
Kura zinapokuwa nyingi za kumkataa hata mbinu za kuiba zinakuwa ngumu mno
 
Nadhani Chadema wakimuweka Lissu, uchaguzi wa mwaka huu utakuwa mkali kuliko ule wa 2015. Kwa sababu, uchaguzi uliopita watu walikuwa hawajamjua vzr kiongozi aliyepo sasa na style yake ya uongozi, ila kwa sasa jinsi watu walivyochapika kazi itakuwepo. Pia Tundu Lissu ni mtu ambaye hana kashafa yeyote ikiwemo usaliti. Ni mtu ambaye amejipambanua kwa wengi kama ni mtetea umma na msema kweli asiyependa uonevu na mtetezi wa katiba na sheria. Pia kinachotia chachu ziaidi ni uwezo mkubwa wa kujieleza na kujenga hoja kitu ambacho Mzee Lowasa mwaka 2015 hakuwa nacho kabisa. Maana ilifika mahali Lowasa hata kusimama na kusema sentensi 5 ilikuwa ni shida. Yeye aliishia tu kusema "wangapi watanipa kura? Asanteni".

.. Nawasihi na Kuwaomba sn Chadema, wananchi wapo tayar na wanahitaji mabadiriko ya kweli, Tundulisu ni mwenzenu na mpambanaji wa miaka mingi na hajawahi kukisaliti chama na mnajua uwezo wake. Mtaji wa siasa ni watu na uwezo wa kuwashawshi na wala sio pesa. Msiache mbachao kwa msala upitao. Hao waliotoka CCM, wameangalia tu fursa kwamba kwa vile kule wameharibu au kutimuliwa basi wameona huku ndio kimbilio. Kama wasingefukuzwa au kuharibu kule, leo bado wangekuwa CCM na wangeendelea Kukiponda Chadema. Ni muhimu waendelee kujifunza. Na ndio maana msipowapa tu nafasi wanatudi walipotoka. Mjifunze kwa yaliyopita uchaguzi wa 2015. Mpeni nafasi hiyo Tundu Lissu kwa sasa. Macho na maskio yao yote ya watz yapo kwake. Nyarandu hana mvuto alionao Lissu kwa sasa. Pia naomba niwashauri kuangalia mazingira ya kuungana na vyama vingine makini mfanye kampeni za pamoja. Huu mwaka mzuri.
 
kwa kauli hii na uandishi huu mkuu nami niseme sijawi kua na chama but for the first time naweza chukua kadi ya chadema mda wowote ngoja nimuombe roho mtakatifu aniongoze kwa hili ,balikiwa sana mkuu
 
Mleta Ni like Chadema time la siku nyingi nalijua hili .Mada zake nyingi Ni za kusifia Chadema sio chama kingine kiwe CCM au chochote
Amewahadaa watu sana kwa post hii huyu mchadema. Lakini kwangu ni big NO. Maandishi ya wanachadema wote yanafanana. Kwa maana hiyo basi akawahadae wasiojielewa na propaganda zake za kizamani. Mtoa Mada ni Lichadema la miaka yote. Na halijawahi kuwa CCM ...
 
Karibu Ndugu Mshangai huku chadema ni raha tupu tunakula pesa za haki. Hatutegemei kuroga? Kuteka au kuua kujiongezea kipato na madaraka. Huku wanachama na viongozi never regret their actions.

Tundu Lissu ndio Chaguo la watanzania kwa sasa. Ukubali ukatae huo ndio ukweli. Hata vyombo vya ulinzi na usalama vinajua hilo.
 
Mkuu hilo lipo wazi na Hesabu kuwa limetimia kwa mh Lissu kuwa mpeperusha bendera wa cdm, maana tunajua kuwa yeye ndiye kiongozi anaye kubalika hapa nchini kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…